Binafsi naona serikali aijaweka kiupambele swala la wafugaji kama sector ya kukuza uchumi wa ndani na nje kuna changamoto nyingi kubwa zaidi ni ukosefu wa elimu kwa wafugaji sjaona serikali ikiweka mpango mkakati wa kuweka wataalamu kuwaelimisha wafugaji ufugaji wenye tija mfano jinsi ya kupanda malisho ,kupunguza idadi kubwa ya wanyama katika eneo moja au athari za kimazngira zinazosababishwa na overstocking /overgrazing
Pili kuna ukosefu wa breed za ngombe wa nyama wenye tija ukiangalia ngmbe wa mmasai anatumia miaka mingi kufikia uzito wa kuchinjwa ambapo aileti faida zaida yankuaribu mazingira .
Tatu ukosefu wa malisho wa kutosha pamoja na kua na ardhi kubwa hapa tz lakini bado kuna changamoto ya uhaba wa malisho hasa kipindi cha kiangazi matokea yake kunakua idadi kubwa ya vifo vya wanyama kila mwaka
Mwisho naweza kusema wafugaji wangepatiwa elimu juu ufugaji wa kisasa na kuachana na ufugaji wa zamani wajue kupanda malisho mbali mbali kwenye maeneo yao ili kupunguza kuhama hapa na pale kufuata malisho hata pia jinsi ya kutunza vyanzo vya maji ,kuzalisha malisho na kuyastore kama silage na hay kuhakikisha upatikanaji wa tiba za wanyama pia
Bwana
salmin siraj Mimi napingana na wewe. Serikali imefanya mengi tu kwenye sekta ya kilimo na ufugaji. Miradi ya ASDP ipo tangu miaka ya 2008 kuwaelimisha kilimo na ufugaji wa kibiashara. SAGCOT, MIVARF yote imekuja miaka takribani 10 iliyopita. Kuna mabwana mifugo kila halmashauri mpaka kwenye majiji. Kuna kata Zina bwana/bibi mifugo. Ulitaka serikali ifanye nini la ziada?
Tangu enzi na enzi (ukiacha mwaka Jana 2021) huwa Kuna maonesho ya nanenane, unajua lengo lake ni Nini??
Pale kuna wakulima wakubwa na wadogo, wafugaji wakubwa mpaka ranch, Kuna vyuo vya kilimo na ufugaji, Kuna VETA/SIDO. Pale unakuta mbegu Bora za ng'ombe, mbuzi, kondoo, kanga, Bata, hata malisho. Shamba la mifugo la Mafinga wanazalisha mbegu za nyasi nzuri kwa ajili ya malisho, uliwahi kuzitafuta ukakosa?
Mfugaji gani anazitafuta elimu anaikosa?
Mimi mwenyewe nimewahi kwenda kuonesha ufugaji wa Bata bukini pale John Mwakangale Uyole nikanunua na mbegu za lucina.
Swali ni je Hawa wafugaji wanahudhuria sehemu kama hizi?
Wafugaji wanawekeza kwenye elimu?
Acheni Lawama za kipuuzi. Ngozi nyeusi wengi hatuzingatii maarifa na technology. Tunafanya ili mradi. Hata umwelimishe vipi anarudia Mambo yake vilevile. Unless soko limwekee masharti ndipo atalazimika kuyafuata mfano kwenye tumbaku na Parachichi.