Nini hatima ya vijana wa taifa la Tanzania na matumizi ya pombe kali? Tujadili kidogo

Death favors no man,kila mtu atakufa wakati wake ukifika.Vijana hawajapenda kufika hii hatua ni makosa yaliyofanyika vizazi kadhaa nyuma au makosa ambayo jamii imefanya katika malezi(haya ni matokeo, tafuta chanzo ndio utapata ufumbuzi wa tatizo,matokeo hayana kazi sana kwenye kutatua tatizo bali chanzo chake)
Mkuu lakini hali inatisha sn mpk mtu unaogopa asee, mwanzoni ilikuwa ni mjini sahivi mpk vijijini hali ni mbaya zaidi, lazima tutafute solution ya tatizo mapema
 
Ukipima kupitia nature takwimu ni zilezile... Zamani watu walikua wachache ndio maana ulikua unaona wazee fulani mmoja mmoja wamelewa chakari kumbe hawakua wazee bali ni wababa wenye familia changa kama uonavyo leo.
Watoto wadogo wanawaona ni wababa lakini wewe unaona ni vijana kwakua wewe ni mzee wa makamo 😆

Sasa basi tukirudi kwenye mada ni kwamba takwimu hazijabadilika sana sababu watu wameongezeka mara dufu.

Kulingana na uwingi wa watu ni ngumu kuelewa hili ila hesabu vijana mtaani kwako utakuta walevi wabobevu ni wachache kuliko vijana wasio walevi.... Kilichoongezeka ni msongo wa mawazo tu
 
Hivi karibuni kumeshuhudiwa kuongezeka kwa matumizi makubwa ya pombe kali, hususa kwa vijana kati ya miaka 15 mpk 30, kubeti, uvutaji bangi, mirungi, movi za hovyo, miziki ya hovyo n.k, kama taifa tutegemee nini haswa? vijana wengi sahivi hawataki kazi wala hawana nguvu za kufanya kazi, ni wachache sn wanaokwepa huu mtego, hatuoni kama kuna hatari huko mbeleni?
1. Kutakuwa na wagonjwa wengi sn wa figo, ini na mapafu 2. Taifa linapoteza nguvu kazi pamoja na walipa kodi 3. Mmomonyoko wa maadili kwenye jamii unashuka kwa kasi sn 4. Kuongozeka kwa wizi mitaani n.k
Ukitaka kutajirika kwa haraka wakati huu wewe fungua kiwanda cha pombe kali au weka mashine za kubeti n.k, Je serikali yetu haioni hii hatari mbeleni? Naomba tuweke siasa pembeni tujadili kuokoa kizazi cha kesho. Karibuni wote, natamani Waziri Gwajima ni wanaFJ Wizara yake inahusika na hili kundi.
infact,
hiyo ni changamoto ambayo kwa kiasi fulani inachochewa sana hata na viongozi wa vyama vya siasa nchini ambao baadhi yao wamekua role modes wa wananchama wao hususani vijana katika ufakamiaji wa mipombe na nyama. Sote ni mashuhuda tumeona na tunaendelea kuona hayo.

Viongozi wanafakamia mipombe uloitaja kwenye hoja mahususi hadharani, mipombe mingine michungu ambayo ukitaka kumeza lazma ukunje sura.

Na wengine hadi wanaomba kuchangiwa pesa wakidai ili ziwasaidie kufanya jambo fulani, kmbe ni kwaajili ya kununua pombe na nyama. Ndio maana umeona saivi vijana wengi ndani ya vyama vya siasa ni majasiri sana kuporomosha matusi hadharani bila woga kumbe ni kwasababu wamefadhiliwa na kuchochewa na pombe na viongozi wao ili kutukana na kusababisha fujo katika jamii.

Mi nadhani viongozi wa kisiasa wakiacha pombe, tatizo la ulevi litapungua kwa kiasi kikubwa nchini na mihemko, ghadhabu na kuporomosha matusi kwa vijana ndani ya jamii kutapungua sana.

Lakini pia athari za pombe kwenye afya za vijana zitapungua pia.
Tuwafundishe vijana maadili mema, sio kuwafundisha kufakamia pombe na kuporomosha matusi.

Kunywa pombe kistaarabu.
Unywanji pombe kupita kiasi na hatari kwa afya yako, isiuzwe kwa walio na umri wa chini ya miaka18 :NoGodNo:
 
Ukipima kupitia nature takwimu ni zilezile... Zamani watu walikua wachache ndio maana ulikua unaona wazee fulani mmoja mmoja wamelewa chakari kumbe hawakua wazee bali ni wababa wenye familia changa kama uonavyo leo.
Watoto wadogo wanawaona ni wababa lakini wewe unaona ni vijana kwakua wewe ni mzee wa makamo 😆

Sasa basi tukirudi kwenye mada ni kwamba takwimu hazijabadilika sana sababu watu wameongezeka mara dufu.

Kulingana na uwingi wa watu ni ngumu kuelewa hili ila hesabu vijana mtaani kwako utakuta walevi wabobevu ni wachache kuliko vijana wasio walevi.... Kilichoongezeka ni msongo wa mawazo tu
Zamani sn miaka 2000 nipo msingi viwanda vya alzeti vilikuwa vingi na viwanda vya pombe vilikuwa ni viwili kanda ya kaskazini nzima TBL na Serengeti, leo hii viwanda vya pombe kali ni vingi(karibu kila mtaa) kuliko viwanda vya alzeti kwanini?
 
Zamani hawakuweza kunywa pombe za viwandani bali walikunywa pombe zilizokuwa zinatengenezwa mtoni (chang'aa)
 
Hivi karibuni kumeshuhudiwa kuongezeka kwa matumizi makubwa ya pombe kali, hususa kwa vijana kati ya miaka 15 mpk 30, kubeti, uvutaji bangi, mirungi, movi za hovyo, miziki ya hovyo n.k, kama taifa tutegemee nini haswa?

Vijana wengi sahivi hawataki kazi wala hawana nguvu za kufanya kazi, ni wachache sn wanaokwepa huu mtego, hatuoni kama kuna hatari huko mbeleni?

  • Kutakuwa na wagonjwa wengi sana wa figo, ini na mapafu.
  • Taifa linapoteza nguvu kazi pamoja na walipa kodi.
  • Mmomonyoko wa maadili kwenye jamii unashuka kwa kasi sana.
  • Kuongezeka kwa wizi mitaani, n.k.
Karibuni wote, natamani Waziri Gwajima ni wanaFJ Wizara yake inahusika na hili kundi
Inaumiza sana vijana wengi wameshajikatia tamaa ya maisha😢😢
 
Zamani hawakuweza kunywa pombe za viwandani bali walikunywa pombe zilizokuwa zinatengenezwa mtoni (chang'aa)
Sahihi lakini hazikuwa na madhara kama za leo, miaka 3 nilikuwa nalima kupata vibarua ni ngumu sn vijana muda wote wamelewa, kipindi cha Magu 2020 vibarua walikuwa ni wengi kupita kiasi, fanya research
 
Kwa sasa kinachofanya walewe haraka ni njaa na msongo wa mawazo....zamani ilikua mtu halewi haraka ndio maana walipendelea kunywa namba
 
Mkuu lakini hali inatisha sn mpk mtu unaogopa asee, mwanzoni ilikuwa ni mjini sahivi mpk vijijini hali ni mbaya zaidi, lazima tutafute solution ya tatizo mapema
Solution ni kujua kwanini tunaona hii picha kwa vijana.Hakuna kiumbe mwenye akili timamu atatumia siku nzima kulewa tena pombe kali,kuvuta bangi,kubeti au kufanya anasa yoyote.

Ni matokeo ya misongo kwa vijana,vijana kushindwa kuona kesho yenye mwanga na malezi ya hovyo.Mfano,mtu kafanya elimu yake miaka 15+ ,anagraduate (mbaya zaidi kama alipata na mwenza akiwa chuo)anakosa namna nzuri ya kutumia maarifa yake,(kufanya jambo kuwa gumu,jamii ina mu-attack indirectly)mwisho wa siku itakuwa kama hivi.

Nini kifanyike:wazazi watoe malezi bora kwa watoto wao, pamoja na kuwaonyesha pande zaidi ya moja katika maisha(sio tu mtoto kwa sababu akiamka anakuta mkate na siagi basi ukashindwa wewe mzazi kumuonyesha kuwa kuna magimbi pia hutumika wakati wa kifungua kinywa.Hii ina msaada badae akiwa exposed kwenye mazingira magumu).

Kwa wahitumu wa chuo:Jamii iwape muda kwanza katika hii transition period(kutoka katika elimu ya nadharia(theories,principles..etc) nakuingia katika jamii ambapo elimu yao inabidi kutoa matunda)

Jamii isiwashambulie bali iwape kitu tunaita positive reinforcement pale ambapo watakuwa wameshindwa kupata match kati ya maarifa waliyopata shuleni na jamii ambazo watakuwa wanaishi baada ya maisha ya shule kufika tamati.
 
Point sn
 
Back
Top Bottom