Nini asili ya neno Kilimanjaro

Nini asili ya neno Kilimanjaro

kodo

Member
Joined
May 11, 2011
Posts
14
Reaction score
4
Kilimanjaro ni neno maarufu sana miongoni mwa wakaazi wa Afrika na duniani kote. Umaarufu wa jina hili umetokana na Mlima mrefu uliosimama pekee unaoitwa Mlima Kilimanjaro, upatikanao kaskazini mwa Tanzania.

Asili ya neno hili ni makosa ya kisarufi yaliyofanywa na wageni kutoka ng'ambo ambao waliwasili eneo hilo karne ya 18 na kuwakuta wazawa 'natives' wakiishi maeneo hayo kuuzunguka mlima huo. Inasemekana kuwa wazawa wa eneo hilo yaani wachaga waliuita mlima huo 'kilimakyaro', wakimaanisha kilimakirefu.

Lakini kutokana na kushindwa kutamka hilo neno 'wazungu' walitamka kwa namna yao na kuuita huo mlima Kilimanjaro, ambalo ndilo neno litumikalo hadi hivi sasa kutokana na kwamba wao waliweza kuhifadhi hilo jina kwa njia ya maandishi na kulitangaza kote duniani. Mungu akijaalia kesho tutaangalia historia ya neno Olduvai.
 
Inawezekana pia kutokana na kwamba babu zetu waliitumia milima kama sehemu za ibada pia lakini kwa maana ya Kilimanjaro, ndiyo hiyo iliyoelezwa hapo juu
 
Kilimanjaro ni neno maarufu sana miongoni mwa wakaazi wa Afrika na duniani kote. Umaarufu wa jina hili umetokana na Mlima mrefu uliosimama pekee unaoitwa Mlima Kilimanjaro, upatikanao kaskazini mwa Tanzania. Asili ya neno hili ni makosa ya kisarufi yaliyofanywa na wageni kutoka ng'ambo ambao waliwasili eneo hilo karne ya 18 na kuwakuta wazawa 'natives' wakiishi maeneo hayo kuuzunguka mlima huo. Inasemekana kuwa wazawa wa eneo hilo yaani wachaga waliuita mlima huo 'kilimakyaro', wakimaanisha kilimakirefu. Lakini kutokana na kushindwa kutamka hilo neno 'wazungu' walitamka kwa namna yao na kuuita huo mlima Kilimanjaro, ambalo ndilo neno litumikalo hadi hivi sasa kutokana na kwamba wao waliweza kuhifadhi hilo jina kwa njia ya maandishi na kulitangaza kote duniani. Mungu akijaalia kesho tutaangalia historia ya neno Olduvai.
Sasa kama ni hivyo kwa nini lisitumike jina la asili (Kilimakyaro) kuliko kuendelea kutumia jina lenye historia ya makosa ya kisarufi kutoka kwa wageni?
 
Aother school of thought
1. Wachagga kwa asili kabla ya kuletwa dini za kigini walikuwa wanauabudu mlima huu. Wakiamka asubuhi lazima wauangalie na kushukuru kwa kuamka salama. Walikuwa wanauita mlima wa Mungu ambao kiasili walikuwa wanaamini Mungu yupo mawinguni(RUWA) hivyo wazungu walipo kuja walikuta wanauita ( KILIMA= MLIMA...KYA= WA....RUWA= MUNGU) KILIMA KYA RUWA = MLIMA WA MUNGU....WAO WAKISHINDWA KUTAMKA WAKAITA KILIMANJARO
 
Of course tuna kila sababu ya kuwafundisha na kurithisha kizazi kijacho asili ya kwetu kuliko kwa wazungu, ziwa Victoria tunaambiwa mzungu ndo kagundua wakati lipo tokea mwanzo,he mzungu na msukuma wa mwanza nan wa kwanza kufika Mwanza?

Historia ya machifu wetu hawajulikan lkn historia ya akina Richard Turnbull, John Speke, Livingstone etc zimekuwa na umaarufu zaidi.Tuna haja ya vizazi vyetu kuwajua akina Chief Kingalu,Mkwawa, Mutesa,Mangisina na wengineo kuliko kuwajua zaidi wazungu ambao kwetu sio wa muhimu.

Tuna safari ndefu ya kurithisha kizazi chetu...
cc: mahonda
 
Aother school of thought
1. Wachagga kwa asili kabla ya kuletwa dini za kigini walikuwa wanauabudu mlima huu. Wakiamka asubuhi lazima wauangalie na kushukuru kwa kuamka salama. Walikuwa wanauita mlima wa Mungu ambao kiasili walikuwa wanaamini Mungu yupo mawinguni(RUWA) hivyo wazungu walipo kuja walikuta wanauita ( KILIMA= MLIMA...KYA= WA....RUWA= MUNGU) KILIMA KYA RUWA = MLIMA WA MUNGU....WAO WAKISHINDWA KUTAMKA WAKAITA KILIMANJARO
Kwann tutumie jina lenye makosa?
 
sio makosa Bali ni makusudi tu ili iwe wao ndio wametoa jina
Mabeberu ni Wajanja sana
 
Back
Top Bottom