Ninawaza kufungua Duka la Vinywaji

Ninawaza kufungua Duka la Vinywaji

More Chances

Senior Member
Joined
Jun 24, 2022
Posts
151
Reaction score
344
I wish niwe na biashara kabla ya mwaka huu kuisha. Moja ya biashara inayo trend kichwani mwangu ni duka la vinywaji. Yani niuze vitu vifuatavyo.

Bia
Pombe kali kama K. vant na konyagi. Soda zote +plus takeaway. Maji ya jumla na rejareja. Sigara za jumla na rejareja. Wine kidogo. Naomba wale wenye idea na ujuzi na biashara hii andikeni chochote mnachokijua, kama bei za vinywaji hivo, upatikanaji, changamoto, Faida,vibali. Working capital yangu ni 2.5 -3.5M kwa kuanzia

Natanguliza shukrani

Pia comments zote zitasomwa
 
Frem ya biashara ni yako au unapangisha?
 
Unaweza kuanza mkuu, huku ukiweka kwanza bidhaa zinatoka kwa haraka kisha faida uwe unaongeza bidhaa zingine unazohitaji ziwepo.

Muhimu ni kuwa na uvumilivu, nidhamu ya pesa, utayari na kupata location nzuri
 
Hii nilifungua mwaka jana...

Kreti tu zilikula milion 2 kreti tupu..za bia 100 za soda 100 kwa elf 10, ukisema usubirie za bei rahis mtaani unapoteza mda..ukiwa na bia pamoja na soda unahitaji store kama frem sio kubwa, kwa mtaji huo anza kidogo na maji pamoja na soda
Screenshot_20220511-210933.jpg
 
Hii nilifungua mwaka jana...

Kreti tu zilikula milion 2 kreti tupu..za bia 100 za soda 100 kwa elf 10, ukisema usubirie za bei rahis mtaani unapoteza mda..ukiwa na bia pamoja na soda unahitaji store kama frem sio kubwa, kwa mtaji huo anza kidogo na maji pamoja na sodaView attachment 2282932
Mkuu kwa hiyo picha ya kuchungulia getini tena screenshot,una uhakika duka hilo ni lako?
 
Kwa mtaji huo huwezi, ukinunua caton kadhaa za pombe Kali hela imeisha, ongeza zifike 6
 
Kumbuka Kuna kununua cret ukinunua za bia 50 na soda 50 milion moja inakata
 
Zingatia location mkuu ni biashara inahitaji nidhamu Sana kwenye matumizi faida yake ni ndogo ndogo Sana,mfano soda faida kwa cret haizidi 900 mpaka 1000 na bia hivyo hivyo, pombe Kali ndo kidogo unaweza kupata 2000 hadi 3000 kwa caton.
 
mkuu kwa hiyo picha ya kuchungulia getini tena screenshot,una uhakika duka hilo ni lako?
Hmmh aiseeh waTz ni watu waajabu sana, kwahiyo ulitaka apige ndani ya duka lake ili uamini kuwa ni lake? Okay, hata kama sio lake kwanini usifuate idea anayotoa?
 
Back
Top Bottom