The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Kwa miaka mingi sana nimekuwa nikijiaminisha kuwa napenda sana machungwa. Nimekuwa nikiwaambia watu napenda sana machungwa. Msimu wa machungwa ukifika huwa ni kawaida kwangu kununua machunga mengi, na kumenya na kula si chini ya machungwa matano kila siku. Nayajua machungwa ya Tanga na yale matamu kuliko yote ya Kilwa, licha ya kuwa siyo mengi kama ya Tanga na kwingineko.
Siku za hivi karibuni nimejikuta najiuliza kama kweli nayapenda machungwa kiasi hiko, au labda nilikuwa najiongepea na kuongopea watu nnao waambia machungwa ndiyo matunda nnayopenda kuliko yote.
Nina mda mrefu sana sijanunua machungwa, na hata nikinunua najikuta nayatazama tu wala sina hamu nayo kama zamani. Why? Sababu ya machenza. Kiukweli nikiona machenza nakosa la kuongea kabisa, naweza sema napenda machungwa kama ut hakuna machenza. Nikiona machenza basi hakuna tunda lingine ninalo litamani, na yakiwepo machenza basi sigusi kabisa machungwa. Ingawa sijawahi jiambia wala kumuambia mtu kuhusu machenza.
ukweli ni kwamba, kama kuna machenza siwezi kula machungwa wala matunda mengine. Shida machenza huwa hayapatikani sana kwa wingi kama machungwa. Ni kama machenza yakiwepo basi hayana mshindani, lakini ni ngumu kusema "Napenda machenza," ni kama najidanganya mwenyewe.
Nimejikuta najiuliza vitu gani vingine ambavyo pia najiaminisha navipenda lakini kiukweli siyo chaguo sahihi, ikipatikana kumbe wala sio kihivyo kabisa!