Nini amekosa AY?

Nini amekosa AY?

Hahaha nimecheka sana,yani kuna vitu vingine watu wanaviongea unabaki kucheka tu....tunaambiwa ata kisiwa cha mbudya ni chake eti !

Hivi mtu anaweza kumiliki kisiwa chote kama mafia na nungwi?

ninachojua ana kipande cha hiyo mbudya ndo anapigia business hapo,ndo pengine anaitwa rais wa mbudya kwa sababu hiyo?
 
Habadiliki, yaan ukiskiliza nyimbo zake zile zile, mf FA yeye anabadilika kidogo sana ila anajitahidi kutunga maneno ya kuguza, yaan maneno ya kwenye nyimbo zake ni matam, AY anatakiwa aache ile rap yake,
 
Kuna nchi za ulaya ukibahatika kuishi unaonekana utakuwa na wakati mgumu sana wewe bibie maana utakuta kuna show kubwa inafanyika kwa kiingilio kikubwa ukiingia humo unakuta mwanamuziki mwenyewe kawekewa kiti kabisa cha kukaa jukwaani hakuna mauno hapo na utashangaa show hiyo imevunja rekodi.

Achana na watu weupe kabisa hawa ndio wanajuwa muziki ni nini, mimi ukija nyumbani kwangu jumapili bila hata ya mimi sijakwambia lolote utapata ishara tu kama uko na mtu tofauti utakaposikia tu playlist yangu au afadhari naweza kuweka choice fm wale tunaongea lugha moja.

Hivoooo eeeeh??? Basi sawa....
 
AY ni msanii mwenye mafanikio makubwa kuliko yoyote ukitoa jide ila hapendi kujisifia ni mkimya wala hapendi skendo.

Tatizo lenu mtu anayejionyesha ndio mnajua ana mafanikio .Mimi namfahanu sana AY ana mafanikio makubwa sana na show nyingi anapiga nje mfano show anazopiga Kenya na Uganda ata zinazidi Tz

Uwa apendi kujifagilia na kujionyesha kama wengine ni mkimya pia mfanyabiashara anewekeza Tz ata kenya pia

Mafanikio in busness wise ukiacha mziki YES huyu jamaa anainvest aisee.. ila kimuziki sasa ndo kapotea
 
ay , banana, ali kiba ni wasanii niliowakubali sana ila wameniangusha sana.

hawana ubunifu kabisaaa

watabaki hivyo hvy hadi kumezwa na historia!

Banana anajifunza kurap na mwalimu wake ni mwanaFa

kuhusu Ally kiba na Ay nakuombea uishi maisha marefu zaidi ili ushuhudie kufutika kwao,kwani hawatofutika miaka ya karibuni hapa
 
mkuu ungesoma vizuri sentensi yangu ungenielewa,kuna neno fununu nimeliweka hapo mwweh!!
suala la kupanga kawaida sana wala sio kipimo cha maendeleo ya mtu, wasanii wangapi wanapanga bhana? bongo tu ndo nchi unayoweza kumiliki ardhi yako na kuifanyia utakavyo,nenda kwa wengine ndo utaona mziki..hata Christ brown, Jason darule, Balotelli, Di Maria wote hao wamepanga, namimi pia nimepanga vilevile japo Diamond na Ay hawanifikii kimkwanja.

hahaha una sh. ngapi bank?
 
Ay anafanya muziki ili kumpa connection ya michongo mingine lakini muziki haumlipi kivile kama unavyomlipa Diamond au Ommy Dimpoz nk

Diamond anategemea muziki kwa asilimia 100 kumuingizia kipato na amefanikiwa sana kwa hilo kwa kupata show ndani na nje na kuingia mikataba minono na makampuni mbali mbali tofauti ma Ay

Kama nilivyosema awali tatizo la Ay ni aina ya muziki anafanya. Na mafanikio yapo kwa njia nyingi ama direct au indirect
 
Habadiliki, yaan ukiskiliza nyimbo zake zile zile, mf FA yeye anabadilika kidogo sana ila anajitahidi kutunga maneno ya kuguza, yaan maneno ya kwenye nyimbo zake ni matam, AY anatakiwa aache ile rap yake,

Mkuu hata akibadili mashairi unadhani atafikia vocal ya plutnumz...thubutu
Dogo anajua kucheza na sauti bhana hayo mengine tumuachie yeye na akina Zari wake.
 
Ungekuwa unapoteza mda hapa JF?:A S wink::A S wink:

nani kakwambia napoteza muda wakati hujui hata mishe zangu..kama narefresh mind tu utajuaje? mungu mwenyewe aliumba dunia siku sita, siku ya saba akapumzika akawa anakula bata, we vipi weweeeee!!!
 
Unajua kuna jambo watu hawajalijua kuhusu diamond. Ikulu ilikuwa inamsapoti sana alikiba lakini alikiba aliridhika mapema. Sasa hivi ikulu inamsapoti diamond ki muziki. Diamond anapiga kelele nyingi, asubiri ikulu inayokuja mwaka huu kama atapewa support ki hiyo. Kila jambo na wakati wake awe makini tu. AY ana fanya la maana kufanya mambo yake personal kwa sababu anajielewa.
 
kwahy joh makini ndio hawatakiwi kusema, ila wema daimondo kiba wao ndio wasemwe tu? ajabu
 
Unajua kuna jambo watu hawajalijua kuhusu diamond. Ikulu ilikuwa inamsapoti sana alikiba lakini alikiba aliridhika mapema. Sasa hivi ikulu inamsapoti diamond ki muziki. Diamond anapiga kelele nyingi, asubiri ikulu inayokuja mwaka huu kama atapewa support ki hiyo. Kila jambo na wakati wake awe makini tu. AY ana fanya la maana kufanya mambo yake personal kwa sababu anajielewa.

umeongea ujinga wa mwaka, eti ikulu kumsapoti daimondo. mara ikulu ilimsapoti kiba.

hv watu huwa mnasoma coments zenu kbl ya kupost ?!
 
umeongea ujinga wa mwaka, eti ikulu kumsapoti daimondo. mara ikulu ilimsapoti kiba.

hv watu huwa mnasoma coments zenu kbl ya kupost ?!

We bado mdogo sana. Mjini mgeni mno na hujui chochote, tena mshamba mara mia. Huwezi kujua wala kuelewa nilichopost. Mjini ndiyo wananielewa coz data zipo
 
Kuhusu muziki wa AY inawezekana level zake ni za juu sana hadi sisi hatuuelewi...anaweza akawa international levels lakin national level hayupo kabisa

AY abadili kidogo muziki wake aweke mambo ya kitaa kidogo..hapa wanaojua muziki watanielewa..watu kama WEUSI wana connect na kitaa..SHAA ameconnect na kitaa na mwimbo wake sugua gaga..sasa jamaa amebaki malevo ya masaki..nini na nini..hao watu wa masaki sio wengi..AY kama unataka kufanya vizuri zaidi connect na kitaa gonga ngoma zitazobamba muuza miwa..mwendesha bodaboda..hao ndio walio wengi..
 
Dah kweli jamaa hana nyuta tuu. Ngoma zake nyingi ni za kimataifa.
 
We bado mdogo sana. Mjini mgeni mno na hujui chochote, tena mshamba mara mia. Huwezi kujua wala kuelewa nilichopost. Mjini ndiyo wananielewa coz data zipo

Wanaoelewa ishu za mjini kama hzi ni wachache! mfuate pm ukamweleweshe maana jamaa naskia yupo mpakani na msumbiji ishu za town atazijulia wapi!
 
Back
Top Bottom