Ningeshauri suala la Manara liishe hivi...

Ningeshauri suala la Manara liishe hivi...

MUSHEKY

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
2,812
Reaction score
2,760
Moja kwa moja kwenye mada,

Toka kutolewa kwa hukumu iliyomfungia aliyekua msemaji wa klabu ya yanga ndugu Haji Sunday Manara kumekua na makundi mawili ama moja linahisi Manara ameonewa ama jingine linahisi TFF wapo sahihi

Nirudi nyuma kidogo kuwakumbusha mashabiki wa mpira kua sheria yoyote ya taasisi yoyote ile ndani ya Tanzania haikinzani na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mantiki hiyo katiba yetu ndio sheria mama ya sheria zote hapa nchini

Kwa kua sheria na kanuni za TFF zilitumika kumuadhibu kiongozi huyu wa kabumbu hapa nchini sanjali na zile zilizotumika pia kuwaadhibu kocha Mbwana Makata wa Dodoma jiji na mtangazaji Shafi Dauda ni kanuni hizo hizo za TFF

Kwa heshima na taadhima nimshauri ndugu yangu Haji Manara afuate sheria na kanuni zile zile za TFF kuitafuta haki yake kama anahisi ameonewa

Ipo wazi na ifahamike mlalamikaji baada ya hukumu kupita alipewa fursa ambayo ni haki yake kimsingi kukata rufaa ndani ya muda uliowekwa kisheria na yeye mwenyewe anajua kua muda huo ukipita hakuna cha ziada kwake zaidi ya watoa hukumu kukoleza wino wa hukumu hiyo

Jambo ambalo wanafamilia ya mpira wanapaswa kumshauri haji ni kwamba malumbano anayoyaendeleza kwenye media na kutafuta uungwaji mkono na followers wengi ni kupoteza muda tu kusiko na msingi wowote

Aidha ipo hoja ya msingi ya Manara kwamba Karia alimtukana n.k, kama Sunday anaona iko hivyo anapaswa kutumia sheria zile zile kumshtaki Karia na kwa kua sheria ni msumeno karia ataitwa mbele ya jopo na ushahidi wa Manara utasikilizwa na hukumu itatolewa ikishindikana atakata rufaa kwenye vyombo vyenye mamlaka zaidi n.k

Mwisho kabisa nimeona mahali Haji manara anamtaka waziri wa michezo kuingilia kati suala lake na TFF akiamini kwamba mwanasiasa huyu atainfluence maamuza ya TFF dhidi yake

Nimuombe Manara aachane na majaribio ya namna hiyo kwani sheria za mpira Duniani "FIFA" zinaharamisha kabisa masuala ya hukumu za kisoka kuingiliwa na wanasiasa na moja ya adhabu ni kuifanya nchi husika kufungiwa kushiriki michuano yoyote inayotambulia na chombo jicho cha kuendesha kandanda la Dunia

Niseme tu watanzania tunaupenda mpira na hatupo tayari kwa hilo na nawashauri watanzania tuufunge mjadala wa Manara kwa kumshauri asitafute suluhu ya jambo "lake" kwa kuitisha press za mara kwa mara ama kulalamika juu ya maamuzi fulani bali afuate taratibu za kisheria hata ikiwezekana kimya kimya akate rufaa ama vinginevyo

Hayo ndio yanafanyika hata kwenye hukumu za raia kwenye mahakama za kiraia, hutapata haki yako kwa kurandaranda huku na kule kudai uamuzi wa mahakama si sahihi

Nawasilisha
 
Moja kwa moja kwenye mada,

Toka kutolewa kwa hukumu iliyomfungia aliyekua msemaji wa klabu ya yanga ndugu Haji Sunday Manara kumekua na makundi mawili ama moja linahisi Manara ameonewa ama jingine linahisi TFF wapo sahihi...
Manara amepewa hukumu ya kukomoa ambayo ipo nje ya sheria za TFF,

Wampe nakala yake ya hukumu basi
 
Moja kwa moja kwenye mada,

Toka kutolewa kwa hukumu iliyomfungia aliyekua msemaji wa klabu ya yanga ndugu Haji Sunday Manara kumekua na makundi mawili ama moja linahisi Manara ameonewa ama jingine linahisi TFF wapo sahihi...
Manara ni mpumbavu mdogo mwenye wafuasi wengi wajinga. Case closed.. karibuni Ontario, CA!
 
Manara Ni tahira .. ndio taabu ya kukosa elimu anatuma ujanja ujanja wa mjini tuu...
Wewe kama ni msomi na mwerevu kwa nini ukili kuzidiwa na taahira ujanja ujanja wa mjini? Wewe ndiye kubwa la mataahira.
 
the saga continues... Manara akimbize hii ishu kimya kimya
 
Kupewa hukumu kwa kanuni "ambazo hazijasajiliwa" ni hoja nzito na muhimu sana ya kushinda rufaa.

Akate rufaa kwenye mamlaka za juu (za kisoka) atapata haki yake.

Simple.
Yeye ni nani hapa Tanzania?.
 
TFF NA 'KICHEKESHO' CHA SAKATA LA HAJI MANARA

Mbali na mambo mengine katika sakata hilo, bado pia kuna mengine ambayo ni pamoja na haya yafuatayo:

(1) Katika Kanuni zote za adhabu za TFF, hakuna hata moja ya kumtoza mtu shilingi milioni 20;

(2) Katika mashtaka yale, mlalamikaji alipaswa awe Wallace Karia mwenyewe na siyo Sekretarieti ya TFF ambayo ndiyo inailipa posho zote Kamati ya Maadili, hivyo lazima itekeleze maelekezo inayoielekeza kama mwajiri.

Hapa kwa tafsiri nyingine, mlalamikaji hakuwa Karia ila Sekretarieti ya TFF ambayo haijasema inahusikaje na ugomvi wa Manara na Karia wala kuwa ina maslahi gani na malumbano hayo, hasa pale ambapo yule anayedaiwa kudhalilishwa hakulalamika.

Mwisho katika hili, kwa vile Kamati ya Maadili inalipwa posho zote za shughuli zake na Sekretarieti ya TFF zikiwemo za kusikiliza mashtaka, hapa maana yake ni kwamba yenyewe ndiyo iliyokuwa mlalamikaji, shahidi wa upande wa mashtaka na hakimu aliyetoa hukumu hiyo;

(3) Karia aliyepaswa awe ndiye shahidi mkuu wa upande wa mashtaka, kisha wengine wote wabaki kuwa mashuhuda, lakini hakuitwa wala kufika ili kutoa ushahidi wake;

(4) Kamati ya Maadili ya TFF haijasema chanzo cha Manara kufanya hivyo wala haijataja mashahidi waliofika mbele yake ili kutoa ushahidi wao dhidi ya Manara.

Hii ni kwa sababu, inawezekana Manara alikuwa anajihami au kujibu mapigo baada ya kuchkozwa, kutukanwa au kudhalilishwa kwanza na Karia; na

(5) Kwa mujibu wa Sheria za TFF, anayefikishwa katika Kamati ya Maadili kwa masuala ya soka ni kiongozi wa kuchaguliwa wa Klabu, Chama cha Soka cha ngazi yoyote, chombo cha Shirikisho la Soka au mwenye nafasi ya kuteuliwa iliyopo kwenye muundo wa Shirikisho la Kandanda Duniani au FIFA.

Nafasi ya "Mhamasishaji" kama aliyonayo Manara haipo katika muundo wa FIFA, hivyo anaweza tu kuwa ni shabiki wa Yanga ambaye hawezi kushtakiwa katika Kamati ya Maadili ya TFF ila mahakamani kama alimdhalilisha Karia.

Alipaswa ashtakiwe Kituo cha Polisi na Karia mwenyewe, kisha apelekwe mahakamani kama mtu binafsi na mlalamikaji akawe shahidi wa Jamhuri kama mtu binafsi na siyo kama Rais wa TFF.

Katika kutekeleza mfumo na muundo wa FIFA, Yanga yenyewe ina Afisa Habari wake, Hassan Bumbuli. Huyo ndiye anaweza kushtakiwa katika Kamati ya Maadili ya TFF.

Kutokana na hali hiyo na hata vinginevyo, swali linalozuka hapa ni je, tangu lini Manara ni kiongozi wa kuchaguliwa au afisa wa kuteuliwa wa Yanga kwa kuzingatia muundo wa FIFA?

Ni cha kujifunza hapa na kukishika kila mshabiki na kukipigia kelele siku zote hadi Manara atakapoachiwa huru ni wajibu ni kwa nini mashabiki au shabiki anaporusha chupa ya maji uwanjani inaazibiwa klabu na si mhusika why Manara ahukumiwe kama yeye wakati anaipigania timu.

Kesi hii tutashinda kabla ya tar.6.8.2022.Tumuombe Mungu
 
Back
Top Bottom