Ningepata nafasi ya kushauri TAMISEMI

Ningepata nafasi ya kushauri TAMISEMI

opondo

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
526
Reaction score
1,321
Nitoe ushauri kwa upande wa ajira hizi za ualimu na wataalamu wa afya
IMG_8435.png

Mpaka sasa kada ya ualimu nafasi ni 9800 na waombaji wa hiyo nafasi ni laki moja na elfu kumi na tisa (119000). Roughly ni kwamba nafasi moja inagombaniwa na watu 12, pia upande wa afya naona hali sio mbaya saana kama kwenye kada ya ualimu hao wanaonekana ni wengi maana watu wa sociology wameruhusiwa kuomba kwahiyo wanafanya hiyo idadi ya 39,000 kuonekana ni wengi.

Endapo serikali ikiamua kutoa ajira 10,000 kila mwaka itachukua miaka 12 kuwamaliza waliopo, then kumbuka mwaka huu pia wapo wanaograduate si chini ya 20,000.

Ushauri wangu kwa TAMISEMI kupunguza idadi hii ya walimu maana mwakani watafika laki na nusu. Kuna course ambazo zilianzishwa kwa nia njema kwa ajili ya kupata waalimu wa science wa haraka mfano special diploma mtu anamaliza form four anaenda kusoma ualimu kwa miaka mitatu. Inabidi zisitishwe kwanza twende na mfumo wa kawaida ambao ni certificate, diploma, na bachelor degree.

Kwa mfumo huo utasaidia rate ya wanaomaliza kwenye kada ya ualimu kupungua huku wakiendelea kuwaajiri wale waliopo mtaani.

IMG-20220504-WA0070.jpg
Hapo ni mathematics ambalo hilo somo zamani walimu walikua hawapo lakini kwa sasa wamekua ni wengi kama masomo mengine. Pia ushauri wa wahitimu waliomaliza na waliopo bado vyuoni wanasoma ni vyema wakafikiria nje ya box zaidi maana kwa uhalisia serikali haiwezi kuajiri watu wote kuepusha na kulalamika ni vyema kuwaza ujasiriamali na kilimo kwa kutengeneza vikundi vidogo vidogo kwa ajiri ya kupewa mikopo.
 
Watu ndo waache kukariri maisha kwa kukimbilia ualimu wakiamini wakimaliza watapata ajira kiurahisi.

Kuna wengine wamesoma kozi ya ualimu kwa shinikizo toka kwa wazazi wao kwamba wakimaliza watapata ajira kiurahisi kuliko wakisoma kada nyingine.

Ni wakati sasa wa vijana kusoma na kozi zingine mana kozi ya ualimu ishakua jau.
 
Kozi ya ualimu ilivurugika hapo 2016 kuendelea ila tofauti nyuma kidogo ilikua ni inawaacha asilimia chache pasipo ajira. Wengi walio omba maombi ni kuanzia 2016 na kuendelea. Wasilaumiwe
 
Watu ndo waache kukariri maisha kwa kukimbilia ualimu wakiamini wakimaliza watapata ajira kiurahisi.

Kuna wengine wamesoma kozi ya ualimu kwa shinikizo toka kwa wazazi wao kwamba wakimaliza watapata ajira kiurahisi kuliko wakisoma kada nyingine.

Ni wakati sasa wa vijana kusoma na kozi zingine mana kozi ya ualimu ishakua jau.
Hata hao wa afya nao wamerundikana.

Kikubwa inabidi watu wakubaliane na hali halisi maana suala la ajira limeshakuwa changamoto, hivyo mtu anaposoma kozi yoyote iwe akili kumkichwa.
 
Tamisemi inawafanyia utani waombaji! Hizo siku wanaongeza kwa lengo gani hasa? Mbona idadi ya waombaji na hizo nafasi zenyewe, haviendani?

Ifikie wakati waache kuchezea akili za vijana wetu.
 
Tamisemi inawafanyia utani waombaji! Hizo siku wanaongeza kwa lengo gani hasa? Mbona idadi ya waombaji na hizo nafasi zenyewe, haviendani?

Ifikie wakati waache kuchezea akili za vijana wetu.
Bora mtu akwambie ukweli mchungu kuliko uongo wa kubembeleza, najiuliza hao laki na 20 wanashindwa kuwapata wenye vigezo
 
Ni mda gan Tamisemi hutumia kupitia maombi hadi kutangaza majina ya waliopata
 
Back
Top Bottom