Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Haya ni maoni yangu kwamba siasa ni ajira iliyotawaliwa na roho mbaya ushirikina na mauaji!!
Kama isingekuwa siasa mawazo asingekufa ,Wala mwandishi wa chanel ten daudi mwangosi asingekufa! Isingekuwa siasa Leo Ben saa nane angekuwa anawasindikiza watoto wake shule asubuhi na kwenda kuwachukua jioni!
Kuna mtu anaitwa mwanasiasa aliamua tu kuondoa roho ya mwenzake kwa sababu ya siasa !
Utamkuta huyo mtu anapeleka maburungutu ya pesa makanisani kutoa sadaka na kuchangia harambee mbali mbali isingekuwa siasa azory gwanda na watu kibao waliokutwa wanaelea baharini kwenye sandarusi yasingewakuta yaliyowakuta.
Leo deus soka hajulikani alipo na wengine wengi kama mzee kibao wameuliwa kinyama sana sababu kubwa ni siasa ! Sijamsahau mawazo na wengine wengi Sana !
Siasa imebeba ma vampire na sio watu wenye utu! Wanasiasa hawakutakiwa hata kuingia makanisani kabisa na ndio wanashinda mitandaoni kukosoa dini wakitaka zifanye wanavyotaka wao !
Leo ni uchaguzi wa serikali za mitaa ajabu Kuna mahali nasikia kura zimepigwa kabla vituo havijafunguliwa ! Aliyefanya hivi utamkuta jumapili kanisani au msikitini anaomba Dua !
Siasa ya nchi yetu imetawaliwa na shetani anayemaliza vijana wetu Kila uchao ' tunasikia kigoma watu wamepotea hawajulikani walipo sababu ni uenyekiti wa serikali za mitaa ,mungu awape ufunuo viongozi wa dini wanasiasa sio rafiki wa mungu na sadaka zao ni ubatili mfupu
Tujifunze kwa nabii eliya na mfalme ahabu ,eliya hakumuunga mkono Bali alipambana nae