Daaaah,, nakumbka mwaka 2012 apo nipo la saba, shule ilikua mjini kabisa na ili ufike shule lazima uvuke lami,sasa watoto walikua wanagongwa sana na magari na hapakua na kivuko chochote.
siku io kagongwa mtoto asubuhi,walimu walisubiri tushibe ugali mchana,kisha ikagongwa kengele,tukaenda mstarini😁, aseee mkuu wa shule alitwambia kauli moja tu,(nendeni barabaran mkasema tunataka matuta)😂😂.
Aloooh mengine tulijiongeza wenyewe, kama kuweka magogo na kuimba nyimbo,kumfata mkuu wa mkoa kwake (RIP yule mama),afu ilikua jioni mabasi ya dar ndo yanafika🤣kwan walituweza sasa,tukiona dereva m'babe tunalala kabisa na mkuu wa mkoa alikuja shulen mda ule ule na kulkua na mvua.
Siku ya pili tuliwekewa trafiki na sku ya tatu zebra crossing,,leo ad taa zipo😂🤣.
Samahani uandishi m'bovu poleni kwa gazeti pia.