Ninatangaza msiba,mama amenitoka

Ninatangaza msiba,mama amenitoka

Yakuonea

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
601
Reaction score
277
Kwa jina lake manani, muumba wa vyote vitu
Mola aso mfanani, halinganishwi na mtu
Amenipa mtihani, na leo si mali kitu
NINATANGAZA MSIBA , MAMA AMENITOKA

Kwa 'kwikwi' najililia, msiba umenipata
Sina pakushikilia, nimejawa na matata
Mama katoka dunia, ni wapi nitakamata
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Machozi yabubujika, nimejawa na huzuni
Mama alivyofutika, ni kama niko ndotoni
Uhai umezimika, na sasa mimi ni duni
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Maradhi yalimwandama, akawa yu kitandani
Akakosa raha mama, Afya ikawa tabuni
wanawe tulishikana, kujua chanzo ni nini
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Sukari ikawa juu, kifua kilimbana
Akavimba na miguu, Dawa zilishindikana
Pumzi ikakata puu, kaitwa kwa maulana
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Alikuwa ni rafiki, na mengi aliusia
Nisipende unafiki, na maovu ya dunia
Dunia ina mikiki, ni vyema kuzingatia
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Nishikane na ibada, mama alisisitiza
Niheshimu wangu dada, nisipende kujikweza
Leo sina msaada, mwenzenu mie nawaza
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Ewe mola rahmani, msitiri mama yangu
Atulie kaburini, asipatwe na machungu
Muepushe ya motoni, mpe mema kwa mafungu
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Na hapa ninasimama, moyoni bado nalia
Kaondoka wangu mama, naona chungu dunia
siwezi hata kusema, unyonge umezidia
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA


"INNA LILAH WAINNA ILAYH RAJ'UUN"


NYOTE NAWASHUKURUNI

Pole nimezipokea, mama nimesha mzika
Kwa mola amerejea, kaenda kupumzika
Na dua namuombea, alindwe na malaika
NYOTE NAWASHUKURUNI, MAMA NIMESHAMZIKA

Ni kubwa pengo la mama, na katu halizibiki
Vitabuni ukisoma, navyo pia vyaafiki
Mama ni mwongozo mwema, "wemae" haupimiki
NYOTE NAWASHUKURUNI, MAMA NIMESHAMZIKA

Kuna walionibeza, sijui hata kwa nini
Mama nimepoteza, wao waleta utani
Ni jambo la kushangaza, mwanibeza nimsibani
NYOTE NAWASHUKURUNI, MAMA NIMESHAMZIKA

Vipi mwakosa huruma, mahoka wanifanyia
mwanijaza na shutuma, eti kifo nazulia
Mola awape hekima,dunia tunapitia
NYOTE NAWASHUKURUNI, MAMA NIMESHAMZIKA

Dua zangu nazituma, ewe mola zipokee
mama mpe huruma, adhabu muondolee
mwanae nipe hekima, na busara za pekee
NYOTE NAWASHUKURUNI, MAMA NIMESHAMZIKA

"INNA LILAH WAINNA ILAYH RAJ'UUN"
 
Ukitoka hapo kapige picha na kikwete ikulu, usisahau kutoa na shukrani.
 
PAMOJA TUNALIA

Nalia nawe pamoja,mama tukimlilia,
Ni msiba sio hoja,jamvini metufikia,
Msiba si wa mmoja,wote tunamlilia,
Pamoja twamlilia,mama yako wetu sote.

La msingi zingatia,wosia lokuachia,
Malezi alokulea,mema yote shikilia,
Japo bado unalia,hekimaze zingatia,
Pamoja twamlilia,mama yako wetu sote.

Kilio sipitilize,kufuru ikaingia,
Muumba si mchukize,ya kwake kuingilia,
Na nduguzo uwajuze,majonzi kuvumilia,
Pamoja twamlilia,mama yako wetu sote.


Eehe Yakuonea,nadhani umeelewa,
Machungu we vumilia,huzuni usijelewa,
Mama katutangulia,wote hilo twaelewa,
Hebu jikaze KIUME,upya maisha upange.
 
Ukitoka hapo kapige picha na kikwete ikulu, usisahau kutoa na shukrani.

Deno AROBAINATISA,maswali najiuliza,
Mbona kama una visa,kwa mwenzio nauliza?
Au kunao mkasa,nimeliingia giza?
Hakika mi sielewi,hebu nifumbue macho!

 
mama kweli amekufa,
au mwapenda misifa,
si vizuri kusema kafa,
wakati mama hajafa.

mwaturusha roho zetu,
mwachezea akili zetu,
turudishie raha zetu,
soma desturi zetu.

mod ingia kazini,
tia huuzi kapuni,
anatutia huzuni,
piga ban ale ban.
 
PAMOJA TUNALIA

Nalia nawe pamoja,mama tukimlilia,
Ni msiba sio hoja,jamvini metufikia,
Msiba si wa mmoja,wote tunamlilia,
Pamoja twamlilia,mama yako wetu sote.

La msingi zingatia,wosia lokuachia,
Malezi alokulea,mema yote shikilia,
Japo bado unalia,hekimaze zingatia,
Pamoja twamlilia,mama yako wetu sote.

Kilio sipitilize,kufuru ikaingia,
Muumba si mchukize,ya kwake kuingilia,
Na nduguzo uwajuze,majonzi kuvumilia,
Pamoja twamlilia,mama yako wetu sote.


Eehe Yakuonea,nadhani umeelewa,
Machungu we vumilia,huzuni usijelewa,
Mama katutangulia,wote hilo twaelewa,
Hebu jikaze KIUME,upya maisha upange.

Ninashukuru ndugu, sote safari yetu ni moja. . . , .
 
mama kweli amekufa,
au mwapenda misifa,
si vizuri kusema kafa,
wakati mama hajafa.

mwaturusha roho zetu,
mwachezea akili zetu,
turudishie raha zetu,
soma desturi zetu.

mod ingia kazini,
tia huuzi kapuni,
anatutia huzuni,
piga ban ale ban.

katika mitihani inayoweza kumkumba mwanadamu mmoja wapo ni pindi akikabiliwa na kifo, na hili ndio lilionikuta mimi,kusema nimefikwa na msiba sidhani kama eti ninataka sifa kama unavyosema au nastahili ban
 
.., ndugu hapa kuna nini? Naona mashairi' ya miminwa' kama mvua za masika' naomba mtuweke wazi' tuweze toa zetu rambi rambi'
 
Naja kumimina pole,kwa mja aliyefiwa.
Omba peponi alale, kaburi likifukiwa.
walofiwa wako tele, kufiwa si kuonewa.
ila uwe na subira, mama kaenda kulala.
 
Kwa jina lake manani, muumba wa vyote vitu
Mola aso mfanani, halinganishwi na mtu
Amenipa mtihani, na leo si mali kitu
NINATANGAZA MSIBA , MAMA AMENITOKA

Kwa 'kwikwi' najililia, msiba umenipata
Sina pakushikilia, nimejawa na matata
Mama katoka dunia, ni wapi nitakamata
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Machozi yabubujika, nimejawa na huzuni
Mama alivyofutika, ni kama niko ndotoni
Uhai umezimika, na sasa mimi ni duni
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Maradhi yalimwandama, akawa yu kitandani
Akakosa raha mama, Afya ikawa tabuni
wanawe tulishikana, kujua chanzo ni nini
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Sukari ikawa juu, kifua kilimbana
Akavimba na miguu, Dawa zilishindikana
Pumzi ikakata puu, kaitwa kwa maulana
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Alikuwa ni rafiki, na mengi aliusia
Nisipende unafiki, na maovu ya dunia
Dunia ina mikiki, ni vyema kuzingatia
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Nishikane na ibada, mama alisisitiza
Niheshimu wangu dada, nisipende kujikweza
Leo sina msaada, mwenzenu mie nawaza
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Ewe mola rahmani, msitiri mama yangu
Atulie kaburini, asipatwe na machungu
Muepushe ya motoni, mpe mema kwa mafungu
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA

Na hapa ninasimama, moyoni bado nalia
Kaondoka wangu mama, naona chungu dunia
siwezi hata kusema, unyonge umezidia
NINATANGAZA MSIBA, MAMA AMENITOKA



"INNA LILAH WAINNA ILAYH RAJ'UUN"


Pole sana - ILA SHAIRI/UTENZI WAKO VIMENIFANYA NA MIMI NILIE NIKIMKUMBUKA MAMA ALIYENITOKA 1996 - ITS REAL SAD - AND THE WAY YOU HAVE EXPRESSED HAS TOUCHED MY HEART ..................:crying:
:crying::crying::crying::crying::crying::crying::crying::crying:
 
Mungu ailaze roho yake mhali pema peponi
 
sijui nikuambieje i know the pain pole sana
 
Back
Top Bottom