Ningekuwa Mkuu wa Wilaya ningetatua tatizo la ajira kwa watu wote wanaoishi wilayani kwangu

huku wakipoteza maarifa yao waliojifunza vyuoni bila kuyafanyia chochote.
Wahitimu wenye sifa za kupoteza maarifa na kukaa bila ya kufanya chochote eti kwa kuwa HAWAJAPEWA ajira ni mzigo kwa taifa.

Kwanza hawakuyapata maarifa (labda maarifa yasiyotakiwa kwenye jamii, mf kunywa pombe, kubet, kungonoka n.k).
Mwenye maarifa hawezi kukaa bila ya kufanya chochote ktk nchi ya Tanzania iliyajaliwa ardhi tele yenye rutuba. Mhitimu huyu kama hajaiona fursa ktk hili ni mbumbumbu.

Pili nashauri wahitimu wa aina hii wakamatwe wafunguliwe kesi za uhujumu uchumi. Wamefuja fedha za walipa kodi kwa kusomeshwa na serikali halafu wanamaliza anakaa bila ya kufanya chochote? How? Walienda shule kulemaa ama kupata mbinu za kujitafutia riziki?

Huu ujinga wa kumaliza vyuo halafu mnakuja kutujazia server huku kuilalamikia serikali kuhusu ajira ukome. Kwanza mnajidhalilisha. Wewe na mm ambaye sikusoma tuna tofauti gani Sasa??

Ingieni msituni mkalime wajinga nyie.

.
 
Mimi nimewahi kuwaza, kwanini mkuu wa mkoa asichukue watu wake hasa vijana wasio na kazi wooote mkoani kwake awapeleke shambani wakalime, awalishe, awalipe pesa kidogo ya kujikimu mf 50000 kwa mwezi, awape mahali pa kulala(hata majumba ya mabati tu kwa muda), then wakivuna serikali itafute masoko mazao yauzwe au serikali inunue yenyewe faida ipigwe pasu kati ya serikali na wakulima ili kufidia gharama zilizotumika from there mtu atakuwa na mtaji akiamua kuendelea kulima poa akiamua kuondoka kuanza maisha mapya ni nzuri pia.
 
Suppose wewe ni mkuu wa wilaya ya Liwale au Namtumbo ambapo hakuna kiwanda wala kampuni yoyote ile ungefanyaje?

Wahitimu wenye sifa za kupoteza maarifa na kukaa bila ya kufanya chochote eti kwa kuwa HAWAJAPEWA ajira ni mzigo kwa taifa...
Mbona unatukana mkuu, badala ya kutoa hoja. Mwanzoni umeanza vizuri lakini huku mwishoni umeanza kutoa matusi kulikoni. Uliza swala sehemu ambayo haieleweki ujibiwe.

Hili ni jukwaa huru kila mtu anauhuru wa kuandika chochote kinacho elimisha. Hapo ilibidi uandike mawazo yako bila kutukana.
 
Ni rahisi sana maana nafasi za magereza urekebishaji bado ziko wazi
 
Mimi nimewahi kuwaza, kwanini mkuu wa mkoa asichukue watu wake hasa vijana wasio na kazi wooote mkoani kwake awapeleke shambani wakalime, awalishe...
Mimi nashauri wahitimu wasio na kazi wakamatwe wafunguliwe kesi za uhujumu uchumi. Wamefuja fedha za walipa kodi kwa kusomeshwa na serikali halafu wanamaliza anakaa bila ya kufanya chochote? How? Walienda shule kulemaa ama kupata mbinu za kujitafutia riziki??.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Mkuu nimekunote.
 
Mkuu sio rahisi hivyo. Ukichukua tu wilaya moja wasio na kazi wanaweza kujaza viwanda vyote Bongo πŸ˜€πŸ˜€
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Tuanze na wilaya yako boss. Waliosomea fedha wako wangapi, waliosomea uhandisi wapo wangapi, waliosomea afya wapo wangapi, waliosomea ualimu wapo wangapi, waliosomea uchumi wapo wangapi.

Wawe ni waziri wa wa hapo walayani kwako, ulipo zaliwa. Hapo wilayani kwako kuna hospitali ngapi, shule ngapi, dispensari ngapi, banki ngapi, kampuni zingine ngapi, viwanda vingapi n.k
 
Yaani viwanda?

Je, ungekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyamba ungewaweka hao vijana katika Viwanda vipi?
Hili jambo mi mwenyewe nimelifikiria kaongelea mjini tu hajaainisha ingekuaje km angekua vijijini
 
Siyo rahisi kupata uteuzi kwa vijana wa Sasa. Kijana wa mwaka 1955 bado mfano Miuchika anapewa shavu hadi leo, huyu wa 2020 inabidi asubiri sana. Bora wakapime tu.
Mimi nina kazi zangu nafanya mkuu nimeajiri watanzania. Ila 2025 nagombea ubunge ili kusaidia watanzania. Naingia bungeni kwenda kuwasemea watanzania. Nadhani umenipata mkuu.
 
Nadhani hii italeta chachu kidogo vijana kwa vijana.
 
Haya twende kazi..kiwanda ni kimoja(hata sijui kwa nini nakiita kiwanda πŸ˜€ ), hospitali moja, benki mbili (moja wafanyakazi naona watatu tu), shule sijui labda tuseme za uhakika labda tatu..chuo cha ualimu kimoja...haya niambie hao wasio na ajira wote nawapeleka wapi? Nakuhakikishia yani ukichukua wasio na kazi wilaya moja tu wanajaza karibia nusu ya kazi zote hii Bongo πŸ˜€. Boss unaelewa GoT yenyewe haina wafanyakazi zaidi ya 1million nchi ya watu 50plus million? Tatizo ni kubwa sana boss..kubwa sana na hakuna strategy yoyote ya kusolve hili swala.
 
Unazijua wilaya za Tanzania?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚boss umesahau dispensary, shule za private, hospitali za private
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚boss umesahau dispensary, shule za private, hospitali za private
Hivyo ndio vilivyopo boss. Nina uhakika kuna wilaya zingine ni majanga zaidi πŸ˜€ πŸ˜€. GoT yenyewe imeingia mitini kuhusu ajira, ukiona government wenye kila wanakimbia ujue ni balaa. Na bado vyuo vinamwaga tu watu mtaani.
 
Hivyo ndio vilivyopo boss. Nina uhakika kuna wilaya zingine ni majanga zaidi πŸ˜€ πŸ˜€. GoT yenyewe imeingia mitini kuhusu ajira, ukiona government wenye kila wanakimbia ujue ni balaa. Na bado vyuo vinamwaga tu watu mtaani.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mimi ningeteuliwa kuwa DAS kwenye wilaya hiyo ningekuongezea mawazo;-

(1) Ningekusanya taariga za hao vijana mezani kwangu ofisi iwatambue

(2) Ningewashawishi tuanzishe joging team kila mwisho wa wiki tunajog pamoja na wewe ukiwepo. Hili lingetusadia kuwatambu ni nani na nani ni watiifu na wenye nidhamu

(3) Wilaya ikipata nafasi za kazi hata kama za kujitolea ningekushauri tuanze na wale wenye nidhamu kwenye joging team yetu

(4) Kisha zile mil 50 za ahadi zikifika kwenye jimbo letu tungeanza na hawa vijana kuwawezesha kujiajiri wenyewe hata kwa mitaji midogo midogo huku wakisubiri ajira ya kudumu

(5) Makampuni au wawekezaji wakija hawa vijana wetu ndio tutawapa kipaumbele kama watahitaji wataalamu wa nyanja mbalimbali

(6) Mwisho ningefanya kila mbinu mteule wetu akupandishe cheo au akuhamishe wilaya wilaya ili aje mkuu wa wilaya mwingine ajifunze namna tulivyotokomeza tatizo la ajira wilayani kwetu
 
Unaongelea wahitumu kama vile wamesoma Nuclear Science kumbe ni hawa hawa wa vyuo vyetu. Ongelea vijana na Ajira za kuleta Maendeleo. Wewe unadhani Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Atawaweka kwenye Kampuni gani?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Mkuu hii mikakati nadhani kuna wakuu wawilaya humu wananote saivi. Wanadhani ukuu wa wilaya ni kutakua kero za maji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…