kwa wale ambao mmefuatilia game za congo drc nadhani kuna vitu vya kujifunza kwa wachezaji wao. kwanza kabisa wanajiamini hawana mapepe pia control imelala karibia wote, mchezaji wa kongo akipata mpira kwanza anakuwa mtulivu cyo km wachezaji wetu akipata mpira unakuwa km una moto jinsi anavyopatwa na wenge! wakiwa wanaenda kushambulia unaona kabsa wana mipango na sio wakurupukaji wanacheza kwa malengo na kila mchezaji anatimiza majukum yake jinsi anavyotakiwa pia licha ya wengi wao kuonekana umri umeenda lkn wana stamina sana cyo rahisi kuchukua mpira kizembe kwa wachezaji wa kikongo kwani karibia timu nzima wameshiba kitu cha mwisho tofauti na timu nyingi za afcon timu ya kongo licha ya kutumia mabavu vile vile wanatumia akili sana ......kwa yoyote ambaye anatka kuthibitisha hya aanze kuzifuatilia game za kongo kwa jicho la tatu atapata majibu ,binafsi naamini kongo anaweza kuibuka bingwa wa kombe hili