GE2025 Nini CCM kinawashinda kuwa kama wenzenu CPV ya Vietnam na CPC ya China ?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
6,406
Reaction score
12,736
Mi mi sijali CCM mmeanza kuitawala Tanzania kwa muda gani na mtaitawala Tanzania kwa muda gani hata mkiitawala Tanzania kwa miaka 100 kwangu sawa tu.

Shida yangu kwa nini msiwe kama wenzenu CPV ya Vietnam angalia mahali Vietnam walipoitoa na kuamua kufanya Doi Moi leo Vietnam ipo wapi na inaelekea wapi ? Kidunia inazungumzwaje ukifananisha na Tanzania yenu mnayoiongoza CCM ?

Hawa CPV nyie CCM ni moja ya marafiki zenu sasa kwa nini msiige yaliyo bora muitoe nchi hapa ilipo.

Kwangu udikteta wa kichama kama ulipo hapa Tanzania na huko Vietnam na China angalau aina hii ya udikteta ni nzuri kwa sababu hata transition of power mara nyingi matatizo yanayoweza kutokea kwenye udikteta mwingine kwenye huu udikteta ni ngumu kutokea pia ni udikteta fulani unaoleta uwajibikaji wa pamoja na huchochea maendeleo ya haraka hasa pale ukitumika vyema kwa sababu wote mnakuwa na lengo moja nafikiri tunaona mahali Vietnam na China walipo na wanapoenda.

Haya hawa nao rafiki zenu CPC wa China ni moja ya vyama vya kisiasa bora kabisa duniani naposema bora namaanisha bora kweli kwa nini msijifunze kwao pia.

CCM mmekaa madarakani muda mrefu na mnajua mbinu za kuendelea kukaa madarakani muda mrefu kwangu hilo sio tatizo basi jifunzeni kwa hawa marafiki zenu CPC angalau mbinu ya kupunguza ukosoaji na matatizo ya kisiasa ndani ya nchi ni kuiinua nchi juu kiuchumi.

Mahali hao CPC wameitoa China na ilipo na inapoelekea mpaka leo kuwa tishio kwa mataifa ya magharibi sio jambo dogo hata kidogo.

Wenzenu hawa CPV na CPC ni madikteta kama nyie lakini wenzenu wana angalau sina tatizo kabisa na udikteta wa kichama wa hao wavietnam na wachina, huu udikteta wa kichama wa maendeleo ya taifa CCM mkiutumia sitakuwa na tatizo na nyie na nitawaunga mkono kwenye mambo yenu mengi yatakayo kuwa CCM.

Shida kubwa ya Watanzania ni maendeleo kelele zote hizi zitapunguzwa au kuzimwa kabisa hapa Tanzania endapo CCM mkijifunza na kuanza kua act kama wenzenu CPV na CPC.

Hakuna kazi ngumu kuwa ongoza Wavietnam walio zaidi ya 100M na Wachina walio zaidi ya 1.4Bln hawa wanatulizwa na kuongozwa vyema sababu nchi zao zinapata maendeleo makubwa na kuukimbia umasikini sasa CCM hamtaweza kutuliza sauti za Watanzania kwa mabavu bali maendeleo makubwa tu Watanzania wao wenyewe watakaa kimya maana hata vya kukosoa havitakuwepo.

Sasa nimbieni ndugu zangu leo hii sisi humu tungekuwa Wachina tungekuwa tunakosoa nini sasa kila siku nchini kwetu kwenda kwa CPC maana karibu kila kitu wanafanya hata ambavyo hatuja demand.

CCM jaribuni kubadilika
 
Ipi kufika huko lazima waue democracy na katiba nzima iwe restructured kuwa ya chama kimoja

Lakini sasa wako too late
 
Wala sio ngumu maana hata China CPC ndio inafahamika kuwa inatawala lakini kuna tuvyama tudogo dogo

Ukweli ni kwamba hata sasa nchini tupo chini ya chama kimoja hata katiba yetu ni ya muundo wa chama kimoja haikuundwa kukidhi mahitaji ya vyama vyingi kwa usawa.
 
Katiba ni mbovu..
CHina huko kiongozi aki ifisadi nchi adhabu yake ni kifo, hawataki mchezo ndio maana wapo pale...
Na ndicho wananchi Tanzania wanpambania kupata katiba mpya, hii katiba tuliyonayo ni mbovu.. haifai..
 
Katiba ni mbovu..
CHina huko kiongozi aki ifisadi nchi adhabu yake ni kifo, hawataki mchezo ndio maana wapo pale...
Na ndicho wananchi wanakipambania, hii katiba tuliyonayo ni mbovu.. haifai..
Katiba mpya ni muhimu
 
TANU/CCM haikujengwa kama CCP katika suala la uwajibikaji
Wakati Nyerere anazungumzia kuwachapa viboko mafisadi na wala rushwa China wao walikuwa wanawanyonga.
Basi kazi ngumu japo sina hakika kama hakuna mambo ya msingi watakayoona yakujifunza.

Njia ya mabavu hii inayoondelea kupitiliza haiwezi zima kelele za ukosoaji.

Umasikini unao kithiri unazidisha ukosoaji sijui CCM hawaoni hili kuwa ni tatizo
 
Suala lingine ni utamaduni, Wachina wana utamaduni wa uchapakazi tofauti na Waafrika, viongozi wazembe na wavivu wanatoka miongoni mwa jamii, Nyerere alikuwa anacheza bao na wazee wa Kiswahili nchi ikiwa bado masikini kabisa.
 
Haya ni mambo yanayofanywa na viongozi wenye vision. Sisi kwenye foleni tumepanga kina Samia, Makonda, Steve Nyerere ...... Nchi siyo tamasha la taarabu..
Kwa kweli kazi ipo na ubaya kamati kuu ya kisiasa kwa sasa ipokonywa nguvu zote na mwenyekiti angalau wenzao wavietnam na wachina bado kamati kuu zina nguvu hata za kumtoa katibu mkuu wa chama hapa kwenye kazi ngumu kweli kweli kumtoa mwenyekiti wa chama hata mawazo yake kupingwa au kukosolewa.
 
Mi mi sijali CCM mmeanza kuitawala Tanzania kwa muda gani na mtaitawala Tanzania kwa muda gani hata mkiitawala Tanzania kwa miaka 100 kwangu sawa tu.

Shida yangu kwa nini msiwe kama wenzenu CPV ya Vietnam angalia mahali Vietnam walipoitoa na kuamua kufanya Doi Moi leo Vietnam ipo wapi na inaelekea wapi ? Kidunia inazungumzwaje ukifananisha na Tanzania yenu mnayoiongoza CCM ?

Hawa CPV nyie CCM ni moja ya marafiki zenu sasa kwa nini msiige yaliyo bora muitoe nchi hapa ilipo.

Kwangu udikteta wa kichama kama ulipo hapa Tanzania na huko Vietnam na China angalau aina hii ya udikteta ni nzuri kwa sababu hata transition of power mara nyingi matatizo yanayoweza kutokea kwenye udikteta mwingine kwenye huu udikteta ni ngumu kutokea pia ni udikteta fulani unaoleta uwajibikaji wa pamoja na huchochea maendeleo ya haraka hasa pale ukitumika vyema kwa sababu wote mnakuwa na lengo moja nafikiri tunaona mahali Vietnam na China walipo na wanapoenda.

Haya hawa nao rafiki zenu CPC wa China ni moja ya vyama vya kisiasa bora kabisa duniani naposema bora namaanisha bora kweli kwa nini msijifunze kwao pia.

CCM mmekaa madarakani muda mrefu na mnajua mbinu za kuendelea kukaa madarakani muda mrefu kwangu hilo sio tatizo basi jifunzeni kwa hawa marafiki zenu CPC angalau mbinu ya kupunguza ukosoaji na matatizo ya kisiasa ndani ya nchi ni kuiinua nchi juu kiuchumi.

Mahali hao CPC wameitoa China na ilipo na inapoelekea mpaka leo kuwa tishio kwa mataifa ya magharibi sio jambo dogo hata kidogo.

Wenzenu hawa CPV na CPC ni madikteta kama nyie lakini wenzenu wana angalau sina tatizo kabisa na udikteta wa kichama wa hao wavietnam na wachina, huu udikteta wa kichama wa maendeleo ya taifa CCM mkiutumia sitakuwa na tatizo na nyie na nitawaunga mkono kwenye mambo yenu mengi yatakayo kuwa CCM.

Shida kubwa ya Watanzania ni maendeleo kelele zote hizi zitapunguzwa au kuzimwa kabisa hapa Tanzania endapo CCM mkijifunza na kuanza kua act kama wenzenu CPV na CPC.

Hakuna kazi ngumu kuwa ongoza Wavietnam walio zaidi ya 100M na Wachina walio zaidi ya 1.4Bln hawa wanatulizwa na kuongozwa vyema sababu nchi zao zinapata maendeleo makubwa na kuukimbia umasikini sasa CCM hamtaweza kutuliza sauti za Watanzania kwa mabavu bali maendeleo makubwa tu Watanzania wao wenyewe watakaa kimya maana hata vya kukosoa havitakuwepo.

Sasa nimbieni ndugu zangu leo hii sisi humu tungekuwa Wachina tungekuwa tunakosoa nini sasa kila siku nchini kwetu kwenda kwa CPC maana karibu kila kitu wanafanya hata ambavyo hatuja demand.

CCM jaribuni kubadilika
Uwizi na rushwa wamwachie nani?
 
Suala lingine ni utamaduni, Wachina wana utamaduni wa uchapakazi tofauti na Waafrika, viongozi wazembe na wavivu wanatoka miongoni mwa jamii, Nyerere alikuwa anacheza bao na wazee wa Kiswahili nchi ikiwa bado masikini kabisa.
Basi tuna tatizo kubwa sio kidogo
 
Basi kazi ngumu japo sina hakika kama hakuna mambo ya msingi watakayoona yakujifunza.

Njia ya mabavu hii inayoondelea kupitiliza haiwezi zima kelele za ukosoaji.

Umasikini unao kithiri unazidisha ukosoaji sijui CCM hawaoni hili kuwa ni tatizo
Suala la kujifunza limeshashindikana,
Jambo kubwa la kujifunza mfano ilikuwa ni jinsi CCP inavyopata makada na viongozi wake kwa merits na vipimo maalumu vya utendaji tofauti na CCM.
 
Kazi ngumu kweli kwa makada hawa machawa aisee kazi ngumu kupitiliza
 
Hii kwa Tanzania ilikua kazi nyepesi sana,Watanzania hawana shida wao wakipata mahitaji yao ya msingi tu hutawasikia wakileta shida.Magufuli angeweza kutupeleka huku,lakini itoshe kusema
 
Back
Top Bottom