Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?

Rev.Kishoka said:
Sijaisoma hiyo paper ya Wangwe, naomba nitumie kwenye email Kishoka70@yahoo.com

Kishoka,

..good luck katika kuisoma ripoti ya Prof.Samwel Mwita Wangwe.

..ushauri wangu usije ukaisoma kwa mtindo ule wa Sheikhe Mazinge anavyosoma Biblia.
 
Zakumi,
No bob, mpango wa Ushanga theory hata haupandi! - kwi! kwi! kwi!

Bro:

Ninaweza kutumia mathematical model kuonyesha nguvu ya nadharia ya ushanga. Kitu ambacho huwezi kukipata kwenye Ujamaa.

Kuhusu kushindwa kwetu: Haya ni maneno ya mbunge wa chama cha Labour kuhusu uhuru wa nchi za kiAfrika kabla ya maandalizi.

To give the colonies their independence would be like giving a child a latch-key, a bank account and a short-gun.

Hivyo failures nyingi zilikuwa sio kuwa wakoloni hawakuachia hiki au kile, bali tulikuwa hatukuandaliwa au kujiandaa kupata uhuru. Na vicious cycles unaziona mpaka leo. Watu wanataka kutawala na sio kuongoza nchi.
 
Zakumi,
Ninaweza kutumia mathematical model kuonyesha nguvu ya nadharia ya ushanga. Kitu ambacho huwezi kukipata kwenye Ujamaa
Mkuu nafanya utani tu kijiwe kinahitaji kuchaka wakati mwingine!..ebu nipe somo la hiyo - Ushanga theory, sound interesting!
Kuhusu kushindwa kwetu: Haya ni maneno ya mbunge wa chama cha Labour kuhusu uhuru wa nchi za kiAfrika kabla ya maandalizi....
To give the colonies their independence would be like giving a child a latch-key, a bank account and a short-gun.
Well, it sound good to me rather than a child stand to be molested!..beside, he the molester feared most of him getting shot.. - kwi! kwi! kwi!.

Kuhusu Utawala mkuu wangu hatuna Ujanja maadam kila kitu tuna copy na ku paste kama Biblia na misahafu itabidi tuwe watu wa mwisho siku zote, hiyo vicious cycles inaanza pale mtu mweusi alipoona Nyapala akipeta toka enzi za kutawaliwa..

Waswahili wanasema basha yeyote lazima alifanyiwa yeye Nanahii utotoni wake, hivyo analipiza machungu..kwi kwi kwi!
 

Nadharia ya ushanga ni utani tu. Hila tunilipokuwa shule kulikwa na modeli za hisabati za kuelezea ni muda gani ugonjwa utasambaa kutoka katika chanjo fulani iwapo utajua kiwango cha kusambaa ugonjwa huo. Kwa mfano kipindupindi, anthrax na vilevile computer virus.

Nyumbani tulikuwa na utani kuwa kuna jamaa mmoja aliyependa wanawake. Jamaa huyu alikuwa anavaa ushanga kiunoni wakati akifanya mapenzi. Kila mwanadada aliyefanya naye mapenzi alisimulia rafiki yake kuwa jamaa anavaa ushanga (rumor monger). Na kila aliyepata habari hiyo alitaka ku-prove kama ni kweli jamaa alikuwa anavaa ushanga.

Hivyo katika kipindi fulani jamaa aliweza kufanya mapenzi na wanawake wengi bila ya yeye kutumia juhudi kubwa, alichotumia ni rumor mongers. Hivyo ukijua wastani wa muda jinsi rumor ya kuvaa ushanga inavyosambaa, basi unaweza kuelewa ni wadada wangapi watakaomtembelea jamaa kuona ushanga.

Kwa kutumia hekima au rumors za ushanga, basi hakuna sababu ya kiongozi kuhubiri maendeleo wakati maendeleo yenyewe hayajulikani na watu. Unatumia gharama nyingi na bado watu hawaelewi somo.

Cha muhimu kiongozi anachotakiwa ni kutafuta ushanga wa maendeleo (agent wa maendeleo). Na aanze na watu wachache ambao watakuwa rumor mongers baada ya kuonja maendeleo. Na hapa ukiweza kupata wastani wa muda wa kuenea mipango yako, basi unaweza kufanya estimation zako bila yeye wewe kufanya mikutano au kutumia gharama nyingi za usafiri.
 
Zakumi,

Hii habari moto sana na nadhani wanasiasa wameisoma vizuri.. hakika inaleta maana sana hasa kwa kina sisi wadanganyika ktk mazingira ya kushangaa na kisha kuvutiwa kusikia shanga zinavaliwa na mwanaume..Yaani hii ya shanga mkuu wangu ina fit many of our blunders..

As a fact hakukuwa na kitu cha maana kwa hao kina dada zaidi ya shanga lakini malipo yake ndio jamaa kaondoka na tunda la nguvu..

Pengine hizi tactics za shanga ndio wanaingia nazo wawekeshaji, maanake hata sielwi kama mtu ana akili zake timamu anaweza kwenda kulala na Barricks!
 
Zakumi na Mkandara,

Angalieni hii nukuu ya juzi kuhusu matumizi yetu, angalienin ni jinsi gani uagizaji wa mali na bidha unavyoongezeka kila siku huku uwezo wetu wa kuzalisha unaporomoka!

 
Rev, Kishoka,
Kwanza kipande hiki kidogo kimenipa utata kukielewa naomba kufahamishwa..

Kwanza kabisa bei ya dhahabu mwaka 2008 from Jan to Dec, ilikuwa juu ya bei iliyoandikwa hapo juu unless hilo neno Troy ounce lina maana tofauti na ile bei ya dunia kwa ounce.. January 2008 bei ilisimama Usd 846.65 (tofauti na amount waliyoiweka) na iliendelea kupanda mwezi hadi mwezi..ni mwaka ambao dhahabu imevunja record kwa bei..Na hakuna mwezi hata mmoja in 2008 bei ya dhahabu ilikuwa chini ya hiyo top amount waliyoiweka hapo juu ya 874.4, kwa hiyo haiwezekani 667.4 au 874.4 kuwa ni bei ya chini, juu wala wastani ktk mahesabu...
Labda kuna kitu sikielewi hapa!

Pili, ukichukua bei za mwaka 2007 na kulinganisha na mwaka 2008 nina hakika itakuwa zaidi ya hiyo 15% kwa sababu nakumbuka dhahabu imekuwa ikipanda bei kwa asilimia 20 kila mwaka kwa miaka mitano from 2000 -2005.. mwaka 2006 ilipanda asilimi 23, na 2007 asilimia 33...Ktk miaka yote ya 2000s iliyopita, mwaka 2008 imevunja record za kupanda kwa bei, sasa iweje tuambiwe was only 15 percent wakati kwa miaka zaidi ya 7 ongezeko limekuwa zaidi ya asilimia 15 kila mwaka?....
Wajuzi naomba somo!
 
Mkandara,

Your guess is same as mine, kushangaa takwimu za kininja! Labda Zakumi, Companero na Sikonge wanaweza kuwa na mtazamo tofauti!
 
Naomba kujua maana ya "Uhujumu Uchumi"
 
Uhujumu uchumi part 2 itafanikiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…