mapema
JF-Expert Member
- Jul 21, 2014
- 640
- 1,881
Tokea nilipofikisha miaka 30 mpaka sasa mwaka wa 6 baadae, nimekuwa na hofu sana na maisha nikitazama nilipotoka na kulinganisha nilipo majibu ya ninakoenda hakuna nuru, mapambano ni mengi ila matokeo chanya ni machache sana.
Miaka kumi nyuma ilikua ni juzi tu hapo nilikua na miaka 20 na, miaka kumi mbele ni kesho kutwa hapo nitakuwa naitafuta 50!
Nilidhani hofu hii ni kwangu tu kumbe wengi ninaokutana nao wakiwa na umri wa miaka zaidi ya 30 wanaandamwa sana na hofu na kukata tamaa .
Kwa wale waliovuka umri huu ni vipi mliweza kuvuka hapa na vipi inavyowezekana kuondoa hofu hii?