Kilimanjaro ni neno maarufu sana miongoni mwa wakaazi wa Afrika na duniani kote. Umaarufu wa jina hili umetokana na Mlima mrefu uliosimama pekee unaoitwa Mlima Kilimanjaro, upatikanao kaskazini mwa Tanzania.
Asili ya neno hili ni makosa ya kisarufi yaliyofanywa na wageni kutoka ng'ambo ambao waliwasili eneo hilo karne ya 18 na kuwakuta wazawa 'natives' wakiishi maeneo hayo kuuzunguka mlima huo. Inasemekana kuwa wazawa wa eneo hilo yaani wachaga waliuita mlima huo 'kilimakyaro', wakimaanisha kilimakirefu.
Lakini kutokana na kushindwa kutamka hilo neno 'wazungu' walitamka kwa namna yao na kuuita huo mlima Kilimanjaro, ambalo ndilo neno litumikalo hadi hivi sasa kutokana na kwamba wao waliweza kuhifadhi hilo jina kwa njia ya maandishi na kulitangaza kote duniani. Mungu akijaalia kesho tutaangalia historia ya neno Olduvai.