Ninayoyasikia mtaani juu ya watumishi wa Umma katika awamu ya sita yanatisha

Ninayoyasikia mtaani juu ya watumishi wa Umma katika awamu ya sita yanatisha

Cha moto unakiona fanyakazi uzushi hauna nafasi kwa sasa utaumia sana.
 
Toka Kinana apewe umakamu naona Bhagosha wameamua kumkumbuka Mwendazake.
 
Miwaongezee mishahara na kuboresha marupurupu na maslahi yao.Siyo unataka tu uhudumiwe kwa haki wakati hautaki kutimiza wajibu wako kwa mtumishi.Nipe haki yangu nitimize wajibu kwa haki.
Kama kazi haina masilahi unaacha sio kufanya ilimradi tu.
 
[emoji1787][emoji1787] awamu ya 5 hata wakamteka bila kujali ye ni nani
Ndiyo maana ya Serekali,hata ukiwa na pesa vp tii mamlaka! Siyo Serekali unakaa unawabembeleza Wafanyabiashara, mwisho wao ndiyo watakupangia mashariti Kama wanavyofanya kwenye hii awamu ya 6!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Upuuzi mtupu umeandika hapa! Acha kuchafua ofisi za umma, hizo ulizoandika labda za ukoo wako.

Kwa kukusaidia Magufuli alikwisha kufa wala haji kurudi tena milele, kajipange upya!
Uje ofisini na kitu kidogo bila hivyo utakula kwa urefu wa kamba yako.
 
Siku hizi mtaani kuna vilio cha maumivu makubwa ya watu kulalamikia utendaji usioridhisha wa watumishi wa Umma. Wengine wanalalamika uzembe ,rushwa, uonevu na kutosikilizwa kukishamiri katika ofisi za Umma.

"Ukienda ofisi ya Umma bila kutoa chochote yawezekana usipate huduma inayoridhisha na zaidi unaweza kuangaliwa tu bila kusikilizwa", alisema mdau mmoja.

Lakini cha ajabu katikati ya vilio na malalamiko JPM anatajwa na wengine wakienda mbali zaidi wakisema JPM aliweza kudhibiti hali hii ya uzembe na rushwa maofisini tunamkumbuka.

Wito
Malalamiko haya yanatolewa na watu wa chini kabisa ambao si rahisi kuweza kufikisha malalamiko yao Juu na kwa kuwa kisemwacho kipo basi Serikali haina budi kudhibiti janga hili kwa nchi.

Naomba kukiri nilichowahi kukutana nacho TRA kinatisha sana. Ile hofu ya mteja ni mfalme TRA hawana kabisa, rushwa na uzembe vinafanyika waziwazi. Hivyo nikisikia watu wanalalamikia utendaji wa mamlaka hii ni ishara wamechoka.

Halmashauri napo hali si shwari, kuna uzembe katika utoaji wa huduma hususani katika idara za afya. Wagonjwa kutopewa huduma stahiki ni jambo la kawaida likichangiwa na rushwa.
Acha tukome kabisa maana watu hawajielewi
 
Upuuzi mtupu umeandika hapa! Acha kuchafua ofisi za umma, hizo ulizoandika labda za ukoo wako.

Kwa kukusaidia Magufuli alikwisha kufa wala haji kurudi tena milele, kajipange upya!
Ila yuko mioyoni mwa watz waliowengi mkuu.
 
Ndiyo maana ya Serekali,hata ukiwa na pesa vp tii mamlaka! Siyo Serekali unakaa unawabembeleza Wafanyabiashara,mwisho wao ndiyo watakupangia mashariti Kama wanavyofanya kwenye hii awamu ya 6!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
ungejua sababu ya kutekwa kwake usingeandika huo uharo. ni serikali ya kijuha tu inaweza kuteka bilionea wa nchi
 
IMG_5940.png

tumia hiyop
 
Back
Top Bottom