Ningeweza kupandisha uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza katika bidhaa mpya zenye thamani kwa sasa duniani

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Kama kichwa cha bandiko hili kinavyojieleza kwamba.

"Ningeweza kupandisha uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza katika bidhaa mpya zenye thamani kwa sasa duniani".

Ndugu zangu,
Naomba nianze kwa kueleza sababu moja inayofanya Gross Domestic Product per capital yetu kuwa ndogo.

Gross Domestic Product (GDP) yetu per capital ni ndogo mnoo na hii ni kwasababu hatuzalishi bidhaa mpya ambazo zina thamani kwasasa bado tupo na bidhaa za zamani zilezile.

Hebu Tujiongeze tuanze kuzalisha bidhaa mpya ambazo zinahitajika na mataifa mbalimbali hizi ndio zenye thamani kubwa kwa sasa.

Tuzalishe bidhaa zifuatazo
1. Natural Gas, LNG:

2. Kemikali: Kemikali zinazotokana na gesi mfano ammonia, Sulphuric acid, mbolea mbalimbali, methanol, n.k:

3. Gesi ya Helium. Hii gesi ina dili kuliko gesi zote duniani kwasasa.

4. Madini ya Lithium kwaajili ya betri za magari ya umeme.

5. Madini ya Nickel

6. Madini Cobalt

7. Madini ya platinum

8. Madini ya Chromium

9. Madini ya Manganes

10. Madini ya Copper

11. Nishati ya umeme (tuzalishe nishati kwa wingi tuwezavyo tuuze kwenye mataifa mbalimbali).

Tukiuza bidhaa hizo zenye thamani tutapata fedha nyingi zitakuza GDP yetu, mwishowe tutajikuta tunaacha kutoza kodi. Lakini hatuwezi kuacha kutoza kodi kwasasa kwasababu hatuna vyanzo mbadala vya mapato ya uhakika ya kuaminika ambayo yanaweza kufinance miradi yetu ya maendeleo na huduma za jamii katika taifa letu.

Hivyo tuweke mikakati huko kwenye bidhaa mpya. Lakini ili kulifanikisha hilo rasilimali watu ndio nyenzo muhimu kwenye kuzalisha hizo bidha mpya.

Tuna wataalam wa madini, wataalam wa mafuta na gesi tuwatumie ili kuwezesha uchumi wetu. Leo tunakimbizana na kodi za miamala ya simu ni kwasababu hatuna uwezo wa kuzigeuza rasilimali zetu kuwa pesa. Tuna madini, tuna gesi ya kawaida, tuna helium tunakwama wapi. Lazima tuwe serious tukitaka kufikia uchumi tunaoutaka ni lazima tuwekeze kwenye rasilimali zetu za asili na rasilimali watu.

Karibuni kwa maoni.

Je, wewe ungefanyaje?
 
kikubwa zaidi ni kuwekeza kikubwa kwenye elimu, hizo ulizotaja ni mapendekezo yako ila uchumi imara unatokana na wananchi wenyewe, ubunifu wao na umbali wanaoweza kwenda katika uchumi wa dunia kwa jumla, sasa shida uko kila mtu anawaza ajira na hata hio ajira anaiwazia kutoka serikalini kujaribu nchi zingine hawataki hata private sector za apa apa hawataki, kilio serikalini
 
Mkuu ili kuwekeza kwenye elimu zinahitajika fedha. Hizo fedha tutazitoa wapi bila ya uchumi mzuri.
 
kikubwa zaidi ni kuwekeza kikubwa kwenye elimu, hizo ulizotaja ni mapendekezo yako ila uchumi imara unatokana na wananchi wenyewe, ubunifu wao na umbali wanaoweza kwenda katika uchumi wa dunia kwa jumla, sasa shida uko kila mtu anawaza ajira na hata hio ajira anaiwazia kutoka serikalini kujaribu nchi zingine hawataki hata private sector za apa apa hawataki, kilio serikalini
Basi wananchi wa tengenezewe mazingira ya kufanya hvyoo vitu
 
Tatizo sisi hua kila kitu tunalalmikia serikali, we are lazy! yaaani hata swala la kua mbunifu unasema serikali iweke mazingira sasa sisi tuna faida gan? unazaliwa unasoma bure, unapewa mkopo na kazi unatafutiwa na serikali?
 
Yes,😂😂😂😂😂
 
Kama kichwa cha bandiko hili kinavyojieleza kwamba.

"Ningeweza kupandisha uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza katika bidhaa mpya zenye thamani kwa sasa duniani".

Ndugu zangu,
Naomba nianze kwa kueleza sababu moja inayofanya Gross Domestic Product per capital yetu kuwa ndogo.

Gross Domestic Product (GDP) yetu per capital ni ndogo mnoo na hii ni kwasababu hatuzalishi bidhaa mpya ambazo zina thamani kwasasa bado tupo na bidhaa za zamani zilezile.

Hebu Tujiongeze tuanze kuzalisha bidhaa mpya ambazo zinahitajika na mataifa mbalimbali hizi ndio zenye thamani kubwa kwa sasa.

Tuzalishe bidhaa zifuatazo
1. Natural Gas, LNG:
2. Kemikali: Kemikali zinazotokana na gesi mfano ammonia, Sulphuric acid, mbolea mbalimbali, methanol, n.k:
3. Helium:

4. Madini ya Lithium kwaajili ya beteri za margari ya umeme.

5. Madini ya Nickel

6. Madini Cobalt

7. Madini ya platinum

8. Madini ya Chromium

9. Madini ya Manganes

10. Madini ya Copper

11. Nishati ya umeme (tuzalishe nishati kwa wingi tuwezavyo tuuze kwenye mataifa mbalimbali).

Tukiuza bidhaa hizo zenye thamani tutapata fedha nyingi zitakuza GDP yetu, mwishowe tutajikuta tunaacha kutoza kodi. Lakini hatuwezi kuacha kutoza kodi kwasasa kwasababu hatuna vyanzo mbadala vya mapato ya uhakika ya kuaminika ambayo yanaweza kufinance miradi yetu ya maendeleo na huduma za jamii katika taifa letu.

Hivyo tuweke mikakati huko kwenye bidhaa mpya. Lakini ili kulifanikisha hilo rasilimali watu ndio nyenzo muhimu kwenye kuzalisha hizo bidha mpya.

Tuna wataalam wa madini, wataalam wa mafuta na gesi tuwatumie ili kuwezesha uchumi wetu. Leo tunakimbizana na kodi za miamala ya simu ni kwasababu hatuna uwezo wa kuzigeuza rasilimali zetu kuwa pesa. Tuna madini, tuna gesi ya kawaida, tuna helium tunakwama wapi. Lazima tuwe serious tukitaka kufikia uchumi tunaoutaka ni lazima tuwekeze kwenye rasilimali zetu za asili na rasilimali watu.

Karibuni kwa maoni.

Je, wewe ungefanyaje?
ukishataja tu "madini" au "gas" jua kwamba wenye uwezo/mitaji kuyachimba na kupeleka kwenye soko la dunia ni hao hao wazungu ambao lazima uwalambe viatu, wakupe masharti ya kuruhusu ushoga na usagaji, wakupe masharti ya democrasia isiyo na mipaka...halafu waingie kukuibia. ukoloni mambo leo hautakuja uishe, mwenye nacho hautakuja umkute na ateendelea kukupangia mipango ya kukutawala tu milele.
 
Ni rahisi sana kuongea...sia ajabu ukipata bahati ya kuongoza hii nchi ndani ya wiki tu ukaomba kuachia ngazi....Tatizo la Tanzania ni tatizo la Africa nzima kasoro northen Africa kwa weupe waarabu....either wakoloni walifanya kitu ili tuendelee kuwa watumwa na watawaliwa au waasisi kipindi cha uhuru walikosea kuchagua njia ya kwenda nayo na sasa solution ni kuanza upya..

Hayo yote uliyotaja yanahitaji mitaji, teknolojia na maarifa ambavyo vyote hatuna mwisho wa siku....tukijaribu kuvitafuta tunajikuta hatuna hela ya kula na matibabu mwishowe tunaamua kuchagua vya muhimu ili tusife na njaa wala magonjwa...
 
Tanzania imekosa viongozi bali ina watawala wako bize kuwaza ujinga badala ya mambo ya taifa.

Ngoja tumalize kampeni ya nyumba ni choo vijijini then tutaangalia maendeleo kwa kuongeza zaidi tozo kwenye miamala ya simu
 
Ningehalalisha kilimo cha bangi, tufanye liwe zao la biashara....nakwambia watu tungepiga hela sana...bangi ya Arusha ni ya kipekee nyie...wakiashaionja huko ughaibuni tunapeleka tani na tani ...kilimo ni uti wa mgongo wa taifa, tumelalia fursa tu kwa misingi isiyokuwa na tija.
 
Mazingira ya biashara yakoje tz Anza apo kwanza nakisha wafikile wale wasiolipa kodi
 
Ni rahisi sana kuongea...sia ajabu ukipata bahati ya kuongoza hii nchi ndani ya wiki tu ukaomba kuachia ngazi....Tatizo la Tanzania ni tatizo la Africa nzima kasoro northen Africa kwa weupe waarabu....either wakoloni walifanya kitu ili tuendelee kuwa watumwa na watawaliwa au waasisi kipindi cha uhuru walikosea kuchagua njia ya kwenda nayo na sasa solution ni kuanza upya..

Hayo yote uliyotaja yanahitaji mitaji, teknolojia na maarifa ambavyo vyote hatuna mwisho wa siku....tukijaribu kuvitafuta tunajikuta hatuna hela ya kula na matibabu mwishowe tunaamua kuchagua vya muhimu ili tusife na njaa wala magonjwa...
Baada ya wakoloni wazungu kuondoka wakoloni weusi wakajivika ukoloni mweusi kwa weusi wenzao.

Watu wa north Africa hawana natural resources nyingi Kama tulivyo sisi waafrika wa kusini mwa Sahara desert ila angalia maisha yao na sisi utapata jibu ukiangalia kwa umakini utagundua wale waarabu wa north Africa Wana viongozi na sio watawala.
 
nchi gani za waarabu north africa haina resources? nyingi zina mafuta na gas, na pia wapo karibu na ulaya hivyo kufanya biashara na ulaya pamoja na arabuni wameanza zamani sana na kujiimarisha. tofauti na sisi. ukija south africa, wana resources nyingi sana, dhahabu unayojidai hapa bongo unachimba, south kuna migodi ya kufa mtu na ni ya tangu enzi za Boer trek, kabla hata Tanganyika haijawepo kwenye ramani ya dunia.
 
Kwani sisi gesi hatuna? Nilicho sema kwenye jibu langu la msingi Ni kwamba hawana resources nyingi Kama sisi,Kama wao wameweza kuuza nchi za ulaya je sisi tumeshindwa vipi kuziuzia nchi za ulaya Kama wao?
 
ninachokubaliana na wewe ni hoja ya "leadership", cha pili, ni ukoloni mamboleo, hao wazungu wakitaka kuwekeza kwako wanataka wakutawale na wakufanye wapendavyo. pia, gas kwa mfano, kwa Africa unahitaji mwekezaji mkubwa sana, akifanikiwa kuweka NLG uweke mtandao wa kuiuza hapahapa Africa, kwasababu ulaya na Asia hakuna soko kubwa la gas za Tanzania na Mozambique, nasema hivi kwasababu Russia ina gas nyingi ajabu na wamesambaza mabomba karibia ulaya magharibi yote toka russia yameenda kusambazwa hadi majumbani ulaya yote, kwahiyo ana uhakika. ujerumani kwa mfano hawezi kuacha kutumia gas ya russia ambapo ni karibu kuipata ili aifuate hii ya Tanzania ambako itabidi atumie garama nyingi sana kusafirisha. Iran, na nchi kadhaa za uarabuni wanayo gas nyingi sana ambayo wanamuuzia China na India na tiger countries.

sisi tunachotakiwa kufanya, ni kuhamasisha mwekezaji aweke kiwanda kikubwa cha gas, ikipatikana itakuwa liability kwake yeye kutafuta masoko kulingana na mtaji aliouwekeza kwasababu atataka kurudisha gharama jambo litakalomfanya atafute soko kwa lazima, na soko kubwa lingekuwa la viwanda vinavyotumia gas hapahapa nchini au nchi jirani, viwanda vitakavyokuwa dependant kwenye gas. zaidi ya hapo tunaweza kuuza pia south africa na india kwa bei ya chini kwa ushindani na waarabu ambao wapo karibu kwao (kuisafirisha kwao ni nafuu kuliko kuisafirisha toka huku hivyo lazima tukubali kuliwa kidogo bei ipungue kama incentive), tukifanikiwa pia kuboresha bandari na miundombini mingine kuunganisha na landlocked countries, tutafanya nchi hizo zijenge viwanda tegemezi na hapa kwetu watajenga viwanda tegemezi kwa gas yetu au umeme wetu wa gas, na ndio litakuwa soko l a uhakika. maisha ya watu yakiboreshwa, watakuwa na nyumba bora na matumizi ya mkaa yatakufa kifo cha mende kila nyumba watatumia umeme au gas vyote toka hapahapa jambo litakaloongeza soko sana, matumizi ya magari ya gas pia in the long run. kwa misingi hiyo kidogo nitakubaliana na wewe.
 
Uchumi mzuri mtaupata wapi ikiwa wabunge ni akina wazungu& kibajaji # msukunani cjui landatumeyataka wenyewe
ila zungu kawaaibisha sana ngozi nyeupe, sio siri. nilifikiri wote huwa wa maana hadi nilikuwa natamani siku moja tujaribishe urais ngozi nyeupe hizi.
 
Kwani Zungu ni mzungu???? 😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kwani sisi gesi hatuna? Nilicho sema kwenye jibu langu la msingi Ni kwamba hawana resources nyingi Kama sisi,Kama wao wameweza kuuza nchi za ulaya je sisi tumeshindwa vipi kuziuzia nchi za ulaya Kama wao?
Nadhani tumekua tukidanganywa sana kwamba sisi ndio tuna mali nyingi kushinda Ulaya na kwingine, we are wrong na hii ndio inatudumaza akili.

Labda nikupe changamoto hii uiangalie upya, sisi tunajadili kwamba tuna vivutio vikubwa vya utalii duniani, lakini unafahamu nchi ya kwanza duniani kwa 2020 ilikuwa France ambayo ilipokea tourists milioni 89.4? Ikifuatiwa na Spain ambayo ilipokea wageni milioni 83.7 then Thailand ambayo ilipokea wageni 32.6 milioni ikifuatiwa na German etc. (According to Google accross the web).

Data hizo hapo ninataka kuonyesha ni namna gani kuwa na kivutio fulani basi ndio kikupe kiburi usifanye jitihada za makusudi ili kuwavuta watalii.

Naongelea sekta moja ya utalii kama mfano tu ili kuweza kuonyesha namna ambavyo tumekuwa tukipotoshwa sana kwamba tuna mali nyingi mno. Mali bila akili na jitihada za makusudi ni kazi bure.

Hapa lazima kuwa na policy ambazo zitaendana na desturi za wageni watakaokuja, wao kwao wanataka kuwa free, ushoga, kujiuza kwao no free, wanakuja kutembea Ila hawataki restrictions na ndio maana hawaji kwetu. Hapa kwetu watalii hawazidi milioni mbili na tunaendelea kujimwambafai tuna mali.

Madini hatuna kushinda nchi kama America even mafuta, wale hawajaanza kufanya open cast mining wanachimba kawaida tu, wakianda na kupiga kambi kama mwadui au GGM kwa ukubwa wa marekani hatutakuwa na kitu tunaweza kuuza kwao.

Kumbuka aliyekuambia Jana kwamba dhahabu Ina thamani kesho anaweza kukuambia haina thamani,

Namaanisha ukoloni mamboleo hautaosha, ukiisha Ina maana dunia umeisha. Binadamu anaishi kwa survival, mkubwa anamtumia mdogo and vice versa.

Sisi bila kuwa na technology yetu na uvumbuzi wa kwetu usiohusisha wazungu, hatutaweza kushinda a nao. Ndio maana unaweza kuona Russia, North Korea, China wanapambana kila siku kuwa na teknolojia zao kwenye kila sekta.

Sisi tuna wataalamu wa kila aina Ila hatujataka kuwaweka pamoja waumize vichwa kuvumbua vifaa mbalimbali ikiwemo vya afya, anga, kilimo etc.

Leo hii mtu akisoma medicine anaishia kuwa daktari tu, lakini hatuwazi kwamba huyohuyo anaweza kuvumbua dawa za magonjwa fulani, au akagundua sababu za ugonjwa fulani kuwepo.

We need to invest in short term and long term strategies za maendeleo yetu ikihusisha ukuaji wa teknolojia yetu isiyo tegemezi. It's damn expensive lakini heri tuinvest hapo kwanza.
 
Back
Top Bottom