Uchaguzi 2020 Ninawapongeza WanaCHADEMA wa Jimbo la Segerea kwa kumkataa John Mrema na kumpa Agnesta Lambert

Uchaguzi 2020 Ninawapongeza WanaCHADEMA wa Jimbo la Segerea kwa kumkataa John Mrema na kumpa Agnesta Lambert

John Mrema ni mtu mwenye Cheo sawa na cha Humphrey Polepole wa CCM yaani ni mwenezi wa Chama Taifa.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikimsema humu JF kuwa yeye ndie amekuwa akiivuruga CHADEMA kwa fitina na majungu yake na kumshauri vibaya M/kiti wa Chama chake yeye pamoja na mtu anaitwa Reginald Munisi.

WanaCHADEMA wamenielewa na wamegundua hila zake na sasa wameanza Kumkataa hadharani. Mrema ameshiriki kura za maoni kugombea jimbo la Segerea ambalo mwaka 2015 aliachiwa Mtatiro ila Mrema kwa kumtumia mwandani wake wakagawa kura zaidi ya 45000. Mwaka huu wamegawana Mzee Segerea yule mwingine Karagwe huko!

Jimbo la Segerea kura za Maoni Tayari
Na matokeo ni kama Ifuatazo

Jumla ya Wapiga Kura 144

Agnes Lambert 76
John Mrema 56
Masatu Wasira 7
Gango Kidera 3
Andrew 1
Kura zilizoharibika 1

Wanawake Oyeeee!

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini nae kapata kura 2 kati 128 huko Muhambwe!

Tunamsubiria Baba yake Mbowe kwenye Urais!
Unataka kusema mzee Ntagazwa nae alienda kugombea Muhambwe?
 
Siwezi kwa vile yeye (au anapashwa) ni KIOO na KIELELEZO cha kila kitu kwetu be it katiba, sheria, democracy, utii, tabia njema, kauli njema, mfariji Mkuu etc etc etc! . Kama anakiuka hayo, basi lazima nimseme! Nimlinganishe na wengine
Kama ni kioo unasemaje kuhusu rushwa, au hiyo ina duoble std??
Gen Boss TAKUKURU kasema anapambana nayo, lakini Kigwangwala kagawa pikipiki zaidi ya 300 na baiskeli phoenix zaidi ya 800 hapo Nzega kwa wapiga kura za maoni Nzega!!
Na Tulia naibu spika kagawa pikipiki kwa wana bodaboda pale Mbeya!!
Ni rushwa ipi mnpambana nayo???
 
haya niliyaona kwa Idd Amin! Sikufikiria kuwa tungelifika huko! Exactly tabia za tawala za madikiteita!
Maendeleo hata maflyover, madege, reli, meli etc bila uhuru na demokrazia ni utumwa!!
South Afrika na nchi zetu, pamoja na maendeleo makubwa tulidai uhuru tujitawale tusiwe watumwa!!
Tuwe watumwa karne ya ishirini ni aibu sana!!
 
John Mrema ni mtu mwenye Cheo sawa na cha Humphrey Polepole wa CCM yaani ni mwenezi wa Chama Taifa.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikimsema humu JF kuwa yeye ndie amekuwa akiivuruga CHADEMA kwa fitina na majungu yake na kumshauri vibaya M/kiti wa Chama chake yeye pamoja na mtu anaitwa Reginald Munisi.

WanaCHADEMA wamenielewa na wamegundua hila zake na sasa wameanza Kumkataa hadharani. Mrema ameshiriki kura za maoni kugombea jimbo la Segerea ambalo mwaka 2015 aliachiwa Mtatiro ila Mrema kwa kumtumia mwandani wake wakagawa kura zaidi ya 45000. Mwaka huu wamegawana Mzee Segerea yule mwingine Karagwe huko!

Jimbo la Segerea kura za Maoni Tayari
Na matokeo ni kama Ifuatazo

Jumla ya Wapiga Kura 144

Agnes Lambert 76
John Mrema 56
Masatu Wasira 7
Gango Kidera 3
Andrew 1
Kura zilizoharibika 1

Wanawake Oyeeee!

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini nae kapata kura 2 kati 128 huko Muhambwe!

Tunamsubiria Baba yake Mbowe kwenye Urais!

Huyo mzee wa baraza la wadhamini sijui kapatwa na kitu gani kichwani!
 
siasa mbaya sana, unatumia muda na fedha halafu unaambulia kura yako mwenyewe.
 
Mshindi wa kwanza tulimpa CROSS
Mshindi wa pili nae CROSS
Wa tatu nae CROSS
Wa Nne ndiye tukampitisha ambae ndiye huyu Ndumbalo

Hayo ni Maneno ya Mwenyekiti wa CCM Taifa-Magu
Uchaguzi sio kura tu, lazima uwe safi. Kama mtu akipitia njia za kando kando kupata ushindi, lazima kamati maalumu zitoe uwamuzi.
 
Wewe utahangaika sana lakini Huteuliwi ng'o, laana ya hela ulizokwapua Chadema inakutafuna, endelea tu na biashara yako ya mama lishe na bar bubu.
kwahiyo hela za chadema alizokwapua ndo mtaji wa baa bubu na mamalishe.

Mkuu baa iko mitaa gani tunywe bia na kuwaponda kina mbowe
 
Kwa hakika CCM haikuwa na na sababu ya kufanya zoezi eti la kutafuta wadhamini kwa mgombea urais na kufanya mkutano mkuu. Kwa kuwa fomu ilikuwa mojayombo vya juu , vingekasimu masuala yote kwa Kamati Kuu. Vinginevyo mambo yote yaliyokuwa yanafanyika ilikuwa usanii mtupu!
 
Back
Top Bottom