Nini hasa maana ya utu?

Nini hasa maana ya utu?

[h=1]Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, maswali 50 ya kujiuliza[/h]"47. Kama nchi, Tanzania ilijijengea sifa kama taifa la watu wenye misimamo ya kujali utu, kuwajali wanyonge, kupigania haki kote duniani, kupinga ubeberu na kila aina ya uonevu. Sifa hizi zimekwenda wapi? Ni kitu gani kimetugeuza kuwa watu wa dhuluma na ulaghai, uroho, ulafi na ubabaishaji? Ni kwa nini tunakubali kupoteza tunu hii iliyotujengea sifa mbele ya mataifa mengine?" - Generali Ulimwengu.
 
Ni Kwa nini tunakubali kupoteza tunu hii iliyotujengea sifa mbele ya mataifa mengine? Hapa G ulimwengu alikuwa anamaanisha UTU!?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
WANAADAMU WASIO NA UTU

"Ikumbukwe kuwa binaadamu ni maumbile na ule uwezo wake wa kibaiolojia, ile hali ya kuwa na utashi ndiyo inaumba utu ndani yake"
... Wazazi/walezi wamesahau wengine wamelazimika kuyaacha majukumu yao kiasili kwa familia, wote tunafikiria namna ya kuongeza kipato, na kuwasahau watoto na hivyo wakitumia muda mwingi chini ya uangalizi wa wasichana wa kazi (naweza nisilaumu sana katika hili kwa sababu ni matokeo ya mfumo wa kiuchumi wa dunia, ambao ni matokeo ya migogro), na mara umri unapoongezeka wanaanza kujitafutia maadili na tabia kutoka kwa wenzao au kupitia mitandao ya internets, Video games na Televisions, hapo tutegemee matokeo yake yatakuwa ni nini?

Ni lazima tutapata wanadam lakini wasio na utu ndani yake, ndiyo ninaa maanisha asiye na utu, ikumbukwe kuwa binaadamu ni maumbile na ule uwezo wake wa kibaiolojia, ila hali ya kuwa na utashi ndiyo inaumba utu ndani yake.

Mada: Ole wako mwanadamu, BY Consigliere ... https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/130284-ole-wako-mwanadamu-2.html
 
Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, maswali 50 ya kujiuliza

"47. Kama nchi, Tanzania ilijijengea sifa kama taifa la watu wenye misimamo ya kujali utu, kuwajali wanyonge, kupigania haki kote duniani, kupinga ubeberu na kila aina ya uonevu. Sifa hizi zimekwenda wapi? Ni kitu gani kimetugeuza kuwa watu wa dhuluma na ulaghai, uroho, ulafi na ubabaishaji? Ni kwa nini tunakubali kupoteza tunu hii iliyotujengea sifa mbele ya mataifa mengine?" - Generali Ulimwengu.
The era of 'one nation one ideology' is gone.
Siku hizi kila mtu anataka afikiri mwenyewe na ajichagulie mwenyewe what is wrong and what is right.
I don't judge this, but tukae tukikumbuka kua freedom of the ones stops where freedom of the others start...
It has to be in such a way as the wamoja waweze kuwa stop wangine (Montesquieux).
 
Short clip (duration 2:50) from the presentation to His Holiness the Dalai Lama of the Mahatma Gandhi International Award for Reconciliation and Peace at the Kalachakra for World Peace in Bodh Gaya, India, on January 4, 2012.
AJ, nadhani kuna kitu muhimu anasema hapa:
We all have the potential of negative emotion, negative action, potential of positive emotion, positive action. So use our Human Inteligence to deliberately minimize the negative emotion and promote the positive emotions.
Kwangu mimi nadhani part of the definition is just there, in bold:
Utu ni ability ya kutumia Human Inteligence to deliberatly promote positive actions and emotions not just for us, but mostly for people around us.
Sijui mwasemaje?
 
Last edited by a moderator:
So use our Human Inteligence to deliberately minimize the negative emotion and promote the positive emotions. Kwangu mimi nadhani part of the definition is just there, in bold:
Utu ni ability ya kutumia Human Inteligence to deliberatly promote positive actions and emotions not just for us, but mostly for people around us. Sijui mwasemaje?
.
Kwa hiyo utu is based on emotion? Ukiwa na positive emotion unakuwa na utu and vice versa. Vipi kwa mtu ambae hana emotions za aina yoyote? Na vipi kuhusu wale wanaosema kuwa women are more emotional than men. If this is true ina maana kuwa wanawake wanaweza kuwa na utu zaidi ya wanaume?
 
.
Kwa hiyo utu is based on emotion? Ukiwa na positive emotion unakuwa na utu and vice versa. Vipi kwa mtu ambae hana emotions za aina yoyote? Na vipi kuhusu wale wanaosema kuwa women are more emotional than men. If this is true ina maana kuwa wanawake wanaweza kuwa na utu zaidi ya wanaume?

Mkuu hujanielewa. ninavoelewa mimi Utu sio positive emotion kama ulivo tafsiri hapo in bold, but niseme the ability to control your emotions in a way that benefit your fellow human beings (and maybe more). Kwa hiyo, wanawake kua more emotional than men doesn't mean that they are more human. It is only how they manage those emotions that could determine Utu wao.

Na hii process haitakiwi kua accidental, it should be a deliberate, conscientious move.
mfano naweza kutoa ni ban alio pigwa FaizaFoxy. Naongea kama member, siongei kama mod, na wala siongei kwa jina la alie toa ban:

Maybe mod alie mpiga ban alihisi kua kwa kusema alicho sema Faiza hakuonesha compassion kwa yule victim. This means that she was unable to promote a positive emotion (compassion). Instead she promoted a negative feeling (sorry I don't remember what she said exactly). So that denotes her inability to manage her emotions in a way that benefits her fellow human beings.

Of course, this raises the debate of what is a positive emotion and what is a negative one, who decides etc. Segolene Royale said that anger is a positive emotion when it is directed against social injustice. It could be, if the anger is controled, and used in the way nimezungumzia hapo juu.
What do you think?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Nadhani kueleza maana ya UTU si rahisi kama inavyodhaniwa,ni suala ambalo linahitaji makubaliano yasiyo na uthibitisho wa kisayansi,ni la ki imani zaidi..nasema haya kwa sababu tukikubali historia ya neno Mtu,na kupokea neno utu ambao ni laazima upatikane kwa mtu,kama ubinadamu unavyo patikana kwa binadamu,basi hatutaweza kumlaumu asiye mtu kwa kukosa utu. mmasai sio mtu,mjaluo sio mtu,....hivyo hawa jamaa sio watu: hawana utu,(kwa maana ya kuwa hawafati dini ya watu)lakini ni binadamu na wana ubinadamu.....nakuja katika suala la utu kwa huyo mtu: si kila mtu ana utu ingawa huwezi kuwa na utu mpaka uwe mtu. utu ni kuamini na kufanya mambo ya watu,ni imani ya (dini) watu. mambo ambayo wao wanaona ni mazuri ukiyafanya umetenda jambo la kiutu,na ukikengeuka,umekosa utu. suala kubwa ni nani katika hao watu anayetamka kuwa hili ni jambo zuri hivyo ni la utu na hili si zuri hivyo si la utu kwa maana halistaili kufanywa na mtu?? kama mtamkaji atatamka kuwa jambo fulani ni zuri na watu wakaliamini,basi ni la utu,(kwao watu)....nimesema ni la kidini kwani nje ya hiyo dini utakuta jambo hilo ni hatari si tu kwa hao "watu" bali hata kwa wasio watu. "Nafikiria kuwa swali litaleta maana ya ni yapi matendo mema na ni yapi si matendo mema."



EMT Sorry nipo out of topic BUT I could not help this.....

Kagenda bado you are almost brand new hapa JF (at least this ID of yours says that); Your second post at JF and it speaks volumes.... I am one of the member hufurahia saana kupata a fellow member with wonderful and interesting insights like hii post yako nime quote. Hopefully utaongeza speed ya post zako na ushiriki.... Karibu saana JF and hopefully tutazidi onana katika mijadala mbali mbali....
 
Utu ni ability ya kutumia Human Inteligence to deliberatly promote positive actions and emotions not just for us, but mostly for people around us.
Sijui mwasemaje?

Basi kinyume cha utu sio unyama? If it is, I should deduce that animals don't have that ability, shouldn't I? But how can we know if that deduction is true?
If this deduction is true, what are we to say about those instances where animals do seem to be deliberately arousing positive emotions in themselves and others (animal parents caring for their young, playing together, etc.)?
If it is false however and animals thus do have utu, is it right to call it "utu", "humanity", as if humans were the sole holders of this ability?
Utu/humanity encompasses all the characteristics that make humans human and so it distinguishes us from animals and objects after all, right?
 
Short clip (duration 2:50) from the presentation to His Holiness the Dalai Lama of the Mahatma Gandhi International Award for Reconciliation and Peace at the Kalachakra for World Peace in Bodh Gaya, India, on January 4, 2012.
AJ, nadhani kuna kitu muhimu anasema hapa:
We all have the potential of negative emotion, negative action, potential of positive emotion, positive action. So use our Human Inteligence to deliberately minimize the negative emotion and promote the positive emotions.
Kwangu mimi nadhani part of the definition is just there, in bold: Utu ni ability ya kutumia Human Inteligence to deliberatly promote positive actions and emotions not just for us, but mostly for people around us. Sijui mwasemaje?

I Loved how he used this key word ... HUMAN INTELLIGENCE ... Si unajua ukiangalia kwa karibu sana, its almost the same thing the Intellectuals call it .... EMOTIONAL INTELLIGENCE ... But his way is even much clear na kuondoa a lot of confusion ...Yaani the intelligence only found in Human being ..etc

... Nimeelewa vema how you have defined UTU basing on Him ... "The ability to use Human Intelligence" ... also real Love this ..

SO? Do you mean if we are able to define Human Intelligence as an ability only found in Human we will have definition of UTU in Place?
 
The era of 'one nation one ideology' is gone.
Siku hizi kila mtu anataka afikiri mwenyewe na ajichagulie mwenyewe what is wrong and what is right.
I don't judge this, but tukae tukikumbuka kua freedom of the ones stops where freedom of the others start...
It has to be in such a way as the wamoja waweze kuwa stop wangine (Montesquieux).

RR Do you want us to believe that ... GLOBAL IDEOLOGY ... Is on its way?

Hahah!! ... How will it Look Like? Na Itachukua muda gani hadi tufikie hapo?
 
Short clip (duration 2:50) from the presentation to His Holiness the Dalai Lama of the Mahatma Gandhi International Award for Reconciliation and Peace at the Kalachakra for World Peace in Bodh Gaya, India, on January 4, 2012.
AJ, nadhani kuna kitu muhimu anasema hapa:
We all have the potential of negative emotion, negative action, potential of positive emotion, positive action. So use our Human Inteligence to deliberately minimize the negative emotion and promote the positive emotions.
Kwangu mimi nadhani part of the definition is just there, in bold:
Utu ni ability ya kutumia Human Inteligence to deliberatly promote positive actions and emotions not just for us, but mostly for people around us.
Sijui mwasemaje?



Nilisikiliza Maongezi ya Dhalai lama.. Bahati mbaya saana..... Leo finally nataka niandike something on what he said (for I don't remember maneno yake word to word) inaniambia "Am sorry an error occurred. please try again later"....lol.... Enways....

Naamini kua ile tu kitendo cha kupromote emotions ziwe negative ama positive as opposed to zile ambazo zitaja naturally ni mtihani in it self. For hapo in other words an individual her/himself is in power of promoting and defining which are positive and which are negative emotions.... Hapa swali linakuja.... "Inakuaje pale ambapo wawili watachukulia positive emotions ya kitu kimoja oppositely?"

Nitolee mfano schools of thoughts of Slavery in Africa..... Miaka ile ya Slavery walikuwepo wanaharakati wengi saana wa kuzungumzia the whole concept and related activities of slaver. Kuna wale ambao waliamini kua Slavery is good for the Africans.... (sijui kama out of selfishness or if indeed ndio ukweli) NA kuna wale ambao waliamini kua Slavery is bad pia.... Na woote walikua watetea na hoja zilizo simama.....
 
Basi kinyume cha utu sio unyama? If it is, I should deduce that animals don't have that ability, shouldn't I? But how can we know if that deduction is true?
If this deduction is true, what are we to say about those instances where animals do seem to be deliberately arousing positive emotions in themselves and others (animal parents caring for their young, playing together, etc.)?
If it is false however and animals thus do have utu, is it right to call it "utu", "humanity", as if humans were the sole holders of this ability?
Utu/humanity encompasses all the characteristics that make humans human and so it distinguishes us from animals and objects after all, right?


Tatizo linakuja hapo.... Kama woote ni wanadamu.... Nani akisema hiki kitendo cha kinyama asikilizwe, na nani asisikilizwe....

Mfano:

Ukeketaji una pande mbili of observations....

One point of view

Mtoto wa kike anapokeketwa.... (katika jamii husika) Mama na ndugu wa yule mtoto huamini kua they are doing what is best for their child, as a result of years of traditions hence yageuka moja ya a stage really crucial to the gal child. With Great belief kua mtoto will have a better future hasa katika ndoa (in the sense of getting a husband na kitendo cha intercourse pia) akikeketwa. At the end of the day wenye malengo ya kutaka mtoto akeketwe do that out of Love for the child.... Huyo mama mtu anae ng'ang'ania mwanae akeketwe is the same one with mapenzi ya dhati juu ya mtoto wake... na would die for the kid to protect her; In this case one of the protection ni kumkeketa.

The other point of view

Wanaopinga kua binti asikeketwe.... mara nyingi they don't know the child in question... Not even responsible for the child wala welfare.... Don't even know her that well ki umri, tabia or whatever.... What matter kwa hawa wapingaji ni kua hicho ni kitendo cha kinyama kumfanyia binti yoyote yule no matter nani! They will fight for this kid for waelewa madhara in the long run, bila kujali mzazi ni nini atataka! Na wanafanya hivo because they care for they welfare of watoto wa kike..... Fighting in all their power kutokomeza kabisa!

SWALI: Kama woote ni wanadamu na woote twatumia "Human Intelligence" Who has the right to define the following:


  • Positive Vs Negative Emotions
  • Utu Vs Unyama
 
Chanzo: Gazeti la Raia Mwema, imeandikwa na Ayub Rioba



SAFU hii ya Fikra Mbadala ilisimama tangu katikati ya mwaka jana wakati nikiwa masomoni. Halikuwa kusudio langu kuacha kuandika lakini iliniwia vigumu kufanya mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja: kuandika safu na kuandika tasnifu. Nikakumbuka methali ya Mtaka Yote, Hukosa Yote. Nikachagua moja.


Wakati nikirejea leo hii ninawiwa na shauku ya kuwatakia kila la kheri wasomaji wa safu hii na gazeti la Raia Mwema kwa ujumla huku nikiwakumbusha kwamba kama ilivyokuwa huko nyuma, nitaendelea kudodosa fikra mbadala zinazoweza kukabili changamoto kubwa na muhimu katika maisha yetu kama watu na kama taifa.


Na madhali ninasisitiza katika kudadisi na kudodosa fikra mbadala, maana yake ni kwamba nitaendelea pia kuhoji fikra mazoea ambazo kwa muda mrefu zimetufunganisha na urithi wa ufukara na faraka na wakati mwingine kutufanya watu dhalili machoni pa binadamu wengine wa dunia hii.


Kama nilivyokwishabainisha siku zilizopita, kuhoji mazoea si jambo rahisi. Hata pale inapokuwa kwamba anayehoji yuko sahihi, mara nyingi walevi wa fikra mazoea humtazama yeye kama hayawani au kiumbe aliyechanganyikiwa.


Na historia, kama nilivyokwishakubainisha huko nyuma, inatufundisha kwamba walevi wa fikra mazoea siku zote hugoma kabisa kusikiliza fikra mbadala kwa kuamini kwamba kile wanachofikiri, wanachokijua na wanachokitenda ndicho Alfa na Omega.
Kwamba ndio ukweli wote kuhusu ubinadamu na kuhusu dunia. Kwamba hivyo ndivyo mambo yanavyotakiwa kuwa. Kwamba namna yoyote ile ya kufikiri, kujua au kutenda tofauti na fikra mazoea ni uasi unaotakiwa kuepukwa kwa juhudi zote.
Nilikwishajadili pia jinsi walevi mazoea wa enzi hizo walivyowahukumu kifo waumini wa fikra mbadala (Kumbuka Socrates na Galileo na hata Steve Biko miaka ya karibuni) kwa sababu tu walijaribu kuonyesha ukweli tofauti na mapokeo yaliyokuwa yamejikita katika fikra mazoea.


Safu hii itaendelea kuhoji bila ukomo. Lakini pia jambo la pili - na la msingi pia - safu hii itaendelea kukumbushia historia yetu sisi kama binadamu (hasa Bara la Afrika) tulikotoka, tulikopitia na tulipofikishwa leo. Kujua historia ni muhimu mno kwa binadamu yeyote anayehitaji kujitambua.
Na haitoshi kabisa kuijua tu historia kupitia miwani ya wageni waliotufanya watumwa, wakatutawala kimabavu na kuendelea kutuchezea shere hata baada ya miaka 50 ya uhuru.


Tunahitaji kuanza kufikiri zaidi, kutafiti zaidi, kujadili zaidi, kutafakari zaidi juu ya uwepo wetu sisi duniani. Haitoshi tu kwetu sisi, kwa mfano, kupaza sauti kila siku kuhusu dhana zinazotumiwa na binadamu wengine kana kwamba wao na sisi tuko sawa.
Haitoshi, kwa mfano, kwetu sisi kuanza kushadidia haki za binadamu, usawa wa binadamu kana kwamba na sisi pia ni binadamu wa daraja moja kama Wazungu, Waasia na wengine wenye rangi tofauti na yetu.

Kujifurahisha huku tunakokufanya kwa mazoea, eti na sisi ni binadamu kamili kama hao wengine, ndiko kunakoleta mkanganyiko mkubwa wa kimantiki katika michakato mingi tunayoibua – hasa tunayoletewa na wageni - inayokuwa na malengo ya kutuletea maendeleo (nitaijadili zaidi dhana ya maendeleo huko mbele).
Ninachojaribu kukisema hapa ni rahisi tu. Kwamba kimantiki endapo mtu mweusi anatangaza kwamba yeye ni binadamu kamili kama wengine, basi analazimika kufikiri, kujua na kutenda kama wale binadamu (ambao mpaka sasa wanajipambanua kama kipimo cha ukamilifu kifikra).

Haiwezekani huyu mtu mweusi akajiita binadamu kamili lakini akafikiri kama kuku, akawa na maarifa kama ya kuku, na wakati huo huo akajaribu kutenda kwa kuiga wale binadamu wengine wanavyotenda.
Matokeo yake ni mkanganyiko mkubwa unaotokana na ukweli kwamba yeye anaigiza kama binadamu kamili lakini anafikiri kama kuku, anajikuta na maarifa kama ya kuku na hata uwezo wake wa kuiga unakuwa unalingana na ule wa kuku.
Lakini bado eti hataki kabisa kujiita kuku-mtu, au basi mtu-kuku. Analazimisha aitwe mtu au binadamu. Na anaweza kupigana kwa hasira pale atakapoitwa – kwa maneno – mtu-kuku.
Lakini hajali kabisa kwamba fikra zake (za kikuku), maarifa yake (ya kikuku) na hata baadhi ya matendo yake (ya kikuku) vinamtambulisha kwa ufasaha zaidi kuhusu hadhi yake ya Ukuku-mtu.

Na ndipo linapokuja swali jingine la kimantiki. Kwamba je, ile tu maumbile ya huyu mtu mweusi kufanana na ya wale binadamu wengine (ambao ni kipimo cha ukamilifu) kunamfanya kuwa binadamu kamili? Je, kufanana tu kwa maumbile kunatosha kumfanya huyu mtu mweusi alazimishe kwamba na yeye basi ni binadamu kamili?
Je, ni katika kutembea kwake kwa miguu miwili huku akitumia mikono kwa shughuli nyingine ndipo anapata uhalali wa kuwa (au kuitwa) binadamu kamili? Je, pale Sokwe anapotembea kwa miguu miwili na kutumia mikono kwa shughuli nyingine naye pia anakuwa amepata uhalali wa kuitwa binadamu kamili? Au Kangaroo wa kule Australia ambaye ana ustadi mkubwa wa kutembelea miguu miwili anaweza kupata uhalali wa kuitwa binadamu?

Mantiki inashawishi kwamba sifa kubwa inayompambanua binadamu kamili na hayawani wengine ni kule kufikiri kwake, ambako humwezesha kutaka kujua zaidi na kujikuta akikusanya maarifa zaidi na ujuzi zaidi unaomsaidia katika kupambana na changamoto za kuishi kwake katika namna ambazo hayawani wengine hawawezi.
 
Gazeti la Raiamwema

Kitufe cha ku insert hyperlink kilishindwa kufanya kazi, nikashindwa kuweka link, but will go and edit right away, sir

Not a biggie, I was just wondering. Thought maybe you were also a columnist!
 
Back
Top Bottom