Nini hatima ya Nyerere Day? Lini mwisho wake?

Nini hatima ya Nyerere Day? Lini mwisho wake?

1.Nyerere day
2.Mkapa day
3.Magufuli day
Mfano: wafuatao nao wakiaga dunia kutakuwa na:-
4.Mwinyi day
5.Kikwete day
6.Samia day ....nk

Hivyo basi ili kuondoa kusiwe na siku nyingi sana za mapumziko.

Wazee wetu hao wote kwa pamoja,watakumbukwa siku ya uhuru wa Tanganyika.
Au siku ya mashujaa itakuwa pia maalum kwa kumbukizi ya hao wazee wetu.
 
Huwa nakaa chini nafikiria sana juu ya Hatima yaani mwisho wa kumkumbuka au kumbukumbu ya Nyerere.

Leo inatimia miaka 22 bila Mwalimu tangu alipo tutoka tarehe na mwezi kama wa leo mnamo Mwaka 1999.

Maswali yangu juu ya Hatima hii leo imetimia miaka 22 pasipo kuwa na Nyerere.
Je, Mwaka gani utakuwa ni mwisho wa kumkumbuka ya Mwalimu? Je, hata miaka 2000 inayo tutaendelea kuwa na Nyerere Day au itakuja kufa.

Na je, kipi kinaweza kufanya Nyerere Day ikome kuazimishwa?

Najua hapa wapo wenye IQ kubwa kama Zero IQ na Pia wapo wenye IQ ndogo kama Mimi. Hivyo kwa wenye IQ ndogo kama Mimi huenda wakapuuza nankuponda juu ya andiko hili.

Lakini kwa ndugu zangu mlio salia pengine mnaweza share chochote juu ya Hatima ya Nyerere Day na kuoendekeza je, huenda Mwaka/miaka gani inaweza kuwa Hatima ya Nyerere Day na sababu gani zinaweza fanya Nyerere Day ikome.
Maana sizani kama Nyerere Day itaadhimishwa miaka yote na sizani hata miaka 2000 au 3000 ijayo watu wataendelea kuadhimisha siku hii.

Je, nini Hatima ya Nyerere Day?
Wewe kweli ni Kasomi.

Legacy never die. Tatizo we unamtizama Nyerere. Wenzio wana enzi na kuishi legacy yake
 
Nyerere day
Kawawa day
Sokoine Day
Karume Day
Mkapa Day
Magufuli day

Tuongeze na wengine ili siku za mapumziko ziwe nyingi....alisikika mtumishi mmoja wa serikali akiomba.
 
Wewe kweli ni Kasomi.

Legacy never die. Tatizo we unamtizama Nyerere. Wenzio wana enzi na kuishi legacy yake
Nimekuelewa mkuu sababu zilizonifanya kuanzisha uzi ni kwamba lini itakuwa mwisho? Ina Maana hata miaka 3000 mbele atazidi kuazimishwa yaani mfano mwaka 5000
 
1.Nyerere day
2.Mkapa day
3.Magufuli day
Mfano: wafuatao nao wakiaga dunia kutakuwa na:-
4.Mwinyi day
5.Kikwete day
6.Samia day ....nk

Hivyo basi ili kuondoka kusiwe na siku nyingi sana za mapumziko.

Wazee wetu hao wote kwa pamoja,watakumbukwa siku ya uhuru wa Tanganyika.
Au siku ya mashujaa itakuwa pia maalum kwa kumbukizi ya hao wazee wetu.
Kweli wao tutawakumbuka kwa siku moja ila huyu Muasisi yeye atakuwa na siku yake special
 
Nyerere day
Kawawa day
Sokoine Day
Karume Day
Mkapa Day
Magufuli day

Tuongeze na wengine ili siku za mapumziko ziwe nyingi....alisikika mtumishi mmoja wa serikali akiomba.
Duh hapo na bado zitaongezeka na days zingine
 
Hii siku ni muhimu sana, lakini inakuwa ya kuliingiza taifa hasara ya matumizi ya fedha kutokana na ukweli kuwa siku hii imekuwa ya kutoa matamko tu ya kumenzi hayati Mwl Nyerere lakini ikipita tu, kila mtu anaendelea na mambo yake, hakuna viongozi Mjamaa/Mkomunisti

1.Nyerere day
2.Mkapa day
3.Magufuli day
Mfano: wafuatao nao wakiaga dunia kutakuwa na:-
4.Mwinyi day
5.Kikwete day
6.Samia day ....nk

Hivyo basi ili kuondoka kusiwe na siku nyingi sana za mapumziko.

Wazee wetu hao wote kwa pamoja,watakumbukwa siku ya uhuru wa Tanganyika.
Au siku ya mashujaa itakuwa pia maalum kwa kumbukizi ya hao wazee wetu.
Ninawakubali sana Hayati Mkapa na Mzee Mwinyi kwa sababu walikuwa na sera za kibepari zenye kuleta tija kwa Taifa. Hata Kikwete alifanya vyema.

Siwakubali Nyerere na Magufuli kwa sababu sera zao za kijamaa zilikuwa hasara kwa Taifa na hazikuleta tija zaidi ya mateso na vilema vya kiuchumi kwa nchi.

Samia ni mzuri pia kwa sababu ana itikadi za akina Mwinyi, Mkapa na Kikwete
 
Nimekuelewa mkuu sababu zilizonifanya kuanzisha uzi ni kwamba lini itakuwa mwisho? Ina Maana hata miaka 3000 mbele atazidi kuazimishwa yaani mfano mwaka 5000
Legacy inaishi historia haiwezi futika
 
Jifunze lugha kwanza ndo ujadili mambo usiyoyaweza wewe dogo! Ni kuadhimishwa na siyo "kuazimishwa"! Nikisha ona hivyo huwa najua wewe ni product ya shule na vyuo vya kata! Weupeee vichwani !
 
Jifunze lugha kwanza ndo ujadili mambo usiyoyaweza wewe dogo! Ni kuadhimishwa na siyo "kuazimishwa"! Nikisha ona hivyo huwa najua wewe ni product ya shule na vyuo vya kata! Weupeee vichwani !
Yaani nyinyi mlio soma shule za kubebwa na magari ya njano ndio hakuna kitu kabisa.
Kazi kubebwa tu.
 
Wanamkumbuka vyema

Hakuna cha vyema apo,,,cpendi kuona wa2 wakinyanyacka na kuzulumiwa,,,hizo national housing inasemekana wahindi walijenga kwa hela zao babu akazitaifisha, ni mdini, hakuwa akiwapenda waisilamu. Hii ki2 mimi imenikera munoo.
 
Back
Top Bottom