Nadhani inabidi tutoke huko kwa kutegemea Dollar ili maisha yetu yaweze kwenda..., Tungekuwa wazalishaji basi tungeshangilia hii hali sababu vitu vyetu vingekuwa cheaper katika soko....
Na tunafanyeji hivyo ? Ni kuacha kutafuta dollar ili kununua vitu ambavyo mahitaji yake sio ya lazima au tunaweza tukawa na alternative...,
Mfano mdogo Sasa hivi tunapigia chepuo nishati safi kuacha kutumia mikaa na tunapigia chepuo LPG ambayo tunaagiza, kitu ambacho tunatumia fedha za kigeni; wakati tungeweza kutumia umeme katika kupikia hence kuondoka na matumizi hayo...
Baada ya kuona kwenye Habari Serikali imeanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia nikaona ni vema tuangalie kwa nchi Yetu Nishati hio ni ipi na ni vipi itatufaa, ili tusije kuingia gharama ambazo zitakuwa hazina manufaa kwetu. Nishati zilizopo: Kwenye kila kaya aina ya Nishati inayotumiwa...