Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?

Kadri tunavyoendelea na majadiliano haya, tunakutana na vitu vile vile tunavyovizungumzia kwa mazingira ya leo.

Elimu duni, Ufanisi mbovu na duni, ukosefu wa Ubunifu, Sheria dhaifu, Utendaji, Uongozi na Ufuatiliaji butu, Sera mbovu na dhaifu, mfumo duni na dhaifu wa uchumi na uzalishaji mali, utegemezi na ukosefu wa uadilifu na uzalendo.

Leo hii tukisema tufufua vita vya Uhujumu uchumi kupiga vita Ulanguzi, Magendo na Ufisadi, je tutapigana vipi kwa matokeo bora ya manufaa na kufuata sheria kuliko vita vya Sokoine?
 
Hakuna correlation yoyote. Wanaoagiza sukari kutoka nje wanaweza kufanya hivyo iwapo tu sukari ya ndani ni bei kubwa kuliko sukari kutoka nje.

Hilo ni suala la Afya na quality control. Kwanini ulalamikie sukari wakati vitu vingi vyenye kutoka nje vina quality mbaya?


Umekubali sukari iingizwe kutoka nchi za nje; unakubali kuhujumu soko la ndani kwa kuleta bidhaa za kiwango duni kutoka nje!

Tena unatetea huo uhujumu uchumi kwa kwenda mbali zaidi na kuandika kuwa suala la Afya na kuquality control na unataka uliexclude na uhujumu uchumi. Hapana ndugu. Uhujumu ni uhujumu tu, ukiihujumu quality control unahujumu afya inturn unadidimiza human resources as a consequence unapunguza uzalishaji na hivyo kupunguza GDP.

Hapo hapo umeridhika kuwa kama sukari ina kiwango duni, it is okay ikiingizwa na kuuzwa nchini kwa bei nafuu kwa vile tu na bidhaa nyingine zina quality ya chini zinaingizwa nchini! Je kwa nini tusinunue bidhaa zinazozalishwa nchini ambazo zina kiwango cha juu na bei ya juu ?


Zakumi hii yote ni uhujumu uchumi, direct and indirect. Wanayoyaandika hapa Mkandara na Rev ni ukweli na ni ukweli mtupu.
 
Rev. Kishoka,
Mfano mwingine, yale mafuta ya Korie yalikuwa bei ndogo kuliko hata Kimbo kutoka Kenya. Sasa jiulize iweje tuende kuagiza mafuta inferior ya Korie, tukitukana Voil na Tanbond yake na hata kuwakwepa kina Blue Band na Kimbo?
__________________

Kwa sababu mafuta ya Korie yalikuwa na high level ya cholesterol.. cheap na kama ujuavyo mafuta mazito ndio mapenzi ya Mdanganyika! hao kina zakumi..Ingewezekana basi hata Diesel tungepikia chakula..
 
Rev. Kishoka,


Kwa sababu mafuta ya Korie yalikuwa na high level ya cholesterol.. cheap na kama ujuavyo mafuta mazito ndio mapenzi ya Mdanganyika! Ingwezekana basi hata Diesel tungepikia chakula..

Mkandara usinichekeshe, sasa leo hii kila mtu anakitambi mithili ya mimba ya miezi 9 kumbe ni mafuta mabaya kwa matumizi au kina Dr. Fupi waliKolimbalizwa kwa kusema kweli kuwa mafuta ya Korie yatatuletea shinikizo la damu na unono?
 


Rev Kishoka:

Hivi leo akitokea mtu na akisema sub-prime mortagage crisis ilikuwa na nia ya kuupindua ubepari, itabidi tumpe masikio?

Over-deregulation ina matatizo yake katika uchumi kama vile tunavyoona sasa hapa US.

Over-regulation nayo ina matatizo yake, kama yale yaliotokea Tanzania au katika nchi za kikomunisti. For God sake, Poland watu walikuwa wanapanga foleni kwa ajili ya mkate, kwanini sisi tufikiri matatizo yetu yalikuwa na external influence sio mapungufu ya siasa zenyewe?
 
Uhaba wa consumer goods ulioanza mwaka 1978 ndio uliozalisha uzembe wa kazi na kukuza rushwa katika Tanzania, matatizo ambayo yanatukabili hadi leo hii. Mwanzo wa phenomena hizo ulikuwa ni kile tulichoita kuhujumu uchumi. Ni Kutokana na ukweli huo ndiyo maana ninasema kuwa vita ya uhujumu uchumi ilikuwa na mantiki fulani ila iliendesha kwa kutumia njia mbaya sana ambazo zilikuwa illegal na ineffective. Ninafahamu kuwa ni kutokana na vita hiyo ndipo matajiri walipogundua kuwa inabidi nao wajihusishe sana na siasa za CCM kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahonga wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa. Kama vita ile ingefanywa vizuri na kutumia njia za kitaalamu, leo hii raia wetu wangekuwa na maendeleo hasa ukizingatia kuwa tulikuwa tumejengwa na msingi mzuri sana wa kujituma.

(a) Uhaba ule ulisababisha watu waliokuwa na access ni kile kidogo kilichokuwapo kudai rushwa ili waweze kukitoa kwa wengine. Watu hawa wakafaidika sana, tumeshaongea jinsi makarani wa RTC na National Milling walivyokuwa wanakufuru.

(b) Wale ambao hawakuwa na nafasi za kuwa na access za uhaba walitafuta namna ya kutumia nafasi zao nao ili ziwafaidie, ndipo msemo kuwa utakula kwenye deski lako ulipoanza: mapolisi wakaanza kuomba rushwa, mahakimu wakawa nao wanapokea rushwa, jambo ambalo lilikuwa mwiko mkubwa sana kabla ya hapo. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa rushwa, ikaingia kwenye utamaduni wetu kiasi kuwa tukawa tunamcheka mtu ambaye yuko kwenye nafasi inayoruhusu rushwa lakini hapokei rushwa.

(c) Kwa vile Azimio la Arusha lilikuwa bado linawabana viongozi wasijirundikie mali, wale wachache walioanza kupokea rushwa na kujipatia mali walitumia majina ya ndugu zao katika account za benki, na katika hati za majumba na biashara mbalimbali. Tabia hii bado ipo sana nchini ambapo siwezi kushangaa nikiambiwa kuwa ile nyumba yenye thamani zaidi ya Shs Bilioni mbili iliyotolewa na Mramba kama dhamana ikiwa imendikishwa kwa jina la mtu mwingine ni ya kwake mwenyewe.

(d) Baada ya Azimio la Zanzibar kuzaliwa, ingawa uhaba wa bidhaa ulianza kupungua, tamaa ya mali kwa njia ya mkato ilishapanda sana miongoni mwetu na watu walishajenga imani kuwa kuna njia ya mkato ya kupatia pesa. Rushwa ilipanda ngazi kutokea kiwango cha chini cha "chau chau" hadi ikaingia miongoni mwa watendaji wakuu wa serikali kama vile mawaziri na ikawa katika kiwango cha juu sana hadi kufikia 10% na 20% ya thamani halisi ya huduma. Mkapa alipoingia madarakani kiwango hiki kilipanda zaidi hadi 45% katika manunuzi ya serikali, kwa mfano radar na ndege ya rais, na zaidi ya 90% katika mikataba wa uuzaji wa raslimali mbalimbali za umma kwa mfano mradi wa Kiwira, uuzaji wa majumba ya serikali, na mikataba mbalimbali ya ardhi zenye madini.

Tulifundishwa kuwa mwanzo wa ngoma ni lele. Na wengine husema kuwa kuwasha moto ni rahisi, ila kazi kubwa ni kuuzima. Tulianzia padogo sana katika kujenga tatizo la rushwa kutokana na uhaba wa bidhaa tu, lakini sasa tatizo hilo limejikita sana katika jumuia yetu na kuwa kama kansa ya ubongo. Kuliondoa kunahitaji umakini wa hali ya juu sana.
 


Zakumi,

Katika Security intelligence spectrum, kilichotokoea Marekani ni suala la usalama wa taifa. Kuanguka kwa uchumi ni suala la usalama wa taifa hata kama si lazima apinduliwe mtu.

Jiulize ikiwa ulafi na uroho wa watu unajulikana na unatumika kama chambo na maadui kuangamiza Taifa, kuna shida gani basi kutokea mazingaombwe na hivyo uchumi wa nchi kuanguka?

Ikiwa China, Russia, India, Brazil na EU wanapigania kuwa na sauti kubwa kiuchumi, kisha wakatumia uroho wa Wamarekani na udhaifu wao wa kuwajibika katika kuwa na sheria kali, je si rahisi kuangamiza uchumi kwa kuwa na mipango mibovu ya kiuchumi ambayo huweza kutoa kipigo cha ajabu?

Je umesahau kisa cha Sovieti kuanguka chali pamoja na Ujamaa mbuzi ilikuwa ni mshindano ya silaha yaliyowekwa kama kiini macho na Reagan na kina Brezhnev wakakimbilia kuweka pesa zote kujenga silaha zinazopepea badala ya kujenga uchumi ndani ya nchi?

Uhujumu bwana Zakumi una sura nyingi sana na si siri kuna Wamarekani wanaoanza kuhoji na kujiuliza hivi kama Madevu Osama na ukichaa wake angeamua kuangusha uchumi na si kuua watu ingekuwaje?

Yesm it may be a conspiracy theory, however there are too many key facts that when are tied and woven together, ,they demonstrate a colusion or consipiracy to sabotage economy and country.

Je ni vigumu kuamini kuwa uhujumu uchumi was classic method ya kupindua Serikali kuliko mtutu wa bunduki?

Angalia outcome yake, maduka yakashehena na bidhaa za kuagiza, tukaanza kukopa hovyo na kutumia hovyo, tukashusha thamani ya sarafu, tukaanza mipango kibao ya kurutubisha uchumi kupitia IMF, tukamalizia na kufungua milango kwa wawekezaji.

Sasa tujiulize, miaka 23 baada ya Nyerere kukimbiza ubawa, je tumefaidika vipi kiuchumi na huu mfumo mpya ambao kwangu mimi mjamaa naona kuwa nusu yake ni nguvu za uhujumu uchumi?
 

Mama:

Naona umebobea kwenye sayansi au mathematics. Watu wenye sifa zenu precision ni kitu muhimu sana. Kwenu nyinyi 2+2 = 4.

Lakini hapa tuna-deal na maendeleo ya binadamu, uchumi na mabadiliko ya kidunia, hivyo kwangu mimi 2+2 = 6 is perfectly legal. Kinachotakiwa ni usahihi wa kutafsiri jibu langu.

Nchi zote zinakabiliwa na counterfeit. Unaweza kuuziwa Rolex ambayo sio Rolex na bado uchumi au maendeleo ya jamii yakaendelea kudunda.

Nyie mnaotaka mazingira perfect kwa maendeleo ya uchumi, you won't get it.
 
Tumezungumzia uzalishaji, uhaba wa bidhaa, ukosefu wa mbinu bora, ubunifu uliozubaa na tamaa kama sehemu za uhujumu uchumi.

Nimeleta habari iliyocapwa Daily News kuhusu suala la Sukari.

Sasa nawapa nukuu nyingine kutoka Daily News kuhusu kuotea kwa pato la Taifa kutokana an bidhaa za viwango vya chini u feki, jiulizeni kama huu si uhujumu ni nini?

Je 1983-84, tulikuwa na kiasi gani cha uhujumu wa bidhaa mbovu?
 


Likewize na sisi tungefanya juhudi zote zile lakini bila kuondoa Uzalishaji wa kijamaa tungeshindwa
 


Hahahahaaaa, kazi ipo lol!

Kwa kauli hizi sishangai kwa nini hatuendelei na kamwe hatutaendelea.

Huyo ecomomists gani asiyetumia hesabu ? Huwezi kuproject development na kustrategize kuondoa uhujumu uchumi and the sort kama hujiweki katika kutafuta mean ambayo lazima iwe na standard deviation au standard error, simple maths kutest accuracy.

Wewe hii unaikataa kabisaa na ndio maana unaona sawa 2+2=6! Nitamuelewa anayeona kwake ni legally correct 2+2= 4.5 more or less.


Kwa hiyo kumbe discussion yote ni bora liende, haina nia ya kuweka bayana tatizo na kutafuta suluhu. Bali ni simulizi na mahenga wetu. Mambo ya kufikirika, ndoto za alinacha.

Tanzania Tanzania yangu. Hufikiri na kudhani kuwa mabadiliko na Tanzania yenye neema na mendeleo kwa watu wake wote yanawezekana kwa kubadili uongozi. Uongozi kama ndio staili hii....hakuna kitu. Wizi mtupuuuuuuu!!!!!!!!!!!
 

Rev Kishoka:

Tulikuwa na mjadala mrefu katika ukumbi wa Business kuhusu kuanguka kwa thamani ya shillingi na inflation.

Moja ya tuliokuwa nayo kule ni kuwa nchi yoyote yenye kutaka kuwa na maendeleo ni lazima ipitie cycles za maendeleo. GDP itapanda na kushuka. Inflation itapanda na kuchuka. Wanaofanikiwa ni wale wanaoweza kutumia tools za uchumi au maendeleo ya jamii kutatua matatizo yao.

Matatizo ya siasa ya Ujamaa yalikosa tools ya kutatua matatizo ya kiuchumi au maendeleo. Tulipoanza na ujamaa tulifikiri kuwa maendeleo yataendelea kudondoka tu bila kupata matatizo. Na tulipopata matatizo hatukuwa na tools zozote za kututoa kule na kilichobakia ni kutafuta maadui.
 

. Naona wewe umekosea tu. Technically mpaka sasa sijasema + ni operation gani katika mlinganyo niliotolea mfano. Kuna uwezekano mkubwa kuwa operation yangu ilikuwa na maana kuwa operand ya kwanza plus 1 kujumlisha operand ya pili plus 1 = 6.

.
 


wizi mtupu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
wizi mtupu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Inawezekana kuwa ni wizi mtupu. Lakini kuna siku nilikuwa napitia kazi moja. Na jamaa akatokea kuzungumzia migogoro ya mashariki ya kati na tofauti kati ya Clinton na Bush.

Clinton approach ilikuwa sio ku-solve matatizo yanayotokea mashariki ya kati bali ya ku-manage. Hivyo kwa muda wote Clinton alipokuwa madarakani Sadaam Hussein alikuwa manageable. Na matatizo mengine ya mashariki hayakuleta matumizi makubwa katika matumizi ya kijeshi ya Marekani.

Kwa upande mwingine Bush aliingia na nadharia ya kutafuta solution. Kinadharia kama angeweza kuumaliza mgogoro wa Iraq katika kipindi kifupi basi asingetumia pesa nyingi katika migogoro ya mashariki ya kati. Lakini matokeo yake tunayaona leo.

Tukirudi kwenye mada ni kweli wanaoagiza sukari kutoka nje wanaumiza viwanda vya ndani au afya za wananchi, directly au indirectly. Lakini hili sio problem la kutafutia solution. Ni la kuli-manage tu hili ku-discourage import. Na zipo tools kibao tu zinazoweza kufanya kazi.

Mkandara na Wewe mnatafuta solution kama Bush. Mnatangaza vita dhidi ya watu na vita viishe kipindi fulani (mission accomplished). Matokeo yake vita haviishi na gharama zinazotumika ni kubwa kuliko faida.
 
Zakumi,
Hapana mkuu wangu wewe ndiye unatumia mifano ya Bush na washabiki wake ambao wanaamini kabisa kwamba Iraq ilikuwa na WMD...Kwa hiyo unatumia siasa za kitabu kurubuni watu wakati ukweli on the ground Saadam na jeshi lake walimalizwa na vita ya kwanza ya mzee Bush mwenyewe..
Pili, sio kweli Bush alitaka kumaliza mgogoro wa Middle East hata kidogo isipokuwa Bush alitaka kumwondoa Saadam ambaye alijaribu kumuua Bush baba asifanikiwe..Mafuta ya Iraq ni sababu ya pili baada ya saadam kutangaza atapokea tu Euro kwa malipo ya mafuta yake..Hakuna mtu wala kiongozi yeyote Marekani anayetaka kumaliza mgogoro wa mashariki ya kati bila Palestina na waarabu ku give in on Israel interest. Huu mgogoro mkuu wangu toka tuzaliwe upo leo hii kweli wewe unaamini kuna mtu anataka kusuluhisha kitu ambacho hakina suluhu zaidi ya mmoja wao ku give in!..
It's Politics of the world na inabidi watu kama nyie muendelee kuamini kwamba ipo siku moja kutakuwepo na amani middle East bila one of them to give in au kumwagika damu.

Jamani inabidi niulize hivi PUNDIT kapotelea wapi?..
 
Jackson Odoyo na Ellen Manyangu

SERIKALI imeshangazwa na kitendo cha wafanyabiashara wa mafuta nchini cha kupandisha bei ya bidhaa hiyo wakati kuna akiba ya kutosha inayoweza kutumika katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa.


Lakini kama imeshindwa kuweka ukomo wa bei ya bidhaa hiyo muhimu, na badala yake imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) kukutana na wafanyabiashara wa mafuta kujadili suala hilo na kulitafutia ufumbuzi.


Serikali imetoa kauli hiyo wiki moja baada ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta ghafla kwa madai kuwa shehena walizokuwa wakitegemea zinashindwa kuja kutokana na utekaji wa meli unaofanywa na maharamia wa Kisomali kwenye Bahari ya Hindi.


Awali wafanyabiashara hao walikuwa wakiuza mafuta hayo kati ya Sh1,300 na Sh1,400 lakini hivi katika kipindi cha kuelekea sikukuu ya Krismasi, yalipanda ghafla hadi kufikia bei ya kati ya Sh1,700 na Sh2,000 kwa petroli katika sehemu mbalimbali nchini.


Lakini kampuni ya mafuta ya BP iliendelea kuuza petroli kwa Sh1,450.


Jana, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa serikali haifahamu sababu za wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta.


"Hatuelewi kwanini wameamua kupandisha bei wakati mafuta yapo ya kutosha na yanaweza kutumika mwezi mzima," alisema Waziri Malima na kuongeza:


"Pamoja na kwamba mafuta bado yapo ya kutosha nchini, sababu ya msingi iliyowafanya wapandishe bei hiyo haijulikani."


Naibu waziri huyo pia alikanusha madai kwamba kupanda kwa bei ya mafuta kunasababishwa na meli zenye shehena ya mafuta kushindwa kufika nchini kwa kuhofia kutekwa na maharamia wa Kisomali na kusema kwamba madai hayo si kweli na hayana uhusiano na suala la kupanga kwa bei hapa nchini.


Alisema sababu nyingi zinaweza kujitokeza katika kipindi hiki, lakini ukweli ni kwamba sababu zote hizo hazina ushahidi hata kidogo hivyo haziwezi kuwa sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta katika vituo vya kuuza mafuta sehemu yoyote nchini.


"Wataalam wetu wamejaribu kutafuta sababu inayoweza kuwafanya wafanyabiasha hao kupandisha bei za mafuta kuanzia madai ya kuwepo kwa foleni kutoka mafuta yanapotolewa bandarini hadi yanakapofika kwa mtumiaji wa mwisho na kubaini kwamba hakuna mahusiano yoyote na kupanda kwa bei," alisema.


"Na wala hatuwezi kukubaliana na madai kwamba maharamia wa Kisomali ni chanzo cha kupanda bei mafuta... haya madai yote si kweli hata kidogo," alisisitiza.


Maharamia hao wa Kisomali wamesababisha hofu kwenye Bahari ya Hindi kutokana na kuendeleza vitendo vya utekaji meli na kudai fedha nyingi ili waziachie. Hata hivyo, hakuna taarifa zozote za kutekwa kwa meli yenye shehena ya mafuta ya Tanzania.


Katika soko la dunia, bei ya nishati hiyo imeshuka kiasi cha kugota kwenye dola 40 za Kimarekani kwa pipa kutokana na msukosuko wa kifedha ulioikumba dunia, kiasi cha kusababisha nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi dunia chini ya umoja wao wa Opec kukubaliana kupunguza uzalishaji wa nishati hiyo ili bei isioendelee kushuka.


Mahitaji ya mafuta katika nchi zenye viwanda, ambazo ndio wateja wakubwa wa bidhaa hiyo, yamekuwa yakishuka siku hadi siku kutokana na msukosuko huo, huku serikali za nchi hizo zikitaka mabadiliko katika teknolojia ya nishati inayotumika kuendeshea viwanda na magari.


Akizungumzia jitihada za serikali kukabiliana na tatizo hilo, Waziri Malima alisema kupanda kwa bei kunaathiri uchumi wa nchi na hivyo wizara yake imeiagiza Ewura kukutana na wafanyabiasha leo na kujadili suala hilo na baadaye mamlaka hiyo ipeleke maelezo kamili kuhusu suala hilo.


Alifafanua kwamba haiwezekani mafuta yakapanda hapa nchini peke yake wakati nje ya nchi yanakotolewa bei yake inazidi kushuka hivyo ni lazima Ewura itoe maelezo ya kutosha ya sababu za bei ya bidhaa hiyo kuzidi kwenda juu.


"Ninapenda kuchukua fursa hii kuwahakikishia wananchi kwamba serikali inafuatilia kwa karibu suala hili na itachukua hatua muafaka kila inapobidi ili kuhakikisha kuwa upatikanaji wa bidhaa za mafuta nchini unakuwa wa uhakika," alisema naibu waziri huyo.


Hata hivyo, alisema matokeo hayo yanadhihirisha kuwa bado kuna kazi ya kufanywa na Ewura katika kusimamia mifumuko mikubwa kama hiyo ya bei ambayo ina athari kwa uchumi na kwamba wizara yake kwa kushirikiana na chombo hicho na taasisi nyingine watalitafutia ufumbuzi suala hilo ikiwa sambamba na kulipatia utaratibu wa kisheria utakaoimarisha utekelezaji na usimamizi wa sheria na kanuni zake.


Mkurugenzi wa mafuta kutoka Ewura, Felix Gamlagosi alisema mafuta yapo ya kutosha hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi na yatatumika kwa mwezi mmoja na kwamba katika kipindi hicho mafuta mengine yatakuwa yameshawasili nchini.


Mbali na Gamlagosi kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi, alisema kuwa kisheria wao kama Ewura bado hawawezi kudhibiti upangaji wa bei ya nishati hiyo.


"Kisheria hatuwezi kupanga bei ya mafuta kwa sababu haizalishwi na mtu mmoja mfano..., waagizaji wa mafuta nchini ni watu 25 na wauzaji wa mwisho ni 900 sasa je, katika hali hiyo ni nani utakayeweza kumdhibiti," alihoji Gamlagosi.


"Bidhaa inayozalishwa na mtu mmoja kama umeme na maji ndiyo rahisi kuipangia bei na kuidhibiti ili wasifanye biashara ya kuwaumiza watumiaji wa mwisho."

Wazo:
Je hawa wanaotengeneza artificial demand kwa kumanipulate supply na hivyo kusababisha ongezeko la bei ya mafuta tunaweza kusema wanafanya ulanguzi na hivyo wanahujumu uchumi?

Kama mafuta yapo ya kutosha (tukiamini maneno ya Malima), na ya kuwa hakuna tishio lolote la msingi la supply, wauzaji wa mafuta wanapoamua kushikilia ugavi wa mafuta hayo ili kuongeza bei serikali ikiamua kufanya mshike mshike na kuwakamata itasemwa wanaonewa?

Nakumbuka wakati kimbunga kinakuja mwaka huu na mwaka jana, na siku chache kabla hakijapiga, bei ya mafuta hapa Michigan iliongezeka kwa kiasi kikubwa kwa madai kuwa refineries zilizoko gulf coast zitakuwa zimeharibiwa. Serikali ya Jimbo waliamua mara moja kuanzisha operesheni ya kutembelea vituo vyote vya mafuta ambavyo viliongeza bei ya mafuta pasipo msingi wowote na kuna watu ambao walikuwa cited na kulazimishwa kushusha bei kuakisi hali halisi ya soko.

Sasa leo hii JK na serikali yake wakianzisha operesheni ya kuwafuatilia hawa wenye mafuta ambao wanachezea soko kwa makusudi ili kupata faida ya haraka haraka wakitumia sheria ya 1984 na mabadiliko yake, tutasema wanaonewa? Au watu wanafikiri katika Tanzania hakuna uhujumu uchumi?
 
Mwanakijiji:

Ndio huo ni uhujumu uchumi lakini sio uhujumu uchumi. Nchi ni lazima ziwe na sheria na mikakati ya kukuza uchumi.


Soko huria lina mambo yake mojawapo ni kuweka kanuni za ushindaji na za biashara zenye kuwaza kuinua maendeleo ya wanachi.

Huwezi kuzitunga kanuni hizo bila soko lenyewe kuanza kazi na matatizo kujitokeza. Kwa matatizo yanayotokea sasa kanuni na sheria zinatakiwa kutungwa hili matatizo hayo yasitokee baadaye.

Hivyo sheria za 1984 hazitakiwi kutumika kwa sababu hazina innovation yoyote katika soko huru. Kwanza zilikiuka haki za binadamu na zinatakiwa kufutwa mara moja.
 
Nashauri kwamba ni vizuri kuionesha sheria hiyo ili tuweze kuikosoa sawasawa, kwani hadi hivi sasa hakuna ushahidi ulioletwa wa mapungufu ya sheria hiyo.Itafute halafu uje uioneshe ina makosa gani katika suala la soko. Kinachonishangaza zaidi hakuna aliyejaribu kuiweka sheria hiyo hapa na watu wakaichambua na kuonesha mapungufu yake. Aidha sheria ilikuwa na makosa au utekelezaji ulikuwa na makosa. Ninavyoona wengi wanapinga jinsi Operesheni ilivyoendeshwa. Wale wanaoipinga sheria hawajafafanua hasa mapungufu ya sheria hiyo ni yapi kwa kuonesha ushahidi wa wazi.

La pili, ni hatari kuisoma historia kwa vipande bila kuiunganisha. Leo hii mtu akisimama na kusema matatizo ya uchumi wa dunia yalianza mwishoni mwaka 2008 na chanzo chake kilikuwa ni kati ya 2007/2008 na akajikita kuangalia historia kwa kipindi hicho hafanyi haki kwa dhamira yake na wala kwa utashi wake. Wana historia ya kiuchumi wataangalia kiini cha chanzo cha matatizo ya kiuchumi wengine wanaenda nyuma hadi miaka ya utawala wa Clinton! Nimekaa pembeni kuangalia mjadala huu na kwa kiasi kikubwa watu wamebakia kuangalia mwaka 1983/1984 kana kwamba matukio hayo yalitokea katika ombwe. Waheshimiwa wengi wanazungumza kwa umakini na umahiri mkubwa lakini wanakwepa kupenya kwenye kingo za historia. Kuna mtu anajua ugavi wa bidhaa nchini ulikuwaje mwaka 1983/1984 na mahitaji yalikuwaje na hicho kilisabaishwa na nini? Hapa wasomi wetu wangetusaidia.

La tatu, ni jaribu la kuonesha kuwa Nyerere (Rais) na Sokoine (Waziri Mkuu) waliiamka tu alfajiri moja na kuanza kamata kamata; kwamba hawakuna na taarifa zozote aidha za kijasusi au za kiuchumi zilizosababisha maamuzi yao; kwamba wao wawili walijiamulia tu "hey Mr. President lets go and kamata walanguzi"! Really? Kwamba sisi leo miaka karibu thelathini baadaye tuna taarifa za uhakika kuwa yaliyokuwa ni "mawazo ya Nyerere na Sokoine"! I know some of us have an insatiable proclivity to arrogance, but I didn't think it'd be by this much! Kweli Nyerere na akili zake timamu aliamua tu kuanzisha operesheni kwa sababu anajisikia na hana msingi wowote isipokuwa wivu, chuki, ignorance of realities on the ground! Oh yeah? Ila sisi leo ndio tunajua "what actually happened" bila kuonesha angalau empirical data kwamba "hii x,y, na z ndivyo ilivyokuwa wakati ule na Nyerere hakujua hili"!

Oh well!... wengine yawezekana ni vigumu kutazama masuala ya uhujumu uchumi ya miaka ile kwa sababu familia zetu ziliathirika n.k Bahati nzuri ninakumbukumbu nzuri tu ya wafanyabiashara wa Tanga waliokuwa wanachimbia bidhaa nje ya majumba yao na wengine kutengeneza false doors... sizungumzii nilichosikia.. Ukiingia kwenye duka lao hakuna kitu; ila ukitaka kitu fulani unalipa fedha zaidi wanaenda kuchukua wanakujua wao wenyewe. Na walipozukiwa na vyombo vya dola.... hawakuwa na jjinsi ya kuelezea ndiyo maana siyo wote walioshitakiwa kwenye makosa ya kuhujumu uchumi wote waliachiliwa!

Now, ukija kwenye suala la jinsi lilivyotekelezwa huo ni mjadala mwingine all together kwani sijaona hadi leo hii nchi ambayo imeweza kuendesha operesheni yoyote ile na wananchi wake WOTE wakashangilia!

BTW: Nimeambatanisha hapa sheria nzimaya Uhujumu Uchumi na Mabadiliko yake.
 

Attachments

Mzee Mwanakijiji,
Believe me 20 yrs from now kuna watu watasema JK alikuwa mbumbumbu na mjinga kupitisha sheria hizi za Uhujumu uchumi, hata maswala ya EPA, Richmond na kadhalika ni blaaa blaa blaa, wataua kishenzi na kutungiwa hata hadithi yake...
Hawa wote mkuu wangu walikuwa watoto wa friji Open...wazee wao wakitumia zile Landrover na bendera za chama kufuata magunia ya mchele Kyela..Hawakumbuki ama hawakupata kuona jinsi mali ilivyokuwa ikitupwa baharini wengine wakizika mali na hela utafikiri anazikwa mtu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…