Na kama hujaoa ndio unakumbana na maswali na ushauri wa kuoa toka wanaoteseka na ndoa. Watakuhimiza kuoa huku wao wanataabika! Ukiwa na presha unaweza kuchua fisi unaliweka ndani.
Tulia maisha ni haya haya...hofu ni ukumbusho wa kuwekeza Kwa ajili ya uzeeni utapoisha nguvu ya kufanya KAZI.
Ndio hicho kinacho fikirisha mkuu, miaka kumi nyuma ni kidogo mno, wakati upende mwingine tunaona miaka kumi mbele ni mingi sana.
Hii imenipa wazo fulani la kurudi shule, miaka kadhaa mbele naweza kuwa na kiwango fulani cha elimu.