Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Siasa za vyuo vikuu Tanzania ni siasa za CCM na CHADEMA full stop. Ukilijua hili utajua ni kwanini CHADEMA walianzisha CHASO na CCM walianzisha mkoa maalum wa Vyuo vikuu.
Mwenyekiti wa TAHLISO, (au pengine kama anavyopenda aitwe rais wa TAHLISO, ingawa sina hakika kama sasa katiba imebadilika, ila tangu uenyekiti wa ndugu Paul Makonda, wenyeviti wamekuwa wakijitambulisha kuwa "rais" badala ya "mwenyekiti" kama ilivyo kwenye katiba ya TAHLISO); vyovyote iwavyo ni either CCM au CHADEMA.
Jambo hili huwa linaipa TAHLISO sura ya uungaji mkono serikali inapopata kiongozi kutoka CCM, au chombo cha harakati inapopata kiongozi kutoka CHADEMA. Na kwakweli mambo hayo yamekuwa yakijirudia kwa mtindo huo.
Mwenyekiti wakwanza wa TAHLISO kuwa CCM kwa wazi wazi alikuwa ni Makonda. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Makonda alijua kuutumia ukaribu wake na serikali kwa manufaa ya wanafunzi. Na hii ndio sababu, pamoja na kulinda maslahi ya serikali ndani ya TAHLISO hakuwahi kulaumiwa kuifanya TAHLISO tawi la UVCCM.
Pamoja na wajibu wake kama mwenyekiti wa TAHLISO, Kiliba kama kijana, ana interest zake, na anayo haki ya kuitumia nafasi yake kutengeneza connections zitakazo msaidia baadaye. Marehemu Kipala, Makonda, Chakushemeile na wengine wengi wote walifanya hivyo. Changamoto ya Kiliba ninayoiona ni kuwa over-ambitious na pengine kuwa na haraka ya kufika anakotaka kwenda. Otherwise kama angetembea kwa mwendo wa Makonda pengine ingemsaidia kumpunguzia wakosoaji.