Ningependa kujua Ada ya Shule hizi za Sekondari

Ningependa kujua Ada ya Shule hizi za Sekondari

Hii Canossa hapa Tegeta Primary tu inazidi 10M. Sasa sijui Secondary itasoma ngapi...
Okay nashukuru sana kwa taarifa mkuu. Nitaendelea kufuatilia mpaka nitapata size yangu yenye ufundishaji/elimu bora.

Asante sana!
 
Shule nzuri sana hizi..hakika mzazi au binti anayesoma hizo shule anajivunia.

Anyway elimu bora ndio msingi..achana na hizi shule za bora elimu..ila mtoto kilaza..ili asihoji wanapoiba kura waziwazi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Shule nzuri sana hizi..hakika mzazi au binti anayesoma hizo shule anajivunia.

Anyway elimu bora ndio msingi..achana na hizi shule za ccm za bora elimu..ila mtoto kilaza..ili asihoji wanapoiba kura waziwazi.

#MaendeleoHayanaChama
Asante sana kwa kunitia moyo mkuu jiwe angavu

Mimi nilisoma shule ya tarafa (kabla ya shule za kata) na nilikuwa first intake. Pamoja na kupambana na nikafaulu vizuri sana kidato cha nne lakini ninajua weakness ya shule hizi!
Kama mzazi una uwezo basi huna budi kuwapa vijana elimu bora kutoka kwenye mazingira mazuri.
 
Hivi hii ni kweli kwa CSEE 2023?
malisa_gj_1675252053492310%20(1).jpg
 
Mkuu nenda na namba 1,2, 4, 6, na 11. Pia Ongeza Bright Future. Kabla ya kuuliza Ada kazana kumuandaa huyo binti yako. Kuzipata shule shule hizo ni lazima mtoto awe very bright na well prepared in Maths and Science and General Studies combined. Ada zao jiandae kuanzia 4-4.5 million Kwa nyingi. Ila pia nenda hizo shule ulizia current Ada watakupa clue. Ila pia kama binti yako yuko average basi hakikisha pia anafanya interview kwa shule nilizoacha hapo kwenye orodha yako Ongeza na nyingine nzuri angalia trend ya F4 results. Ukiegemea Sana top schools unaweza kujikita mtoto hajapata hata Moja na interview pia zimepita shuke nyinginezo. Hapo mzazi unachanganyikiwa sana. Pia kuwa Makini na tarehe za interview maana huwa zinagongana bàadhi ya shule hivyo ni kufanya maamuzi sahihi kabisa wakati wa kuchukua form. Miaka miwili hii hakikisha mtoto anapata usaidizi mkubwa mno kwenye masomo shuleni na extra akiwa nyumbani.
. All the best.
Umeandika kwa Hekima Sana, hii struggle ya kutafuta shule inaonekana unaifahamu vizuri sana. Natamani kila mwenye mipango ya kutafuta shule apitie hili jibu lako.
 
Wazazi, mida wa kuwatafutia shule vijana wetu kwa ajili ya kidato cha kwanza 2024 ndiyo huu. Naomba tuendelee kupeana taarifa ya wapi form zao zinapatikana!
 
Wakuu habari. Nina binti yangu hapa yupo darasa la sita miaka 2 ijayo atakuwa anaingia ngazi elimu ya secondary.

Kwa sasa nimeanza kujiandaa kuhakikisha anazidi kuwa na uelewa mzuri wa darasani ili aweze kufaulu vizuri mitihani yake ya mwisho na ile ya kujiunga shule bora kwa elimu ya secondary (O level).

Kwa maana hiyo ningependa kuulizia ada (full package na michango mingine ikiwezekana) kwa shule zifuatazo: -

1. Precious Blood Secondary school
2. Anwarite Girls Secondary School
3. Kifungilo Girls Secondary School
4. St. Mary's Mazinde Juu Secondary School
5. St . Marie Eugenie Secondary School
6. Cannosa Secondary School
7. St. Mary Goreti Secondary School
8. St. Monica Moshono Girls' Secondary School
9. Bethel Sabs Girls Secondary School
10. Marian Girls Seconday School
11. St. Francis Girls

Kwa namna ambavyo nimezifuatilia hizi shuke kwa muda mrefu, nahitaji binti aje asome kati ya shule hizi. Mpaka sasa naendelea kumjengea mzingira ya kufaulu mitihani yao ( uwezo anao).

Je, mnaweza kushare gharama zao ili nijue ni kiasi gani ili niendelee kujiandaa vizuri.

Asanteni.
Nina uzoefu na shule mbili tu hapo, Precious blood na Mazinde juu tu
 
hongera inaonekana una toto wa kike, vip akiba ya kuuza ubuyu imetosheleza kumpeleka huko
 
Nipo kwenye harakati za kufanya interviews za kujiunga na shule hizi na binti yangu, mpaka sasa majibu yashatoka kwa shule mbili, moja kashapata na nyingine kakosa na tunaendelea na interviews ili baadaye achague kwa zile atakazopata.

Tukifikia mwisho nitaleta mrejesho wa struggle hii ya kutafuta shule ili iweze kumsaidia mzazi mwingine atakayepitia uzi huu.

Asanteni.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Aina nyingine ya "MIKOPO KAUSHA DAMU"

Kama kipato chako Cha wastani chamoto utakiona for another 4 coming years
 
Back
Top Bottom