Wasiwasi wa hapo inawezekana ni vile sasa unafikiria kikamilifu.
Wanaosema ni kujipata, sio hicho tu. Kuna mambo kama akili kupevuka na kuitambua maana ya maisha halafu unaanza kujiuliza hivi maisha ndiyo hayahaya? Yaani hata kama una gari na nyumba lakini sasa ndio wakatu unajiuliza hivi maisha ndiyo hayahaya tu.
Hapo umeshafanya kile ulichohisi ndio malengo ya maisha lakini bado haujatulia. Unaanza kujiuliza mbina sijihisi kutimia? Unajua wakati mwingine kubakia na lengo linalojulikana inakupa muelekeo usio na maswali mengi. Mfano tafuta hela, pata mtoto, nunua gari/nyumba ni 'straightforward' goals.
Shida ni vinawezekana na vinaisha u abaki na swali. Wazungu wanaita MidLifeCrisis.
Pendekezo la suluhisho: Jitengenezee/tafuta lengo la maisha lisilo na mwisho hadi mwiaho wa maisha yako na hautapata wasiwasi usioeleweka tena. Purpose - Endless mfano. Changia katika kuboresha maisha yangu na watu wote, Tafiti ulimwengu na etc chochote tu ambacho hakina mwisho na hakikuhusu peke yako kibinafsi.
View attachment 3104589