Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,120
Kwa hiyo comrade unatuambia kwamba jina Tanga lilikuwepo kabla ya jina Tanganyika? Na kama ni hivyo sasa mkoa wa Tanga ulikua uko ndani ya nchi inayoitwaje?
Kwa hiyo comrade unatuambia kwamba jina Tanga lilikuwepo kabla ya jina Tanganyika? Na kama ni hivyo sasa mkoa wa Tanga ulikua uko ndani ya nchi inayoitwaje?
Kumekuwepo na maswali mengi juu ya jina la tanganyika na baadaye tanzania
sisi twajua yakwamba jina tanzania lilitokana na munganiko wa nchi mbili tanganyika na zanzibar,
sasa swali nikwamba Tanganyika ilitokana na nini?
Na nini maana ya Tanganyika?
Na ninani aliyependekeza jina Tanganyika?
Maswali mengine ya ajabu kweli. Vipi ndugu yangu, je kwenye post yangu uliyokwoti niliandika nini? Nilisema kuwa nitalifanyia utafiti kujua lilianza lini lakini ni la siku nyingi kwa vile record zilizoko zinaonyesha kuwa hata mwaka 1859 lilikuwepo ingawa lilianza kutumika kama nchi mwaka 1922 tu.kwahiyo hili ziwa Tanganyika lilikuwa likiitwa hivyo toka mwaka gani?
Maana hata jina la ziwa limetokana na watu kulipa jina,
Tanganyika ni eneo lililohusisha mkoa wa Kigoma, Tabora na sehemu za Rukwa. Hii habari niliipata huko Kigoma. Mzee mmoja anasema eneo lingine la Tanganyika ya leo liliitwa Azania. Hivyo Tz Bara =Tanganyika +Azania.
Researchers watujuze.
Maswali mengine ya ajabu kweli. Vipi ndugu yangu, je kwenye post yangu uliyokwoti niliandika nini? Nilisema kuwa nitalifanyia utafiti kujua lilianza lini lakini ni la siku nyingi kwa vile record zilizoko zinaonyesha kuwa hata mwaka 1859 lilikuwepo ingawa lilianza kutumika kama nchi mwaka 1922 tu.
Usihangaike soma hapa :Tanganyika Territory - Wikipedia, the free encyclopedia
Kama utafiti wako ni kusoma Wikipedia basi huna kiwango cha kujibizana na mimi katika mambo ya historia. Wanaojuia historia hawatumii Wikipedia kama reference. Hata hapo juu nimekuwekea reference nzuri original inayoonyesha kuwa neno Tanganyika lilikuwepo mwaka 1859, karibu miaka sabini kabla ya Tanganyika Territory, nikakuahidi kufanya research zaidi ili kutafuta reference za nyuma zaidi kuona neno hilo lilianzia wapi, halafu wewe unakazania reference nyepesi kama Wikipedia. Iwapo Wikipedia ndilo lingekuwa jibu basi hata kusingekuwa na haja ya kujadili mada hii.
Kama uko siriasi kujua mambo, usiwe mtu wa pupa; jaribu kuwa positive na kuyaangalia kwa mapana yake muda wote.
Wakati facebook inapotosha watoto wa primary na secondary kwa kuwapotezea muda, Wikipedia inawapotosha undergraduates na graduates wanaopenda shortcut ya madesa!
Kama kuna kitu siipendi kwenye mitandao ni Wikipedia!
Ni kweli, watoto wa siku hizi wanapenda sana njia za mkato za kusoma kwenye internete na kuchukulia kuwa huo ndio ukweli.
Nimefanya utafiti wa kutosha na sasa ninaweza kuwaambia wote mageuzi1992, Dingswayo, Richard, King Kong III, mnyinda na wengineo mliochangia post hii kwa kadri ya uwezo wenu kuwa neno "Tanganyika" halina uhusiano wowote maneno ya "Tanga" na "Nyika" kama inavyoripotiwa Wikipedia na kweingineko, nitajaribu kwenda kusahihisha huko Wikipedia nikiweza, kwa vile mtu yoyote anaweza kufanya hivyo.
Ni kweli kuwa jina la nchi Tanganyika limetokana na kuwepo kwa ziwa Tanganyika, lakini asili ya neno Tanganyika lenyewe ndilo lililokuwa na utata. Kwa vile sina muda wa kutosha kuandika historia yote kwa kirefu, nitadondosha kidogo tu kuwa jina "Tanganyika" limetokana na neno "Changanyika." Nitatoa maelezo kwa kina huko mbeleni, ila lina sababu kubwa mbili ni: (1) kuchanganyika kwa waarabu na wamanyema pale ujiji (2) kuchangayika kwa maji ya maziwa ambayo yalikuwa hayajulikani ya ukerewe na ya Nyanja kwenye ziwa hilo la ujiji.
Kwa vile maelezo yake ni marefu yanayohitaji supporting documents na graphics, nitayatoa kwa kina nikipata nafasi nzuri ya kufanya hivyo. Nikiahidi hapa JF mara nyingi huwa ninatimiza hasa iwapo nimeshakamilisha utafiti wangu. Kwa vile sasa hivi nimeshakamilisha utafiti huo, nitaleta ripoti kamili siku chache zijazo. Nitawaacha na ramani hii inayoonyesha ziwa hilo likiitwa jina la kijerumani.
Neno Tanganyika linamaanisha 'nyika ya Tanga'. Watembezi 'explorers' wa kizungu waliokuja wakti wa zamani, walishukia Tanga, na wakaingia bara kutafuta chanzo cha mto Nile. Maeneo yale waliyotembea wakayaita 'nyika ya Tanga' au Tanganyika. Soma zaidi hapa:
Tanganyika Territory - Wikipedia, the free encyclopedia
Mkuu Richard, record yako siyo sahihi kabisa.
Neno Tanganyika siyo muungano wa maneno mawili ya Tanga na Nyika, ni neno lililokuwa linatumiwa na watu wa ujiji kwa maana ya kuchanganyika. Wakati huo Ziwa lile lilikuwa likijulikana kama Ziwa la Ujiji. Mtu alieanza kuliita ziwa lile kuwa ni Ziwa Zanganyika ni Mr. Cooley katika article aliyoandika mwaka 1845 (zaidi ya miaka 10 kabla ya Burtone na Speke hawajatembelea eneo hilo). Mr Cooley aliandika article yake iliyoitwa "Memoir on the Geography of K'yassi" kwenye toleo la 15 la jarida la Journal of the Royal Geographical Society, mwaka 1845. Mr Cooley alikuwa amemuhoji mtu mmoja wa Lamu aliyejulikana kama Khamis Bin Tani alijifanya kuwa anajua maziwa yoye hayo. Wakati huo eno la pwani lilikuwa likijulikana kama Zanguebar. Cooley aliandika
The Mucarang'a, or people of Monomoezi; still retain the com-
mercial habits for which they were formerly so much noted.
They descend annually in large numbers to Zanzibar. The
journey to the coast and back again takes 9 or 10 months, includ-
ing the delay of awaiting the proper season for returning. It
would appear that they start on the journey down in March or
April, probably at the end of the heavy rains, and return in Sep-
tember. They are decently clothed in cotton of their own manu-
facture ; but the most obvious mark of their superiority above
other nations of Eastern Africa is, that they employ beasts of
burden, for their merchandise is conveyed to the coast laden on"
asses of a fine breed. From a town or tribe called Zanganyika;
on the opposite or south-western side of the lake (which near Oha
is 3 days voyage across), they obtain copper, ivory, and oil of a
red colour. They are said to have formerly used for money
''little balls, like glass, of a reddish colour."* There is no
difficulty in guessing what is here meant to be described. The
most famous mountain of Eastern Africa is Kirimanjara, which
we suppose, from a number of circumstances, to be the highest
ridg« crossed by the road to Monomoezi. The top of this moun-
tain is strewed all over with red carnelian, the rounded pebbles
of which were doubtless the money referred to. The importation
of beads has probably caused the disappearance of the carnelian
currency.
View attachment 97875
Kwenye mkutano wa Royal Geographical Society uliokutana December 15, mwaka 1856 (miaka mitatu kabla Speke na Burton hawajafika kweny ziwa lile,) Dr Livingstone naye alizungumza hivi:
DR. LIVINGSTON: When I was on my way from Linyanti to Loando, I met
with an Arab, who was going to return home towards Zanzibar across the
southern end of the lake " Tanganyenko," and who informed me that in the
country of the Banyassa (Wun' Yassa?) there is an elevated ridge which trends
towards the N.N.E. The lake lies west of it, and in the northern part is
called Kalague. They cross the southern end of it, and when crossing they
punt the canoe the whole way, and go from one island to another, spending
three days in crossing. It seems, from the description I got from him, to be a
collection of shallow water, exactly like Lake Ngami, which is not deep either,
as I have seen men punting their canoes over it. It seems to be the rem-
nant of a large lake, which existed in this part, before the fissure was made to
allow the Zambesi to flow out. That part of the country is described by
many natives as being exceedingly marshy. The Makoloko went up to the
Shuia Lake and found all the country exceedingly marshy, and a large lake
seems to be actually in existence, or a large marsh with islands in it. But it
can scarcely be so extensive as has been represented, as in that case I must
have crossed part of it or heard more of it.
Account ya kwanza kuhus jina Tanganyika iliandiwaka na Captain Richard Francis Burton mwaka 1860 katika kitabu chake maarufu cha "Lake Regions of Central Africa" na hasa kwenye ukurasa wa 367, kama nilivyouambatanisha hapa.
View attachment 97874
Record zote hizo hizo za kihistoria nilizotaja hapo ninazo ila kama nilivyosema kwenye post yangu ya awali, naomba nipate muda wa kuzipanga vizuri, kwa vile siwezi kuzimabatanisha hapa kutokana na ukubwa wake.