Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa yuko kwenye harakati kitambo kwenye hii game. AY ndo alianza kuwafumbua macho wasanii kuhusu umuhimu wa kufanya collabo na wasanii wa nje ya nchi.
Pia ndo alikuwa msanii wa kwanza bongo kuwa siriaz kuinvest katika video (ki-international zaid) hata Diamond amewahi kulisema hilo kwenye intavyuu zake/kwenye social networks kwamba jamaa ndo kamuinspire.
Sasa nashindwa kuelewa why anashindwa kuwa succesful kivile japo anajituma sana, yaani naona kama ka-stack palepale, nilitamani naye niwe namsikia kwenye mambo makubwa makubwa kama 'bwa mdogo' Diamond ili walau tuwe na wawakilishi wengi nje.
Mi nazan kama vile watanzania hatumpi sapoti ya kutosha kuanzia media hadi mashabiki, maana eg. huu wimbo mpya alioutoa ft Sean Kingston ni mzuri but sioni ukizungumziwa kihivo. So wadau mnahisi AY anafeli wapi?
AY ni msanii mwenye mafanikio makubwa kuliko yoyote ukitoa jide ila hapendi kujisifia ni mkimya wala hapendi skendo.
Tatizo lenu mtu anayejionyesha ndio mnajua ana mafanikio .Mimi namfahanu sana AY ana mafanikio makubwa sana na show nyingi anapiga nje mfano show anazopiga Kenya na Uganda ata zinazidi Tz
Uwa apendi kujifagilia na kujionyesha kama wengine ni mkimya pia mfanyabiashara anewekeza Tz ata kenya pia
Nani kakwambia AY ka stack? umetumia vigezo vipi labda ku conclude kua Diamond ana mafanikio makubwa kuliko AY?
Au coz hajatembea na msululu wa wasanii wa bongo muvi ndo unasema hana mafanikio ?
tatizo nyota!!
Abonyeze reli (#)nyota (*)itatoka...
Anataka AY ajiite sukari ya warembo....halafu mwanaume na akili zako unamshabikia diamond wakati mpaka mama yako, mkeo, dada yako yy anatamba ni sukari yao
AY hana maskendo ya kulala dada zetu na kuwaacha na kupeleka picha kwa shigongo azitoe magazetini!
akili za kitanzania ndio kama hizi, hajui lolote, hajafanya research, hajauliza ameishatoa conclusion
hana skendo za kulalabna dada zetu??? hivyo analala na dada zake au?
embu nieleweshe Hard driveOyoo paula ww mtu akisema dada zetu...unakuwa haujamuelewa definetly
Nani kakwambia AY ka stack? umetumia vigezo vipi labda ku conclude kua Diamond ana mafanikio makubwa kuliko AY?
Au coz hajatembea na msululu wa wasanii wa bongo muvi ndo unasema hana mafanikio ?
sio kosa lako, uelewa wako ni mdogo sana, ndio maana matusi ndio ngao yako go back to ya comment, uliosema ay hana skendo za kulala na dada zetu, ndio nikakuuliza kama halalagi na dada zetu hulala na nani??? dada zake???? sasa nakushangaa unaviporomosha mitusi.
sisi hiphop headz tunatambua kazi yake ,wakati anapokea tuzo za channel o diamond alikuwa tandale anakula ngisi na pweza wa kudonoa na toothpick,michachandu kibao na michumvi
am so sorry kusema hujanielewa.kumbe mwoga, is it natural someone to sleep with his own sister? what were you thinking askin such stupid question?
I though ungekuja mbogo nikufundishe kujenga hoja, so swali lako ni hoja?? Div 5 bana
I always say, mnaoweza kutumia majina yenu, be smarter bana
hata mimi mwenyewe nashangaa jamaa kaanza toboa na kupiga collabo za nje toka kitambo nadhani ndiye kawapa direction wasanii wengi lakini mpaka leo huwezi sema mziki wake umekua sana.
Mfano mdogo hii track yake mpya ya Touch me, japo kuwa kafanya na msanii mkubwa Sean Kingstone lakini hebu angalia views zake youtube mpaka sasa ni 102,902 tu. youtube ni sehemu moja ya kupima fan base ya msanii, sasa mnaodai jamaa anafanya vizuri sana internationally hao fans zake mbona hawaonekani kuangalia video zake maana almost video zake zote zina viewers wachache.
Mnasema anapiga shows nyingi nje, kama ni kweli basi ni shows ndogo ndgo maana hata vyombo vyetu vya habari uwa havireport walau kutupia vipicha tuone, mbona wengine wakifanya shows nje utaskia kwenye vi blogs na mbona hata yeye mfano alipoenda white house na kipindi kile kufanya show big brother tuliona hizo habari sasa iweje shows nyingi mnazodai anapiga zisiandikwe?
Mziki ni biashara, na ili ufanikiwe kimziki lazima ujitangaze sana, ukiwa na show lazima ufanye watu wajue. Interaction kati ya msanii na fans wake ni muhimu sana ndiyo maana hata wasanii wakubwa wa nje utakuta wako kwenye social network wakitoa habari zao za shows, na mambo yao mengi kwa fans zao. Ile sio show off bali ni kuleta mawasiliano baina ya msanii na fans wake.
Mziki upimwa na tunzo Ay sijui ana tunzo ngapi hapa Tz, tunzo za nje alikuwa anachukua kipindi cha nyuma lakini naona baada ya wasanii wengine hapa tz kuanza nao kwenda international wamemnyanganya nafasi hata za kuwa nominated tu.
All in all Ay namkubari kwa life style yake na ni mtu makini na hustler mwenye kujua kutafta pesa hata nje ya mziki.
am so sorry kusema hujanielewa.