Ninawapongeza wananchi wa mzinga kwa kufunga barabara, serikali hii isiyosikia ichukue hatua

Ninawapongeza wananchi wa mzinga kwa kufunga barabara, serikali hii isiyosikia ichukue hatua

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
7,683
Reaction score
15,128
Habari za wakati huu wana jamii forum bila shaka wote ni wazima na wale ambao mmeamka na changamoto mbali mbali Mungu awafanyie wepesi.

Kwanza niweke wazi mimi ni miongoni wa wananchi tunaoishi mzinga kwa miaka kadhaa sasa.

Kumekua na mfululizo wa ajali kutoka Mbagala kokoto(mlimani) mpaka mbagala mzinga tena za kuogofya kutokana na ufinyu na ubovu wa barabara miaka na miaka. Ndugu zetu wengi wanaoishi mzinga na ambao mzinga kama njia yao wamekua wakipoteza maisha kwa ajali zinazoletwa na uzembe wa mamlaka TANROADS na SERIKALI kwa ujumla.

Jana jioni Roli la maji liliacha njia na kugonga watu inasemekana miongoni wao ni watoto wadogo na kuvunja kingo za daraja na kuingia kwenye mto kutoka saa 11 jioni mpaka asubuhi halijatolewa. Ajali hii imepelekea wananchi wa maeneo hayo kufunga barabara kwa mawe na magogo wakinishinikiza serikali iboreshe barabara na kutanua daraja. Mpaka sasa sijafika kazini lakini sijachukia na nafurahia wananchi kwa kitendo walichofanya ili kupata suluhisho. Kilichonifurahisha wakina mama ndo wamekua mstari wa mbele kufunga barabara licha ya vitisho vya jeshi la polisi kutaka kutumia nguvu.

Kwenye hilo daraja upande wa wapita kwa miguu daraja limeoza kabisa kiasi cha kwamba kama ni mgeni unaweza kutumbukia kwenye mto.

Kwa wiki hizi 3 zinetokea ajali mbaya zaidi ukiachia hii ya leo,mfano kuna bajaji iliangukiwa na lori la cement kama wiki 2 zilizopita hii niliona kwa macho yangu na wote walipoteza maisha,baada ya siku kama nne eneo lile lile daladala,lori la mchanga na bajaji zilipata ajali kwa wakati mmoja na watu kupoteza maisha na ajali nyigine nyingi. Imekua nadra sana kupita pale na kukuta njia iko vizuri ni balaa tu. Binafsi naweza kutoka huki kote ila nikifika rangi 3 nawaza namna ya kufika nyumbani salama.

SERIKALI mnaona raha kununua roboti na kufanya matumizi ya anasa wakati walipa kodi mnatuona wajinga na mazuzu barabara ya kutoka rangi 3 kuanzia kokoto mpaka mtwara ni mbovu ,mtwara hadi masasi ni imechakaa miaka na miaka ila wala hamuwazi
 
Kwanza kabla ya kuchangia hii mada,
Napenda kumshukuru raisi
pia napenda kutoa pole za dhati kwa wakazi wa mzinga.
Napenda kuuliza huko kwenu wabunge ni wa kutoka chama gani?
 
kwani kuna mtu aliwatuma? pambaneni na hali zenu hakuna aliyewatuma kuchagua utawala dhalimu , na nyie ndio mnasifia kila uchao ooh anaupiga mwingi ooh tunamshukuru mama, mshukuruni pia kwa ajali hiyo ili shukrani zenu zimdfikie akiwa huko Ufaransa. Nchi ya viazi mviringo kabisa.
 
barabara ya kilwa ina laana ya kimaendeleo na sio barabara tu, ni mpaka wakazi wao kuanzia mbagala, kongowe, vikindu, kisemvule nakuendelea kunanuka nuksi mambo yanaenda slow sana, Ukitaka kujipiga pini za maendeleo njoo uishi pande hizi.

Barabara pekee ya kwenda kwa wamakonde mpaka kuzamia kwa madiba ndio hiyo na ni ndogo, mbovu kwa miaka 15 na zaidi sasa. Tunapoelekea sio serikali tu ndio ifanye jambo na maombi yanahitajika pia.
 
Nimeshuhudia ajali kubwa mbili eneo hilo.
Ajali nyingi gari zinarudi nyuma au/na kuangukia Bajaj au gari zingine au kuingia mtoni.
Ukipita hapo kukiwa na gari kubwa mbele yako unakuwa na hofu kubwa.
 
feyzal hii barabara ingekuwa IPO wilaya kinondoni ingekuwa imejengwa miaka 10 uliyopita,UJINGA kama huu unasababisha tuone ndani ya nchi hii kuna ubaguzi wa maeneo na kikanda.

Eneo lote la mzinga ni hatarishi Sana na barabara ni nyembamba kama ya mtaani, viongozi wa nchi hii ni vipofu wote
 
Back
Top Bottom