Ningekuwa na maamuzi kwenye club ya Simba, ningemuondoa msemaji wa club ya Simba, Ahmed Ally

Ningekuwa na maamuzi kwenye club ya Simba, ningemuondoa msemaji wa club ya Simba, Ahmed Ally

Inasemwa kwamba kazi ya afisa uhusiano ndio kazi ngumu kabisa huku duniani. Kazi hii inahitaji mtu mwenye uelewa wa mambo haswa yale ambayo atakuwa akiwashirikisha watu kuhusu kampuni, taasisi na mashirika ambayo ndio anafanyia kazi.

Kwa mfano. Afisa uhusiano wa jeshi la polisi. Msemaji wa jeshi la wananchi. Afisa habari wa TRA. Msemaji wa ikulu nk.

Unapokuwa kwenye nafasi ya afisa uhusiano wa taasisi yoyote unaweza kuifanya taasisi ikaonekana inafanya mambo hake vizuri au vibaya. Ndivyo ilivyo kwa msemaji wa klabu ya simba ya dar es salaam ndungu Ahmed Ally.

Kupitia mitandao ya kijamii, Ahmed Ally amekuwa akionekana akiizungumzia Club ya Simba kimzaha mzaha, kiasi kwamba Club ya Simba inaonekana kituko kupitia yeye.

Kwa jinsi navyomwona, yeye ndio ananufaika zaidi kuliko Club ya Simba. Taarifa zake nyingi zimekuwa ni za kimipasho zaidi kuliko zile official club statement ambazo uwasilishaji wake pia unatakiwa kuwa na nidhamu.
Uwasilishaji wake wa taarifa umekaa kitambotambo na kujidaijidai na ni kwa sababu ya kukosa ubunifu na matokeo ya kuigaiga watu wa aina ya kina Hadji Manara.

Ahmed Ally anajinufaisha yeye kwa mgongo wa club ya simba kwa kutaka sifa hata kama ni za kijinga ili mradi apate follers wengi huko insta na facebook.

Ningekuwa na mamlaka, ningempiga chini huyu jamaa.
Tuma maombi umng'oe Ahmed Ally inaonesha wewe ni bora zaidi, tatizo una wivu tu
 
Tangu hizi nafasi za usemaji wa vilabu kuanza tuna msemaji mmoja tu ambaye amefit kwenye hiyo nafasi.
Thobias Kifaru wa kule Manungu Turiani.

Wote wengine, Ally Kamwe, Ahmed Ally na Hadji Manara ni watu wa taarabu na mipasho.
Ligalambwike
 
Hawa wote Mm nawaona ni wale wale, hivyo naona mtoa mada ni shabiki wa Yanga hvy hawezi kuona tatizo kwa Kamwe.
Ila binafsi hao wote Kamwe na Ahmed wanafanya kazi zao vzr mana ndivyo mashabiki wao wanavyotaka.
Sema wewe ndio unataka hizo comedy usitusemee wengine
 
Mashabiki wenyewe wajinga unataka wawe na msemaji mwenye akili,mjinga huongozwana mjinga,football ni mchezo wa kihuni huku africa so relax
 
Kuna kitu hakiko sawa ktk nafasi ya usemaji teams hapa Tz..... Kuna haja ya kushughulika nalo kwa ajili ya AFYA ya SOKA la TZ..
Kuna namna hawa wasemaji wanawaaminisha mashabiki , overating ya wachezaji, un realistic expectations etc. Wanajitahidi kupata media attention bila kujua wanaharibu. ....Wanavyomuelezea KOCHA, au mchezaji ni tofauti na actual performance zao., pressure ni kubwa mno. Wanaharibu.....
.hiii style ikemewe au kuzuiwa kwa wanaoweza kufanya hivyo..
 
Back
Top Bottom