Nini dawa ya mwanamke mwenye wivu kupitiliza?

Joined
Sep 5, 2019
Posts
89
Reaction score
73
Nawasalimu.

Kama tujuavyo, wivu ni sehemu ya mapenzi lakini jamani ukizidi nahisi ni kero kubwa Sana Kwa upande wangu sijui Kwa wengine.

Mke wangu amekuwa na wivu ambao umekuwa Sam taim ni kero Sana. Kwamfano

-Simu yangu ikiingia sms / call lazima akurupuke na kwenda kuisoma ama kuipolea hasa ikiwa ni namba ngeni.

- Nikienda kazini (si mbali Sana na nyumbani) mara amekuja bila hata taarifa Kwa maana kwamba ananilinda.

- Nikiwa sebleni na eidha wageni ama jamaa. Kwa muda Tu mara ataniita ndani

- Nikisafiri atataka tuchati usiku wote, kwamba naweza kuwa na mwanamke mwingine..

- Wakati mwingine hata Nikienda chooni kukata gogo, mara amekuja, mara amegonga mlango kwamba amenimiss.

- Nikiongea na simu tukiwa wote, hata Kama naongea na mwanaume mwenzangu basi anaweza kuikwapua na kukata akidai kuwa naongea Sana na anataka aongee namimi Tu.

- Mara Kwa mara hukagua simu yangu, akikuta namba mpya ataipigia na kujua ni Nani. Kama ni mwanamke hata akiwa mteja wangu basi ni kesi.

NABOEKA SANA (ananiboa)

Ni mke wangu wa ndoa, na tuna miaka mitatu sasa na mtoto mmoja.

MSAADA TAFADHALI
 
Acha kuoa wanawake wafupi wanawivu uliopitiliza

Alafu wanawake wafupi ni shida kweli kweli maana wakiamua tu kuvimba bila sababu wanavimba haswaa.
Mkuu ishu yako ninkama yangu mimi naye wakwangu kila wakati na simu yangu ila mimi huwa namjibu tu kitu kimoja kuwa afuatilie na apekuwe tu ila akipata hicho anachokitafuta akalilie nje na asinisumbue kwa maswali. Kwa kifupi hawa wanawake wafupi wanahitaji uwe na mkwara mzito haswaa.
 
Back
Top Bottom