Ni kweli, watoto wa siku hizi wanapenda sana njia za mkato za kusoma kwenye internete na kuchukulia kuwa huo ndio ukweli.
Nimefanya utafiti wa kutosha na sasa ninaweza kuwaambia wote
mageuzi1992,
Dingswayo,
Richard,
King Kong III,
mnyinda na wengineo mliochangia post hii kwa kadri ya uwezo wenu kuwa neno "Tanganyika" halina uhusiano wowote maneno ya "Tanga" na "Nyika" kama inavyoripotiwa Wikipedia na kweingineko, nitajaribu kwenda kusahihisha huko Wikipedia nikiweza, kwa vile mtu yoyote anaweza kufanya hivyo.
Ni kweli kuwa jina la nchi
Tanganyika limetokana na kuwepo kwa ziwa
Tanganyika, lakini asili ya neno Tanganyika lenyewe ndilo lililokuwa na utata. Kwa vile sina muda wa kutosha kuandika historia yote kwa kirefu, nitadondosha kidogo tu kuwa jina "
Tanganyika" limetokana na neno "
Changanyika." Nitatoa maelezo kwa kina huko mbeleni, ila lina sababu kubwa mbili ni: (1) kuchanganyika kwa waarabu na wamanyema pale ujiji (2) kuchangayika kwa maji ya maziwa ambayo yalikuwa hayajulikani ya ukerewe na ya Nyanja kwenye ziwa hilo la ujiji.
Kwa vile maelezo yake ni marefu yanayohitaji supporting documents na graphics, nitayatoa kwa kina nikipata nafasi nzuri ya kufanya hivyo. Nikiahidi hapa JF mara nyingi huwa ninatimiza hasa iwapo nimeshakamilisha utafiti wangu. Kwa vile sasa hivi nimeshakamilisha utafiti huo, nitaleta ripoti kamili siku chache zijazo. Nitawaacha na ramani hii inayoonyesha ziwa hilo likiitwa jina la kijerumani.