Kuna kitu ambacho watu hamkifahamu kuhusu AY ndomana mtoa mada kathubutu kumfananisha na Diamond kitu ambacho si sahihi sana, yaan ni kama umfananishe Messi (AY) na Mrisho ngasa ( Domo)
Fahamu kuwa alipo Domo kwasasa yeye AY alishapapita miaka mi 5 iliyopita na hajashuka mpaka sasa, yupo next level, diamond bado yupo kwenye kupata more recognition internationally ndomana unamwona kila jambo analofanya lazima ahakikishe media na social network zooote zimepambwa na picha na habari zake,kitu ambacho ni kizuri kwakuwa anazidi kujitangaza zaidi.
Style ya AY kipindi anahustle ilikuwa tofauti na Diamond, AY kamwe hakujitangaza tangaza, watu walistukia tu ma collabo na wasanii wengine wa Africa,mara tuzo za Channel O kachukua, mara collabo na Sean kingstone ikawa hivyo. Japo hajasema ila jiandaeni kolabo inayofuata ni yeye na J-Z (jokes n I wish to be true)
Mondi bin Laden a.k.a Domo yeye kila ananchokifanya lazima atupie kwenye mitandao, anamjengea swimming pool mama ake katupia picha, anashuka kwenye ndege katupia picha, katoka kuoga katupia picha, anakula katupia picha, yaan bado kutupia picha akiwa anagegeda tu. Akifanya video yoyote atasema gharama alizotumia, matamasha afanyayo atasema kapata sh ngapi, hata account atasema haipungui kiasi kadhaa…ila amini msiamini laiti AY angesema mafanikio yake kwenye media basi wazee wa Escrow wangejiona kumbe hata wao wana mpinzani kwenye maswala ya chapaa.
Kufananisha nyimbo za AY na Diamond kwasasa ni kukosea,eti ooh Domo ana viewer wengi kwenye youtube kuliko AY ni kweli kabisaa ila sio kipimo halisi cha kufananisha mafanikio, Domo amefocus zaidi kwenye nyimbo zake na video production bora zitakazomweka pazuri kimataifa zaidi, wakati AY amefocus zaidi kwenye u manager wa wasanii, jamaa ana kampun yake ya management na ana wa manage wasanii wakubwa tu afrika kwasasa, nani anajua kwamba P square wapo chini ya AY?
Nani anajua kuwa Nameless, Wahuu, Bracket na wengineo wote wapo chini ya management ya AY?? Jamaa ana vitega uchumi kibaooo south Africa, kwa fununu tu japo sina uhakika naskia ana bongee la jumba South jumba ambalo wasanii wetu wakienda South ndo uwa wanafikia kwa jamaa, miradi aliyonayo hapa Tz akiiweka hadharani yote lazima mtasema tu huyu jamaa ni muuza sembe.
Namkubali sana Domo tena sana kwakuwa anajituma na ameleta hamasa kubwa kwa wasanii wengine kuthubutu kufanya mziki wao ki international zaidi, mwangalie Linnah, Rich mavoko, chege na temba hata Ali kiba mwenyewe amelazimika kutoa internaonal video just because of Diamond, nilitamani sana Diamond angekuwa chini ya management ya AY naamini angefika mbaaaaali zaidi, hii timu vitambi aliokuwa nao sasa wakina Babu tale na Fellah mmmh,nina mashaka nayo.
KIla la kheri wasanii wa Tz kila la kheri mziki wa bongo fleva.