Nini hatma Amana zetu?

Nini hatma Amana zetu?

Muuza viatu

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2020
Posts
3,840
Reaction score
7,920
Wengi wetu siku hizi tunahifadh pesa ktk mitandao ya simu au ktk mabenki tena muda mwingine unakuta hifadhi hiyo inakuwa ya siri hata familia na marafiki hawajui.

Hili kisheria linakuaje inapotokea muhusika wa akaunti husika anapokaa muda mrefu bila ya akaunti yake kutumika kwa namna yoyote ile kuna namna taasisi husika inapaswa kufanya ili kujua hatma ya mteja wao au hata ikitokea ikabainika amefariki kuna namna wanalazimishwa kuwarudishia warith stahili za mpendwa wao?
 
Urithi wa nchi huo!
Kama ni urithi wa familia msimamizi wa mirathi angekuwa kishachukua.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Pesa ambazo hazijawa claimed kwa miaka mitatu zinarejeshwa benki kuu, including za kwenye mitandao ya simu
Zinapelekwa benki kuu baada ya taasis husika kuamua yenyewe tu kuzipeleka au kuna taasis inayofatilia miamala na kuamua inapotokea hali hiyo???
 
Urithi wa nchi huo!
Kama ni urithi wa familia msimamizi wa mirathi angekuwa kishachukua.

Everyday is Saturday............................... [emoji41]
Nilimaanisha kwa zile pesa ambazo huwa tunazihifadhi kwa kificho bila ya wetu wa karibu kujua
 
Ndiyo hizo hizo hurithiwa na SERIKALI.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Zinapelekwa benki kuu baada ya taasis husika kuamua yenyewe tu kuzipeleka au kuna taasis inayofatilia miamala na kuamua inapotokea hali hiyo???
Ni requirement ya kisheria kwenye sheria ya huduma za fedha za Tanzania, kwamba pesa ambayo haijawa claimed na wahusika kwa muda fulani, lazima iwe reported benki kuu na irejeshwe benki kuu. Mfano, mtu akifariki na pesa zake zilizo kwenye laini ya simu kazijatolewa kwa muda unaostahili (laini ya simu ina expire baada ya miezi mitatu) kama haitumiki, basi zile pesa zinaondolewa kwenye akaunti husika na kurejeshwa serikalini (benki kuu). Ni takwa la kisheria, sio maamuzi ya mabenki ama kampuni za simu.
 
Sawa
 
Back
Top Bottom