Ninayoyasikia mtaani juu ya watumishi wa Umma katika awamu ya sita yanatisha

Siku hizi mtaani kuna vilio cha maumivu makubwa ya watu kulalamikia utendaji usioridhisha wa watumishi wa Umma. Wengine wanalalamika uzembe ,rushwa, uonevu na kutosikilizwa kukishamiri katika ofisi za Umma.

"Ukienda ofisi ya Umma bila kutoa chochote yawezekana usipate huduma inayoridhisha na zaidi unaweza kuangaliwa tu bila kusikilizwa", alisema mdau mmoja.

Lakini cha ajabu katikati ya vilio na malalamiko JPM anatajwa na wengine wakienda mbali zaidi wakisema JPM aliweza kudhibiti hali hii ya uzembe na rushwa maofisini tunamkumbuka.

Wito
Malalamiko haya yanatolewa na watu wa chini kabisa ambao si rahisi kuweza kufikisha malalamiko yao Juu na kwa kuwa kisemwacho kipo basi Serikali haina budi kudhibiti janga hili kwa nchi.

Naomba kukiri nilichowahi kukutana nacho TRA kinatisha sana. Ile hofu ya mteja ni mfalme TRA hawana kabisa, rushwa na uzembe vinafanyika waziwazi. Hivyo nikisikia watu wanalalamikia utendaji wa mamlaka hii ni ishara wamechoka.

Halmashauri napo hali si shwari, kuna uzembe katika utoaji wa huduma hususani katika idara za afya. Wagonjwa kutopewa huduma stahiki ni jambo la kawaida likichangiwa na rushwa.

Waambie waache uchonganishi, mama kishasema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Akili yako ina walakini mdio maana umeandika kwa kutumia akili yenye walakini. Ndizi mbivu 10,000/=??
"...ndizi mbivu 10,000"? Wacha bhwanah, wapi huko!

Mimi haya mambo siyajui mkuu, kwa hiyo usinilaumu kwa kuuliza.
 
Upuuzi mtupu umeandika hapa! Acha kuchafua ofisi za umma, hizo ulizoandika labda za ukoo wako.

Kwa kukusaidia Magufuli alikwisha kufa wala haji kurudi tena milele, kajipange upya!
Ndiyo, "akajipange upya", huku sisi tukiendelea "kula kwa urefu wa kamba zetu"!

Simtetei huyo jamaa, kwa sababu ulalamishi wake unajulikana unakoanzia; na hapo hapo nakukumbusha wewe maelekezo mapya yaliyotolewa.

Sasa sijui nafuu ya waTanzania itatoka wapi?
 
Nilisikia Mh Rais akisema mahabusu namba yao ni sawa na wafungwa. Tatizo mojawapo la mlundikano wa mahabusu ni sheria ya dhamana. Haiwezekani kila Mtanzania mwenye kuhitaji dhamana awe na barua kwa mtu anaye fanyakazi kazini serikalini ama ofisi nyengine rasmi. Kama huna watu hao utafanya nini? Nfio ufuate mlolongo mrefu wa kuanzia serikali za mitaa mpaka halmashauri kupata barua. Hii ni kusababisha ukiritimba usio na msingi.

Kupunguza hili tatizo la msongamano wa mahabusu form za dhamana mahakamani za vikesi vidogo zitolewe na wajumbe wa nyumba kumi au mtuhumiwa adhaminiwe na mtu mwenye kitambulisho cha urai anaye aminika.
 
Mamlaka zinazopokea malalamiko zipo msijifungie ndani
 
Miwaongezee mishahara na kuboresha marupurupu na maslahi yao.Siyo unataka tu uhudumiwe kwa haki wakati hautaki kutimiza wajibu wako kwa mtumishi.Nipe haki yangu nitimize wajibu kwa haki.
Kama unaona mshahara ni mdogo si uachie ngazi uwende huko private sector kwenye mishahara mikibwa,kuliko kubaki hapo na kuleta mgomo baridi kwa Wananchi wa kawaida!? Hiyo ndiyo nidhamu ya Moyoni muliofundishwa na Mama yenu!?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nani alikusimulia mimi ni mtumishi?Hata maneno nilivyoandika unataka kuyabadilibadili utakavyo?Na aliyeleta uzi anaeleza eti anasikia!Umbeya huo.
 
Sasa Kama wewe siyo mtumishi umejuwaji kua mishahara yao na marupurupu yao hayajaboreshwa hadi kufikia kutoa kauli ya Mishahara na Marupurupu yao!?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Sasa Kama wwe siyo mtumishi umejuwaji kua mishahara yao na marupurupu yao hayajaboreshwa hadi kufikia kutoa kauli ya Mishahara na Marupurupu yao!?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kuna kipi ambacho weye unadhani ni cha Siri au kificho kutoka kwa watumishi?SSH alivyosema atawaboreshea mwezi Mei 2022 ulidhani anamletea nani puruzai?
 
Wameambiwa wale kwa urefu wa kamba zao.

Kwani wao hawana matumbo.?

#MaendeleoHayanaChama
 
Wito
Malalamiko haya yanatolewa na watu wa chini kabisa ambao si rahisi kuweza kufikisha malalamiko yao Juu na kwa kuwa kisemwacho kipo basi Serikali haina budi kudhibiti janga hili kwa nchi.

Naomba kukiri nilichowahi kukutana nacho TRA kinatisha sana. Ile hofu ya mteja ni mfalme TRA hawana kabisa, rushwa na uzembe vinafanyika waziwazi. Hivyo nikisikia watu wanalalamikia utendaji wa mamlaka hii ni ishara wamechoka.
Magufuli alimaliza kero instantly
 
Siku hizi mtaani kuna vilio cha maumivu makubwa ya watu kulalamikia utendaji usioridhisha wa watumishi wa Umma. Wengine wanalalamika uzembe ,rushwa, uonevu na kutosikilizwa kukishamiri katika ofisi za Umma.

"Ukienda ofisi ya Umma bila kutoa chochote yawezekana usipate huduma inayoridhisha na zaidi unaweza kuangaliwa tu bila kusikilizwa", alisema mdau mmoja.

Lakini cha ajabu katikati ya vilio na malalamiko JPM anatajwa na wengine wakienda mbali zaidi wakisema JPM aliweza kudhibiti hali hii ya uzembe na rushwa maofisini tunamkumbuka.

Wito
Malalamiko haya yanatolewa na watu wa chini kabisa ambao si rahisi kuweza kufikisha malalamiko yao Juu na kwa kuwa kisemwacho kipo basi Serikali haina budi kudhibiti janga hili kwa nchi.

Naomba kukiri nilichowahi kukutana nacho TRA kinatisha sana. Ile hofu ya mteja ni mfalme TRA hawana kabisa, rushwa na uzembe vinafanyika waziwazi. Hivyo nikisikia watu wanalalamikia utendaji wa mamlaka hii ni ishara wamechoka.

Halmashauri napo hali si shwari, kuna uzembe katika utoaji wa huduma hususani katika idara za afya. Wagonjwa kutopewa huduma stahiki ni jambo la kawaida likichangiwa na rushwa.
Wazandiki hawaishi kulalamika
 
Back
Top Bottom