Chambusiso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 2,592
- 4,640
Wanabodi,
Mama Samia ni Rais na kiongozi wa taifa letu, ni msikivu na mnyenyekevu sana, mwenye subira na utulivu sana wa kusikiliza na kuchambua mambo kabla hajafanya maamuzi na anapofanya maamuzi yake anayasimamia, huku akitoa nafasi ya kukosolewa sana bila kuwa jazba wala kutumia manguvu makubwa aliyonayo. Kumbukeni kwa katiba iliyopo angekuwa mtawala kama waliotangulia leo hii na mijadala migumu inayoendelea tungeshaanza kusikia wakosoaji wanakutana na matokeo hasi tena gizani.
Nimefungua uzi huu kwa watu positive tu wanaoweza kusema mambo yanayojenga watupie hapa, najua sisi ndio wananchi wenyewe na wawakilishi wetu wanajiwakilisha wenyewe tu (kule bungeni) na matumbo yao, lakini mama huyu alisema anapita JF mara kwa mara, so tukiweka mawazo positive hapa naamini yeye na team yake wataokota machache na watachagua ya kufanyia kazi (hatuna bunge), so bila jazba wadau karibuni tushauri mambo makubwa yanayoweza kuleta "transformation" sio ya kutibu njaa, fikiria nchi yako baada ya miaka 30-50 itakuwa wapi kama mawazo yako yatafuatwa au kutumika hata asilimia ndogo tu. Vijana wenye mihemko wanaweza kwenda kwenye nyuzi zingine tu sio lazima wachangie hapa.
Langu nalosema, ningepata nafasi ya kumshauri Mama Samia, Mheshimiwa Rais, ningemwambia apeleke vijana kusoma nje - hata kama uchumi wetu ni mgumu kiasi gani mama rudisha utaratibu wa zamani kupeleka vijana hata 100 kila mwaka wakapate exposure na elimu ya kuja kubadilisha mindset zetu, tumekuwa watanzania tunaofanana wote, hamna msomi wala asiyesoma wote tuna mawazo yanayofanana 100% peleka watu waje na upeo mpya, kama Nyerere alivyofanya miaka ya nyuma, watu waje wawe wataalam, waalimu, viongozi etc. warudi na maarifa mapya, hautapata matokeo mwaka huu au ndani ya uongozi wako lakini miaka 20-30 ijayo kama wamesoma watu angalau watu 3000-5000 nje ya mfumo wa elimu wa kwetu, tutapata mabadiliko makubwa. Ulisema unafungua nchi, fungua sasa na kwenye maarifa. Yaje maarifa mapya na yatumike kwa vizazi vijavyo achana na chawa wanaongalia leo tu!
Wewe ungepata nafasi ungemshauri nini?
Karibuni sana wadau.