Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Siku hizi mtaani kuna vilio cha maumivu makubwa ya watu kulalamikia utendaji usioridhisha wa watumishi wa Umma. Wengine wanalalamika uzembe ,rushwa, uonevu na kutosikilizwa kukishamiri katika ofisi za Umma.
"Ukienda ofisi ya Umma bila kutoa chochote yawezekana usipate huduma inayoridhisha na zaidi unaweza kuangaliwa tu bila kusikilizwa", alisema mdau mmoja.
Lakini cha ajabu katikati ya vilio na malalamiko JPM anatajwa na wengine wakienda mbali zaidi wakisema JPM aliweza kudhibiti hali hii ya uzembe na rushwa maofisini tunamkumbuka.
Wito
Malalamiko haya yanatolewa na watu wa chini kabisa ambao si rahisi kuweza kufikisha malalamiko yao Juu na kwa kuwa kisemwacho kipo basi Serikali haina budi kudhibiti janga hili kwa nchi.
Naomba kukiri nilichowahi kukutana nacho TRA kinatisha sana. Ile hofu ya mteja ni mfalme TRA hawana kabisa, rushwa na uzembe vinafanyika waziwazi. Hivyo nikisikia watu wanalalamikia utendaji wa mamlaka hii ni ishara wamechoka.
Halmashauri napo hali si shwari, kuna uzembe katika utoaji wa huduma hususani katika idara za afya. Wagonjwa kutopewa huduma stahiki ni jambo la kawaida likichangiwa na rushwa.