Ningekuwa na maamuzi kwenye club ya Simba, ningemuondoa msemaji wa club ya Simba, Ahmed Ally

Inasemwa kwamba kazi ya afisa uhusiano ndio kazi ngumu kabisa huku duniani. Kazi hii inahitaji mtu mwenye uelewa wa mambo haswa yale ambayo atakuwa akiwashirikisha watu kuhusu kampuni, taasisi na mashirika ambayo ndio anafanyia kazi.

Kwa mfano. Afisa uhusiano wa jeshi la polisi. Msemaji wa jeshi la wananchi. Afisa habari wa TRA. Msemaji wa ikulu nk.

Unapokuwa kwenye nafasi ya afisa uhusiano wa taasisi yoyote unaweza kuifanya taasisi ikaonekana inafanya mambo hake vizuri au vibaya. Ndivyo ilivyo kwa msemaji wa klabu ya simba ya dar es salaam ndungu Ahmed Ally.

Kupitia mitandao ya kijamii, Ahmed Ally amekuwa akionekana akiizungumzia Club ya Simba kimzaha mzaha, kiasi kwamba Club ya Simba inaonekana kituko kupitia yeye.

Kwa jinsi navyomwona, yeye ndio ananufaika zaidi kuliko Club ya Simba. Taarifa zake nyingi zimekuwa ni za kimipasho zaidi kuliko zile official club statement ambazo uwasilishaji wake pia unatakiwa kuwa na nidhamu.
Uwasilishaji wake wa taarifa umekaa kitambotambo na kujidaijidai na ni kwa sababu ya kukosa ubunifu na matokeo ya kuigaiga watu wa aina ya kina Hadji Manara.

Ahmed Ally anajinufaisha yeye kwa mgongo wa club ya simba kwa kutaka sifa hata kama ni za kijinga ili mradi apate follers wengi huko insta na facebook.

Ningekuwa na mamlaka, ningempiga chini huyu jamaa.
We mamluki mkuu ... Umetumwa... Mbona unataka kuharibu ugali wa mtu? Yanini kutia mchanga kitumbua cha mwenzio? We mchawi wewe!!
 
Msemaji Tanzania alikuwa Antonio Nugaz bwana hao wengine ni wapiga kelele tu
 
Back
Top Bottom