Nini hasa maana ya utu?

Aisee Erasto Mpemba amepatikana, atakuwa mzungumzaji kwenye TedxDar - cheki profile yake hapa: TEDxDar
 

Aisee Erasto Mpemba amepatikana, atakuwa mzungumzaji kwenye TedxDar - cheki profile yake hapa: TEDxDar
 



Kama ulivosema hakuna Universal definition ya Utu.... Ndio maana hata huko nyumba nimezungumzia hili (kua kila mwanadamu hu-define utu) tegemea na mazingira alotoka.

Nimependa mfano wako na umenikumbusha kisa kimoja Uingereza ambao kuna mgonjwa alikua na hali mbaya na anaishi ICU kwa mipira tu; as in wakitoa hizo life supporters mara moja anakata roho. Kukawa na ugomvi mkubwa kati ya wazazi wa mgonjwa na mume (or is it mke... nimesahau). One group ikitaka awe released whereas another group ikitaka aendelee hivo hivo. The Irony is kila mmoja anatetea hoja yake on the basis of which was more humane.... Awe released ama aendelee....
 
Hello AD, samahani kwa kuchelewa kurespond nilikuwa safarini these last two days and it was for some busy thing hata laptop sikuweza kuigusa

All in all, unaweza kunisaidia kulifafanua hili swali vizuri kujua ni nini unataka kufahamu?

Thanks


Usijali kwa kuchelewa Cathode Rays... na naona ni zamu yangu ya kuomba huo msamaha wa kuchelewa....

Well simply nilitaka hili swali ulo pose ujibu as in according to your understanding and Point of view... basing on red...


The question still is how common and standards are these "common standards of achivements" ???
 
Dignity na utu? Daah

Dignity si inahusiana na heshima na taadhima? Au nimekosea?

Mkuu NN huwezi kuvitenga hivi vitu viwili......hudhani kuwa heshima na taadhima huthibitika zaidi palipo na utu?

Can any body respect you whole being au wewe unaweza kumpa mtu ile heshima ama taadhima anayostahili kama huna au huyo mtu hana utu!....close to impossible
 
Usijali kwa kuchelewa Cathode Rays... na naona ni zamu yangu ya kuomba huo msamaha wa kuchelewa....

Well simply nilitaka hili swali ulo pose ujibu as in according to your understanding and Point of view... basing on red...

AD ahsante kwa ufafanuzi na nashukuru kwa kunishtua kupita huku maana siku hizi nimekuwa kama matairi ya gari...kila siku barabarani safari

Anyway, nilichokuwa namaanisha ni ule ule mkanganyiko wa kitafsiri tuliotoka nao huko tulikotoka....kinachoonekana kama haki ya mtu au tuseme utu kwako sio lazima kiwe utu kwangu....

Kabla sijajibu kwa undani naomba nikumbuke moja kati ya nadharia nilizofundishwa kwenye somo la Social Development.....Ni ile nadharia ya Rationality kwenye Social Development (sio lazima sana kuwa sawa na theory ya rationality kwenye uchumi)...... Wanaounga mkono nadharia hii wanasema for development to be development it must be a rational process kwa maana ya mambo makuu mawili. Mosi, mtu mmoja asiendelee kwa mgongo wa mtu mwingine (hapa ndipo inapokuja concept ya inequality gap kwa tajiri kunufaika zaidi kwenye mgongo wa masikini say kwa kumfanyisha kazi za kujinufaisha wakati akimnyonya). Pili, Tunaotafuta maendeleo leo, tusiyatafute kwa kuathiri maisha ya vizazi vijavyo (hapa ndipo inapozaliwa concept ya sustainable development)..........Hata hivyo wanaopinga nadharia hii wanasema hakuna kitu kama rationality kwa sababu kila mtu anawaza tofauti na "what seems to be rational to you must not necessarily be rational to others"....hivyo ni kama kitu ambacho hakipo kabisa.

Kwa nini nimetumia mfano huu, ni kurudi kule kule tolikotoka.......kutafuta tafsiri moja ya jambo kama UTU ni gumu na kuna uwezekano wa kukesha na kukesha na kukesha na watu bado wasikubaliane kwenye baadhi ya maeneo kama jambo fulani linamaanisha kuwa huyo mtu ana utu au kakosa utu

Na nikirudi kwenye swali lako naomba nitumie mfano wa Article 18 ya UDHR inayosema


Kuna wakati nilibahatika kufuatilia mjadala wa Mashehe (kama sijakosea) huko Iraq na baadhi ya nchi nyingine za kiarabu zikizungumzia hii Article na Apostasy (mtu kubadili dini)...Na katika huo mjadala ilikuwa wazi kabisa kuwa stahiki ya mtu mtu aliebadili dini (Apostasy) anastahili kufa?..................Can we then say this "common standard Number 18" ya UDHR is common and standard to all? Je Muslim world wanaweza kuipokea kama standard of Achievements? Je huyu aliyebadili dini atahesabika kama aliefanya tendo la UTU kwa jamii aliyopo (kwake mwenyewe linaeza kuwa hivyo).....

Nakumbuka wale ndugu walisema (bila shaka kumbukumbu zangu ni sahihi) kuwa hizi UDHR lengo lake ni kupeleka "u-magharibi" na Ukristo kwenye Muslim World!....And it is the same thing tunachoongelea mfano kwenye Ushoga kuwa hawa ndugu zetu wa magharibi, kwa kutumia mgongo wa "haki za binadamu", wanataka kutulizimisha kufuata "u-magharibi" wao na kukubaliana na suala la ushoga....

Kwa hiyo utagundua jambo kama hili ni gumu...Yes they call them Common Standards lakini utaona kwa case kama hii they are not common and standards to others while to others, Yes they are

What might be rational to you might not necessarily be rational to others

Unconclusively
, Utu unaweza kutuchukua miaka 100 kutafuta common definition but "it just take a second to live it"
 
... Unconclusively, Utu unaweza kutuchukua miaka 100 kutafuta common definition but "it just take a second to live it"

Nakubali!
The best statement ever!!

@ Gaijin.... Nataka nisikie Gaijin ansemaje ... Akikubali hata kwa 2% .. I count the discussion closed!!
 
Akiongelea Utu, Dr. Martin Luther King Jr. alipata kusema hivi;
"Mtu anacho kimo kirefu ambacho chaweza kufikia viwango vya mbinguni, lakini pia anacho kina kirefu kinachoweza kufika umbali kuzimu ilipo"
Tafsiri katika kiswahili ni yangu/si rasmi.
 
Akiongelea Utu, Dr. Martin Luther King Jr. alipata kusema hivi;
"Mtu anacho kimo kirefu ambacho chaweza kufikia viwango vya mbinguni, lakini pia anacho kina kirefu kinachoweza kufika umbali kuzimu ilipo"
Tafsiri katika kiswahili ni yangu/si rasmi.


Nafikiri unachotaka kusema kiko hapo kwenye neno Viwango na Umbali!
 

Nakubali!
The best statement ever!!

@ Gaijin.... Nataka nisikie Gaijin ansemaje ... Akikubali hata kwa 2% .. I count the discussion closed!!

Azimio Jipya na wengine wote mliochangia, ahasanteni sana, hasa kwa kutohukumiana hata pale yalipoulizwa masuali ya kizushi. Naamini sote tumenufaika kwa namna moja au nyengine kwenye mjadala huu.

Rest assured kuwa Gaijin anakubaliana na zaidi sana ya 2% ya kilichozunguzwa na Cathode Rays pamoja na wengine
 


Pongezi zangu za kipekee kwako kwa kuwa "mchokoza mjadala" kwa kuuliza maswali yenye kutaka kutafakarisha zaidi....lakini pia kwa mwenyekiti wa kigoda hiki EMT na wachangiaji wote
 

Duh! You're so mean. LOL.
Zaidi ya asilimia 2 tuu?
Nilidhani asilimia 98?
Nimejifunza mengi sana kwenye huu mjadala.
Na maswali yako (whether ya kizushi or not) yalifanya tuumize vichwa ile mbaya.
Wewe ni mwalimu or have you been a teacher before?
 

hahahaaaa.........Nahisi mkuu Gaijin alianza kwanza kuwa mwalimu wa MEMKWA then akajitutumua kwa juhudi probably sasa he is heading to be Associate Professor
 

Pongezi zangu za kipekee kwako kwa kuwa "mchokoza mjadala" kwa kuuliza maswali yenye kutaka kutafakarisha zaidi....lakini pia kwa mwenyekiti wa kigoda hiki EMT na wachangiaji wote

.. Kweli we tend to forget Mchokoza mada ... na kumuona Gaijin zaidi .. I don't know why?


Alafu mchokoza mada nilifikiri unamjua Gaijin vilivyo ...the way mlivyoendesha mdahalo ...Sikutegemea hujui Profeshional yake kikamilifu ...
... Honestly ... Utu wenu unaelewana vizuri na hauna tatizo kwenye kuongoza mijadala kama hii!!
 
Nadhani kueleza maana ya UTU si rahisi kama inavyodhaniwa,ni suala ambalo linahitaji makubaliano yasiyo na uthibitisho wa kisayansi,ni la ki imani zaidi..nasema haya kwa sababu tukikubali historia ya neno Mtu,na kupokea neno utu ambao ni laazima upatikane kwa mtu,kama ubinadamu unavyo patikana kwa binadamu,basi hatutaweza kumlaumu asiye mtu kwa kukosa utu. mmasai sio mtu,mjaluo sio mtu,

hivyo hawa jamaa sio watu: hawana utu,(kwa maana ya kuwa hawafati dini ya watu)lakini ni binadamu na wana ubinadamu.....nakuja katika suala la utu kwa huyo mtu: si kila mtu ana utu ingawa huwezi kuwa na utu mpaka uwe mtu. utu ni kuamini na kufanya mambo ya watu,ni imani ya (dini) watu. mambo ambayo wao wanaona ni mazuri ukiyafanya umetenda jambo la kiutu,na ukikengeuka,umekosa utu.

Suala kubwa ni nani katika hao watu anayetamka kuwa hili ni jambo zuri hivyo ni la utu na hili si zuri hivyo si la utu kwa maana halistaili kufanywa na mtu?? kama mtamkaji atatamka kuwa jambo fulani ni zuri na watu wakaliamini,basi ni la utu,(kwao watu)....nimesema ni la kidini kwani nje ya hiyo dini utakuta jambo hilo ni hatari si tu kwa hao "watu" bali hata kwa wasio watu. "Nafikiria kuwa swali litaleta maana ya ni yapi matendo mema na ni yapi si matendo mema."
 
Kagenda Nimefuatia maelezo yako , nimeyaelewa lakini kuna mahali yakanichanganya ... Labda ni kuulize Kinyume cha Utu ni Nini ? Unakubali kuwa ni unyama?
 
Reactions: EMT
Kagenda II,

Mkuu, ukitumia etymology katika hili, utajikuta umeenda kwingine kabisa. Kwa mfano ukiliangalia hilo neno ubinadamu, kwamba linatokana na uwepo wa Binadamu, yaani Bin Adam au Mwana wa Adam. Licha ya kwamba neno hili lina mrengo wa jinsia ya kiume (bin) na kwa hiyo linawaweka kando akina binti, linarejea katika yule atajwaye katika imani za kiibrahim (Uislam, Ukristo na Uyahudi), yaani ADAM. Wajua kwamba Adam huyu alikuwepo hapa duniani takribani miaka 4000 tu iliyopita? Kwa hiyo si yule mama wa Afrika aliyeishi miaka zaidi ya milioni 3 iliyopita. Kwa maana hiyo wote wanaotokana na huyo mama si Binadamu!!

Aidha, kuhusu dhana yako kwamba utu ni suala la kidini, mimi nadhani unahitaji kutafakari zaidi, ni dini gani unazitaja hapa. Zingatia pia kwamba kabla ya ujio wa dini hizi (za kigeni) katika bara la Afrika, wakazi wa bara hili walikuwa tayari wanayo falsafa inayotambua na kuthamini utu. Utawasikia ndugu zetu wa Afrika Kusini kwa mfano, wakitumia msemo waliourithi kutoka kwa wahenga wao 'Omutu Gabantu' . Dokezo; Hayati Brenda Fassie alipata kuimba wimbo wenye dhima ya falsafa hii.
 
Reactions: EMT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…