Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Serikali inapoamua kuchukua hatua dhidi ya masikini iweke usawa kama wanavyochukua Kwa matajiri. Tanzania hakuna tajiri anayekaa mahabusu, hakuna tajiri anayesota mahakamani, hakuna tajiri anayebomolewa nyumba Bila taratibu Kwa Sababu atadai fidia...Ila masikini Hadi huruma. Na pale tajiri anapopata shida watoto wake bado wanabaki mikono salama na wanaendelea na masomo tofauti na masikini.
Kuna clip nimeona; watu wa Gavoo wamebomoa nyumba nakumwacha Mzee na watoto Bila makazi. Unajiuliza hawa watoto nani wakuwalinda? Wana makosa gani? Kwanini serikali isiweke utaratibu wakuwachukua watoto nakuwaweka sehemu salama pale wanapobomoa makazi ya wazazi wao? Hawa ni watoto walioletwa Duniani, kwanini serikali ishiriki kuwanyanyasa?
Naomba Dr. Gwajima tusaidie...wewe kwako ni Haki watoto kuachwa Bila makazi? NI Haki kwako Kwa Sababu nyumba za wazazi zimebomolewa na serikali watoto walioachwa kwenye hizo familia wateseke? Mkiwa serikalini kwanini mnasau kwamba ninyi NI binadamu? Kwanini matatizo ya wananchi kwenu siyo kipaombele? Kama mtawatelekeza watoto hizo Haki za mtoto mtazilindaje?
Si wajibu wako kama mzazi na Waziri kulinda watoto wanaopata haya majanga? Hatuoni kwamba serikali inafanya ukatili na unyama Kwa watoto? Au Kwa Sababu serikali ndiyo umepelekea bomoa bomoa basi hakuna wakuwawajibisha?
Mnatengeneza majeraha na vidonda visivyotibika Kwa watoto; mnawafanya watu waichukie serikali na mwisho watawachukia watumishi WA serikali. Jitahidini kuwa na utu, vuta picha hao NI watoto wenu mngekubali wafanyiwe hivyo? Kuna mambo madogo yanafanywa lakini yanaumiza Sana hasa yakifanywa na MTU anayelipwa salary na anayetumwa na serikali.
Nikuombe uingilie Kati, timu yako ya ustawi wa jamii lazima iwepo kila eneo inapofanyika bomoa bomoa Kwa spirit ya kuangalia affairs za watoto.