Ningekuwa mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Dar Es Salaam, ningefanya haya kujiandaa na Majanga na wakati wa Majanga

Utaratibu mzuri wa raia ni kama ulivyoona na jinsi ulivyofanikiwa kuokoa wenzao pale.

Vinginevyo ukitaka utaratibu mzuri zaidi utawapoteza wengi sana, maana lazima usubiri bajeti, vikao na vifaa kutoka sijui wapi kule!.

Utaratibu mzuri ni kurudia mpango mji wa Kariakoo upya.
 
Ni kweli mchango na nguvu ya raia ktk hali kama hii ni muhimu. Hata hivyo ni vema ku set up utaratibu mzuri ambao hautakuwa kikwazo na kizuizi ktk movement za kuingia na kutoka ukizingatia mazingira ya Kariajoo yalivyo.

Kweli kabisa. Kuwepo na utaratibu ambao iwapo majanga yatatokea watu wasidhurike.
 
Hzo story unaziona na kusikia kwenye moves ndugu hz calamities preparedness usifanye mchezo ndio nyie wakijaza usalama na wanajeshi mnanzisha uzi wa kuwasema

Kubalini kushaurika. Mnajifanya wabishi majanga yakija hakuna wa kusaidia.
 
Sawa hadi pale utakupokuta umetengewa bajeti 200m. Kati ya hizo umepewa maelezo toka juu 150m ziende sehemu ambao haina uhusiano wowote na emergency preparedness halafu halafu hiyo 50m unaambiwa kuna vikao na drill zitakula 45m. Utabaki na 5m ya kutayarisha proposal kwa wadau kuomba msaada kwa ajili ya mafunzo na vikao vya emergency preparedness. Tatizo siyo mipango tatizo ni viongozi.
 
kutokana na idadi ya watu kuongezeka .kitengo cha uokoaji kitenganishwe.kiwe kitengo cha kujitegemea chenyewe. kiajili watu wake na wapewe mafunzo kivyake. tofauti na sasa mtu anapelekwa kikosi cha uokoaji na zimamoto kama adhabu au kumkomoa akiwa hakusanyi rushwa vizuri.
 

haaaaaaaaa haaaaaaaaa
 

Kweli kabisa. Nadhani Bajeti ni ndogo na huwa inaliwa na wajanja. Maana mara nyingi kwenye maafa raia wema ndio hutoa michango.
 
Kweli kabisa. Nadhani Bajeti ni ndogo na huwa inaliwa na wajanja. Maana mara nyingi kwenye maafa raia wema ndio hutoa michango.
Tunachukulia kwa uwepesi sana suala zima la uchaguzi na demokrasia lakini kuwa na viongozi waliopatikana kwa njia zisizokuwa za haki zina madhara makubwa sana kwetu wananchi.
 
Hii tabia yao, ya kufika kwenye uokozi late ifike mwisho sasa. Kwa janga la Kariakoo walichelewa, wasiseme foleni. Huwa kuna V8 zina ving'ora, au hazina zinapita au kupitishwa na askari barabarani. Ndiyo itakuwa kwenye tukio zito hivyo.

Yaani kiongozi akitaka kupita njia inasafishwa, janga likitokea wanasema foleni jinsi ya kufika. Haya madaraja, wanayoyatengeneza itawacost siku isiyo na jina.
 
Umeongea kitu moja muhimu sana ambacho huenda ndio kinatukwamisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…