Ningekuwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, kwa kuokoa muda, kuangalia ustawi wa chama na kutozalisha 'makundi', ningefanya haya upesi tu

Bado nasimama pale pale wawe wamepita Majambazi, Mafisadi, Wahuni na Masikini ila ' Maamuzi ' ya waliowapendekeza yaheshimiwe daima tu.
Hao majangili, mafisadi nk wapelekwe mahakamani haki itendeke, kamati ya ccm haina uwezo wa kuchunguza na kuhukumu mtu.
Hapana kuna watu wanasifa mbaya lkn wamepita.ni muhimu wachujwe.waliopita kuna majangili,mafisadi,majambazi n,k.
Kwa hiyo wajumbe wa chama hawana akili za kutambua nani mbaya nani anafaa?
Je ni Magufuli, Bashiru na Polepole ndio wenye macho mengi kuliko wajumbe wa matawi?
Bashiru hajifunzi kwa Nyerere alipomkata Salwat ,na Salwat akakimbilia chama cha Congress na kumshinda vibaya sana mgombea ubunge kupitia TANU.
 
Sasa Kaka,kwa hiyo Seleman Nchambi ameacha ujangili? Na kwa Sasa ana sifa zote za kuwa kiongozi?

Wewe ' Ujangili ' unaoufanya Kutwa hapo ' Kibaruani ' Kwako kwa ' Wahindi ' umeuacha?
 
Mrisho Gambo aliyetumbuliwa juzi juzi tu!!

Kakuibia ' Chupi ' yako au? Mmekalia ' Umbea Umbea ' tupu. Walioongoza Kura za Maoni ndiyo hao hao wapitishwe tu Kugombea Ubunge period.
 
Taarifa za ' Kimbea ' na ' Kipumbavu ' kama hii yako huwa sishughuliki nazo tafadhali na pia si za ' Hadhi ' yangu. Halafu unaonekana ni Mswahili!!!!
Ubarikiwe sana mkuu kwa dharau zako.....
 
Senseless!
 
Taarifa za ' Kimbea ' na ' Kipumbavu ' kama hii yako huwa sishughuliki nazo tafadhali na pia si za ' Hadhi ' yangu. Halafu unaonekana ni Mswahili!!!!
Mkuu umeulizwa swali zuri, na utapo lijibu litatupa muono wa jinsi gani ya kujipanga na kufanikisha kuwauwa watu ambao huonekana kama ni vigogo. Jibu Mkuu kama unataarifa zozote ambazo zitatufaa..
 
Uko sahihi kabisa.

Aliyepita kwenye kura za maoni ndio awe mgombea.
Hapana hayo maoni tu na kwenye maoni yapo mazuri na mabaya, yakiwa mazuri maoni yanachukuliwa yakiwa mabaya maoni yanatupwa tu hakuna ulazima wa kuyakubali. Mathalan mgombea anakubalika katika chama lakini hakubaliki na wala hauziki Kwa wananchi katika Jimbo, lakini kuna mgombea hakubaliki sana katika chama lakini anakubalika Sana Kwa wananchi ni rahisi kumnadi ana uwezo mkubwa wa kujieleza na kuzinadi sera za chama na kuzifafanua na kukiletea chama ushindi katika uchaguzi. Kwa maana hiyo chama makini kitateua mgombea ambaye akipelekwa kwa wananchi anakubalika, anaaminika na anaheshimika mbele ya jamii inayotaka awe muwakilishi wao bungeni. Chama hakiwezi kumteua mtu eti tu Kwa sababu wanachama wanampenda bila kujali mwenendo wa tabia zake,uwezo wake katika uongozi, uwezo wake katika kujenga hoja na kutolea ufafanuzi mambo mbali mbali ambayao wananchi watamtuma kwenda kuwaakilisha. Naunga mkono mgombea yeyote ambaye hana sifa za kiuongozi hana sifa za kukiletea chama ushindi akatwe tu. Katika chama wakati mwengine mgombea anaweza kushinda kwa sababu ya ushabiki tu au rushwa. Tumeona baadhi ya wabunge waliopita wakati wanachangia hoja fulani unajiuliza huyu kawaje mbunge hana uwezo hata wa kujadili kilicho mbele yake.
 
Huyu hakuomba kura wala hajulikani lakini ameongoza kura za maoni. Ni namna fulani ya uchaguzi. Kweli inawezekana kuna uwazi.
 

Attachments

  • VID-20200721-WA0018.mp4
    2 MB
Wanywe sumu ya panya ili panya wangwe nini... Wale tu bata maana kuna maisha nje ya kuwa watawala!
 
Naunga mkono hoja yako japo nataka uelewe Kwenye kura za maoni hizi ni moja ya michakato iliyojaa madudu kibao, ilikuwa ni heri kura za maoni Za 2015 kurudi nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…