Ningeweza kupandisha uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza katika bidhaa mpya zenye thamani kwa sasa duniani

Ningeweza kupandisha uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza katika bidhaa mpya zenye thamani kwa sasa duniani

ila zungu kawaaibisha sana ngozi nyeupe, sio siri. nilifikiri wote huwa wa maana hadi nilikuwa natamani siku moja tujaribishe urais ngozi nyeupe hizi.
Yule sio ngozi nyeupe aisee, Ile ni mwarabu reject ikawa Mpemba reject ndio umeishia kuwa mwarabu wa ilala.
 
Yule sio ngozi nyeupe aisee, Ile ni mwarabu reject ikawa Mpemba reject ndio umeishia kuwa mwarabu wa ilala.
ukimwangalia ni zaidi ya mwarabu, anaonekana sura ya Waajemi (rostamz, wairan fulani fulani wale waliokuja na mashua bagamoyo kipindi kileee?)
 
ukimwangalia ni zaidi ya mwarabu, anaonekana sura ya Waajemi (rostamz, wairan fulani fulani wale waliokuja na mashua bagamoyo kipindi kileee?)
Mwarabu Koko tu atakuwa kaongezea mkorogo πŸ˜ƒ
 
Upigaji, ufisadi, unyonyaji
Vikikomeshwa hivyo mbona easy hayo mambo mkuu. Na hakuna njia mbadala ya kuvikomesha zaidi ya katiba mpya.

Kwasasa viongozi wanaangalia zaidi nafasi zao na mbaya zaidi hizo nafasi zinalindwa kwa minajili ya kumfurahisha mtu 1 tu.

Sasa kama mtu yeye kutwa kucha anawaza nifanyaje raisi afurahi na sio njia zitazofanya wananchi na raisi wote wawe njia moja si ushubwada huu.

Mawazo haya labda wanayo ila kuyatekeleza ndo inshuu sasa.
 
Tatizo sisi hua kila kitu tunalalmikia serikali, we are lazy! yaaani hata swala la kua mbunifu unasema serikali iweke mazingira sasa sisi tuna faida gan? unazaliwa unasoma bure, unapewa mkopo na kazi unatafutiwa na serikali?
Ni rahisi kuwatupia Wananchi mzigo kwa sababu hata ninyi wenye Mamlaka hamjui cha kufanya.

Hivi unajua ubunifu una gharama kabla kuwa bidhaa ya kuuza? na tena kuna gharama zenye nafasi kubwa ya kupotea bila ubunifu kufikia matarajio.

Ndio yanahitajika mazingira wezeshi na ni Serikali pekee wenye nafasi hiyo, taasisi binafsi zaweza kuwepo lakini kwao ni uchaguzi zaidi ukilinganisha kama kungekuwa na sera nzuri za Serikali kuthamini ubunifu na Wabunifu.

Si rahisi kujua hili kama sio sehemu ya Wabunifu/Wagunduzi.

Mtu/Watu wanapobuni/kugundua kifaa au bidhaa yenye tija na uhitaji basi Mbunifu afikiwe na awezeshwe ili aboreshe kifaa/bidhaa husika...ndivyo wanavyofanya wenzetu hizi bidhaa tunazoziona zinafurika huku.

Ukiangalia Wenzetu huko nje Mtu anayetengenza kifaa uwani kwake bado utastaajabu mashine na malighafi alizonazo ambazo kiukweli Mtanzania wa kawaida ni vigumu kuwa navyo hata kama ana wazo linalofanania hivyohivyo.
 
Yaani ndugu yangu, tatizo ni naloliona ni Tz.kuendelea kuamini na kuweka siasa na mawazo ya siasa za ujamaa/kikomunisti kwenye karibu mambo yote, ambayo ni ya msingi ya kuwezesha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yoyote ktk ulimwengu wa leo, pamoja na kwamba tuna resources nyingi ambazo zingetuwezesha tuwe tumepiga hatua kubwa ya maendeleo.......... bado naona tuna safari ndefu....
Kwani sisi gesi hatuna? Nilicho sema kwenye jibu langu la msingi Ni kwamba hawana resources nyingi Kama sisi,Kama wao wameweza kuuza nchi za ulaya je sisi tumeshindwa vipi kuziuzia nchi za ulaya Kama wao?
I
 
ninachokubaliana na wewe ni hoja ya "leadership", cha pili, ni ukoloni mamboleo, hao wazungu wakitaka kuwekeza kwako wanataka wakutawale na wakufanye wapendavyo. pia, gas kwa mfano, kwa Africa unahitaji mwekezaji mkubwa sana, akifanikiwa kuweka NLG uweke mtandao wa kuiuza hapahapa Africa, kwasababu ulaya na Asia hakuna soko kubwa la gas za Tanzania na Mozambique, nasema hivi kwasababu Russia ina gas nyingi ajabu na wamesambaza mabomba karibia ulaya magharibi yote toka russia yameenda kusambazwa hadi majumbani ulaya yote, kwahiyo ana uhakika. ujerumani kwa mfano hawezi kuacha kutumia gas ya russia ambapo ni karibu kuipata ili aifuate hii ya Tanzania ambako itabidi atumie garama nyingi sana kusafirisha. Iran, na nchi kadhaa za uarabuni wanayo gas nyingi sana ambayo wanamuuzia China na India na tiger countries.

sisi tunachotakiwa kufanya, ni kuhamasisha mwekezaji aweke kiwanda kikubwa cha gas, ikipatikana itakuwa liability kwake yeye kutafuta masoko kulingana na mtaji aliouwekeza kwasababu atataka kurudisha gharama jambo litakalomfanya atafute soko kwa lazima, na soko kubwa lingekuwa la viwanda vinavyotumia gas hapahapa nchini au nchi jirani, viwanda vitakavyokuwa dependant kwenye gas. zaidi ya hapo tunaweza kuuza pia south africa na india kwa bei ya chini kwa ushindani na waarabu ambao wapo karibu kwao (kuisafirisha kwao ni nafuu kuliko kuisafirisha toka huku hivyo lazima tukubali kuliwa kidogo bei ipungue kama incentive), tukifanikiwa pia kuboresha bandari na miundombini mingine kuunganisha na landlocked countries, tutafanya nchi hizo zijenge viwanda tegemezi na hapa kwetu watajenga viwanda tegemezi kwa gas yetu au umeme wetu wa gas, na ndio litakuwa soko l a uhakika. maisha ya watu yakiboreshwa, watakuwa na nyumba bora na matumizi ya mkaa yatakufa kifo cha mende kila nyumba watatumia umeme au gas vyote toka hapahapa jambo litakaloongeza soko sana, matumizi ya magari ya gas pia in the long run. kwa misingi hiyo kidogo nitakubaliana na wewe.
Mkuu umegusia suala la Neo-colonialism moja ya njia ya wazungu kuweka mfumo huo wa ukoloni maomboleo ni kutumia wawekezaji Sasa katika jibu lako la msingi umegusia suala la wawekezaji je,hapa unawalenga wawekezaji gani kutoka nje au wa ndani?
 
Nadhani tumekua tukidanganywa sana kwamba sisi ndio tuna mali nyingi kushinda Ulaya na kwingine, we are wrong na hii ndio inatudumaza akili.

Labda nikupe changamoto hii uiangalie upya, sisi tunajadili kwamba tuna vivutio vikubwa vya utalii duniani, lakini unafahamu nchi ya kwanza duniani kwa 2020 ilikuwa France ambayo ilipokea tourists milioni 89.4? Ikifuatiwa na Spain ambayo ilipokea wageni milioni 83.7 then Thailand ambayo ilipokea wageni 32.6 milioni ikifuatiwa na German etc. (According to Google accross the web).

Data hizo hapo ninataka kuonyesha ni namna gani kuwa na kivutio fulani basi ndio kikupe kiburi usifanye jitihada za makusudi ili kuwavuta watalii.

Naongelea sekta moja ya utalii kama mfano tu ili kuweza kuonyesha namna ambavyo tumekuwa tukipotoshwa sana kwamba tuna mali nyingi mno. Mali bila akili na jitihada za makusudi ni kazi bure.

Hapa lazima kuwa na policy ambazo zitaendana na desturi za wageni watakaokuja, wao kwao wanataka kuwa free, ushoga, kujiuza kwao no free, wanakuja kutembea Ila hawataki restrictions na ndio maana hawaji kwetu. Hapa kwetu watalii hawazidi milioni mbili na tunaendelea kujimwambafai tuna mali.

Madini hatuna kushinda nchi kama America even mafuta, wale hawajaanza kufanya open cast mining wanachimba kawaida tu, wakianda na kupiga kambi kama mwadui au GGM kwa ukubwa wa marekani hatutakuwa na kitu tunaweza kuuza kwao.

Kumbuka aliyekuambia Jana kwamba dhahabu Ina thamani kesho anaweza kukuambia haina thamani,

Namaanisha ukoloni mamboleo hautaosha, ukiisha Ina maana dunia umeisha. Binadamu anaishi kwa survival, mkubwa anamtumia mdogo and vice versa.

Sisi bila kuwa na technology yetu na uvumbuzi wa kwetu usiohusisha wazungu, hatutaweza kushinda a nao. Ndio maana unaweza kuona Russia, North Korea, China wanapambana kila siku kuwa na teknolojia zao kwenye kila sekta.

Sisi tuna wataalamu wa kila aina Ila hatujataka kuwaweka pamoja waumize vichwa kuvumbua vifaa mbalimbali ikiwemo vya afya, anga, kilimo etc.

Leo hii mtu akisoma medicine anaishia kuwa daktari tu, lakini hatuwazi kwamba huyohuyo anaweza kuvumbua dawa za magonjwa fulani, au akagundua sababu za ugonjwa fulani kuwepo.

We need to invest in short term and long term strategies za maendeleo yetu ikihusisha ukuaji wa teknolojia yetu isiyo tegemezi. It's damn expensive lakini heri tuinvest hapo kwanza.
Mkuu kwanza kongole kujenga hoja uku ukichukua sekta ya utalii Kama mfano,Nakubaliana na wewe kusuhu natural resources kwamba Tanzania sio tajiri Kama ambavyo watu wanaaminishwa na Wanasiasa uchwara na wasio na maono kuhusu dunia na namna inavyo kwenda katika mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi,kisiasa, kijamii na teknolojia.

Licha kwamba tunazo natural resources ila nchi imekosa viongozi imara ambao wanaweza kuweka sera imara ya matumizi ya natural resources zilizopo kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika nchi ni aibu nchi kila mwaka kupitisha bakuri kwa nchi wahisani taifa la kutegemea misaada haliwezi piga katika maendeleo kwa sababu ya utegemezi tujifunze basi Kama taifa toka kwa Botswana mbona Wana proper utilization of natural resources licha ni kidogo ukilinganisha na Tanzania na wamepiga hatua nzuri katika maendeleo.
 
Tatizo sisi hua kila kitu tunalalmikia serikali, we are lazy! yaaani hata swala la kua mbunifu unasema serikali iweke mazingira sasa sisi tuna faida gan? unazaliwa unasoma bure, unapewa mkopo na kazi unatafutiwa na serikali?
HiVi unadhani hakuna bunifu nzuri kwenye hii nchii .... Kunabunifu za kipekee na kama zitatiliwa mkazo basi hii nchi ingekuwa mbali Sana tatizo siasa kila mahali pia secta binafsi azipewi kipaombele hii nchi kila kitu ni serikali serikali...hii inasababisha mambo mengi na bunifu nyingi nzuri kukwama.
 
Yaani ndugu yangu, tatizo ni naloliona ni Tz.kuendelea kuamini na kuweka siasa na mawazo ya siasa za ujamaa/kikomunisti kwenye karibu mambo yote, ambayo ni ya msingi ya kuwezesha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yoyote ktk ulimwengu wa leo, pamoja na kwamba tuna resources nyingi ambazo zingetuwezesha tuwe tumepiga hatua kubwa ya maendeleo.......... bado naona tuna safari ndefu....

I
Mkuu Mimi naona ujamaa hauna madhara makubwa Sana Kama kutowajibika, kutowajibika ndo chanzo kikubwa Cha matatizo katika nchi mfano Kuna muda bunge lilikuwa katika mjadala muhimu wa bajeti ya nchi ila wabunge Kuna muda walikuwa wanaacha kujadili bajeti na kuanza kumjadili Mbowe Mpaka ilifika muda Rais kuwaambia waache kudemka wajadili mambo ya msingi je suala hili la wabunge lilichangiwa na ujamaa?
 
Tatizo sisi hua kila kitu tunalalmikia serikali, we are lazy! yaaani hata swala la kua mbunifu unasema serikali iweke mazingira sasa sisi tuna faida gan? unazaliwa unasoma bure, unapewa mkopo na kazi unatafutiwa na serikali?
Serikal ndo inapanga kila kitu bila serikal vitu alivyoo vitaja hapoo juu kutoboa ni ndoto
 
Mkuu Mimi naona ujamaa hauna madhara makubwa Sana Kama kutowajibika, kutowajibika ndo chanzo kikubwa Cha matatizo katika nchi mfano Kuna muda bunge lilikuwa katika mjadala muhimu wa bajeti ya nchi ila wabunge Kuna muda walikuwa wanaacha kujadili bajeti na kuanza kumjadili Mbowe Mpaka ilifika muda Rais kuwaambia waache kudemka wajadili mambo ya msingi je suala hili la wabunge lilichangiwa na ujamaa?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Serikal ndo inapanga kila kitu bila serikal vitu alivyoo vitaja hapoo juu kutoboa ni ndoto
Ndio maana nimesema ningeweza, nimetumia nafsi ya kwanza umoja. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
 
Back
Top Bottom