Wakati mabadiliko ya kutoka mawimbi ya midwave na short wave,tuliaminishwa kwamba Frequency modulation (FM) itakuwa bora na mkombozi wa wapenzi wa redio.
Ninakubali huenda kwa watu wa miji mikbwa kama Arusha, Mwanza ,Dar , na Dodoma wanaweza kuwa wanasikia vizuri kwa utulivu vituo vingi vya redio.
Hata hivyo wawekezaji wengi wa redio ni wavivu wa kufikiri kwa kuwa wanaamini wasikilizaji wa redio wako mjini ila ukweli ni tofauti sana.
Kwanza mjini internate inapatikana vizuri watu wengi wapo busy na social media mjini kuliko kusikiliza redio.
Pia wengi hupenda vioindi vya luninga kuliko kusikiliza redio.
Kama vile haitoshi utakuta vijana wako busy kusikiliza miziki ya hovyo na hawataki elimu wala matangazo ya biashara.
Bahati mbaya wasikilizaji wa redio tuko vijijini ila tuna bahati mbaya sana na hii FM.
Unaweza kukuta hakuna redio yoyote inashika vijijini na ukibahatisha ni hivi viredio vya mikoani ambavyo navyo vimejaa vijana wasiojitambua.Hawana mada wala agenda za akili kama akina unazoweza kupata kwa magwiji kama Masoud Kipanya,Masoud Masoud wa TBC na wachache baadhi.
Vijijini internate ya shida sana,bado hata huwezi kuangalia TV hadi uwe na umeme na Dish.
Watu wengi wanahitaji redio huku vijijini.
Bahati mbaya hata TBC redio ya Taifa ina shindana huko huko mijini.
Ingekuwa zamani tungekuwa tunasikiliza hata KBC na Redio Bujumbura na wakati mwingine hata redio za Uganda.
Tulikuwa tunasikiliza BBC kwa uhakika kwenye shortwave ambapo kwa sasa hatusikii tena!
Walikuwa na kipindi cha kusisimua cha kujifunza kiingereza muda wa saa 11:30 alfajiri kabla ya kusikia taarifa ya habari
Ukweli naichukia sana hii teknolojia ni ya kipuuzi sana,kwani watu mnaowajali huko mjini wana option nyingi sana za kufuatilia kuliko kusikiliza redio.
Ningekuwa Rais Redio ya Taifa ingesikika hadi majarubani na watu wakivuna mpunga huku wanasikiliza.
Hata andiko hili imenichukua zaidi ya saa moja hadi kulipost kwq sababu internate inakatika katika na unajikuta unakutana na konokono tu wa JF