TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,999
- 24,328
Chini ya Mkataba wa Montreal (Montreal Convention), mashirika ya ndege yana wajibu wa kisheria kuwajibika kwa mizigo iliyopotea, kuharibika au kuchelewa.
Begi kutofika kwenye mkanda wa kusafirisha mizigo 'baggage carousel' katika uwanja wa ndege si lazima imaanishe limepotea kabisa.
Mara nyingi mzigo unaweza kuwa umechelewa kufika au kusafirishwa kwa ndege nyingine. Hivyo, usiondoke uwanjani kabla ya kuchukua hatua muhimu.
Kwanza, nenda kwenye dawati la "Lost & Found" au "Baggage Service" la shirika la ndege ulilosafiria. Eleza kuwa mzigo wako haujafika na toa taarifa za safari yako.
Pili, jaza Property Irregularity Report (PIR). Toa maelezo sahihi kuhusu begi lako, ikiwemo rangi, ukubwa, chapa na alama zake.
Wasilisha pia baggage tag uliyopewa wakati wa check-in. Hakikisha unapewa nakala ya PIR pamoja na Reference Number ya kufuatilia mzigo.
Tatu, toa anwani na namba ya simu unayopatikana. Ikiwa mzigo utapatikana baadaye, mashirika mengi ya ndege huupanga uwasilishwe kwenye hoteli au anwani uliyotoa, kulingana na taratibu zao.
Nne, ulizia msaada wa mahitaji ya dharura. Ikiwa umecheleweshewa mzigo ukiwa na safari au ukae ugenini, ulizia kuhusu "Amenities Kit" au utaratibu wa kurejeshewa gharama za vitu muhimu kama nguo na vifaa vya usafi.
Hifadhi risiti zote za manunuzi ya dharura.
Mwisho, fuatilia mzigo mtandaoni kwa kutumia namba ya kumbukumbu ya PIR kupitia mfumo wa Baggage Tracker wa shirika la ndege.
Muhimu: Usiondoke eneo la mizigo bila kutoa taarifa rasmi.
Kuchukua hatua mapema hurahisisha ufuatiliaji na madai yoyote yanayoweza kuhusishwa na mzigo uliochelewa au kupotea.