Nini hatma ya Shilingi ya Tanzania baada ya kuporomoka dhidi ya Dola ya Marekani?

Nini hatma ya Shilingi ya Tanzania baada ya kuporomoka dhidi ya Dola ya Marekani?

Wachambuzi wenye vimelea vya uchawa wanasema " hakuna uhusiano wowote kati thamani ya shilingi na ukuaji wa uchumi" na mifano yao ni thamani ya shilingi ya Kenya na Tanzania.
Estonia wanatumia Euro na uchumi wao bado upo kwenye recession.
Euro kwa miaka mitano ipo na thamani karibia ile ile against USD.
Na kuna nchi nyingi za Euro uchumi wake haupo kwenye recession.
 
Kenya wanazalisha na kuuza kwa wingi nje, uswahilini tunaagiza zaidi nje kuliko kuzalisha na kuuza
Rand Moja ya South Africa ni sawa na Japan yen 8.
Na Japan ndie anae export zaidi ukilinganisha na South Africa. Hili unali zungumziaje bwana mchumi
 
Nadhani inabidi tutoke huko kwa kutegemea Dollar ili maisha yetu yaweze kwenda..., Tungekuwa wazalishaji basi tungeshangilia hii hali sababu vitu vyetu vingekuwa cheaper katika soko....

Na tunafanyeji hivyo ? Ni kuacha kutafuta dollar ili kununua vitu ambavyo mahitaji yake sio ya lazima au tunaweza tukawa na alternative..., Mfano mdogo Sasa hivi tunapigia chepuo nishati safi kuacha kutumia mikaa na tunapigia chepuo LPG ambayo tunaagiza, kitu ambacho tunatumia fedha za kigeni; wakati tungeweza kutumia umeme katika kupikia hence kuondoka na matumizi hayo...

Watakwambia umeme ni hatari kwa kupikia
 
Back
Top Bottom