Ningekuwa sina ajira ningefanya jambo moja ambalo lingenipelekea kuajiriwa haraka na kwa urahisi

wa magari umeenda mbali hao wa simu tu wana connection huko huko
Polisi wengi wana njaa sana. Ukitaka wakuone jembe, wapelekee deal la pesa siyo wahalifu.

Kuna kipindi polisi wa pale Msimbazi walikuwa wanashirikiana mpaka na wale omba omba wa nje ya geti.

Omba omba anaomba kibabe usipompa anakuzingua halafu polisi wanaingilia. Unatolewa upepo.

Wengine hasa wale wa magari ya doria ndio kazi yao kukamata watu kwenye maeneo ya starehe usiku, wanakuweka kwenye difenda wanazurula na wewe mpaka saa 8 usiku mkubwa mpaka uwape pesa ndio wanakuachia.

Sasa watu kama hao ukiwashirikisha uhalifu wanaona unataka kuwapotezea muda tu.
 
Hizo movie za kikorea zinawapeleka pabaya aiseee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16]
 
Kibongobongo ungeishia kutatuliwa rinda. Maisha ya u snitch, vipo vitengo hiyo ndio kazi yao, na zaidi kama mdau mmoja alivyokuelekeza hapo juu. Unaweza kupeleka report kwa mfadhiri wao ikala kwako. Bora una ajira mkuu we deal na mambo zako...hiyo ajira uliyoitaka ni ngumu kuliko ugumu wenyewe maana utaiponza mpaka familia yako.
 
Unaweza kukuta mkubwa wao ni mtu unayefahamiana nae ila hujui
 
nakwambia wakianza kutoa ajira upya na ww ungekuwa huna basi kwa akili uliyonayo usingepata kabisa
 
Mkuu ni series gani imeku motivate? [emoji23][emoji23][emoji23] hiyo nguvu yakufuatilia watu kwanini usiiweke kwenye udalali ukawa unafuatilia bidhaa?
 
Kabla ya kukamilisha upelelezi wako ungekua umeshatangulia mbele za haki
 
Kwa hiyo, tuseme hiyo ajira uliyonayo umeipata kwa kufanya hayo?
 
nimesoma hii post, dah nmejikuta nacheka kwa nguvu kinyama
 
Miongoni mwa mambo unayotakiwa kuwa mwangalifu sana ni mambo ya uhalifu. Ukikurupuka inaweza kugharimu uhai wako.

Unaweza kufanya uchunguzi wako ukifanikiwa kuwajua members ukaamini umewafahamu wote, kumbe kuna makamanda wakuu (VIVULI) watoa maagizo hujawajua. Unaweza kukutana na OCD, RPC au yeyote ukamueleza KUMBE YEYE ni miongoni mwao.

Amini kwamba makundi ya kijambazi huwa yanayosimama mgao kwa hao uliowataja.

Na kwa asilimia kubwa vyombo vya ulinzi na usalama vina taarifa nyingi sana ya vitendo vya kihalifu, na wanawajua members wengi mnooo vikundi hivyo.

Mara nyingine huwa vinaachwa mahususi tu, kwa sababu maalumu au hata bila sababu.
 
Kwanza hao OCD na RPC ndio wakuogopwa kabisa usijichanganye kabisa
 
Mwaka mzima unachunguza hilo genge la wahalifu, pesa za izo shughuli zako unatoa wapi??
Una uhakika hiyo ni njia ya kupewa ajira??
Ni ajira gani hiyo ujayoitaka, kwa hapo unakua umesaidia polisi, mbona ni wengi hutoa taarifa za kusaidia uchunguz na hawapati izo kazi
 
Kuna watu wakishiba wanasumbua sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…