Nini huathiri ukuaji bora wa ng'ombe wa nyama? Nini kifanyike?

Nini huathiri ukuaji bora wa ng'ombe wa nyama? Nini kifanyike?

Chukua sample ya wafugaji ishirini kawaulze wamehawahi kutembelewa na maafsa mifugo kwenye maeneo yao mfano mdgo juzi mweshimiwa Makanu wa raisi alisema ajawahi kuona afsa mifugo akitembelea shamba lake achana na hivo kila wilaya kuna eneo kama hapo mafinga linalowafunza watu kupanda malisho mbalimbali jibu ni bado fuatilia nchi zetu jirani serikal zao zinawapa suport sana wafugaji
Bwana salmin siraj Mimi napingana na wewe. Serikali imefanya mengi tu kwenye sekta ya kilimo na ufugaji. Miradi ya ASDP ipo tangu miaka ya 2008 kuwaelimisha kilimo na ufugaji wa kibiashara. SAGCOT, MIVARF yote imekuja miaka takribani 10 iliyopita. Kuna mabwana mifugo kila halmashauri mpaka kwenye majiji. Kuna kata Zina bwana/bibi mifugo. Ulitaka serikali ifanye nini la ziada?

Tangu enzi na enzi (ukiacha mwaka Jana 2021) huwa Kuna maonesho ya nanenane, unajua lengo lake ni Nini??
Pale kuna wakulima wakubwa na wadogo, wafugaji wakubwa mpaka ranch, Kuna vyuo vya kilimo na ufugaji, Kuna VETA/SIDO. Pale unakuta mbegu Bora za ng'ombe, mbuzi, kondoo, kanga, Bata, hata malisho. Shamba la mifugo la Mafinga wanazalisha mbegu za nyasi nzuri kwa ajili ya malisho, uliwahi kuzitafuta ukakosa?
Mfugaji gani anazitafuta elimu anaikosa?

Mimi mwenyewe nimewahi kwenda kuonesha ufugaji wa Bata bukini pale John Mwakangale Uyole nikanunua na mbegu za lucina.

Swali ni je Hawa wafugaji wanahudhuria sehemu kama hizi?
Wafugaji wanawekeza kwenye elimu?
Acheni Lawama za kipuuzi. Ngozi nyeusi wengi hatuzingatii maarifa na technology. Tunafanya ili mradi. Hata umwelimishe vipi anarudia Mambo yake vilevile. Unless soko limwekee masharti ndipo atalazimika kuyafuata mfano kwenye tumbaku na Parachichi.
 
Chukua sample ya wafugaji ishirini kawaulze wamehawahi kutembelewa na maafsa mifugo kwenye maeneo yao mfano mdgo juzi mweshimiwa Makanu wa raisi alisema ajawahi kuona afsa mifugo akitembelea shamba lake achana na hivo kila wilaya kuna eneo kama hapo mafinga linalowafunza watu kupanda malisho mbalimbali jibu ni bado fuatilia nchi zetu jirani serikal zao zinawapa suport sana wafugaji
Sasa mkuu, wewe ni mkulima unataka uzalishe kwa wingi halafu unasubiri Afisa Mifugo akufuate shambani akubembeleze, hii inaingia akilini?
Unaulizia Shamba la malisho Mafinga ndiyo lipo barabara ya kuelekea Sawala. na ukitaka mbegu za nyasi unapata mwaka mzima. Narudia Tena, huwezi kuzitafuta elimu ukaikosa, ukisubiri ufuatwe basi endelea kusubiri.

Siku hizi Kuna mpaka makampuni binafsi ya ushauri wa kufuga. Ranch zimetenga mashamba ya kufuga ndani ya ranch hata pale Ruvu, mpaka ranch ya Kibirizi Karagwe bado Wafugaji hawaendi. Hakuna anayekatazwa kuwa na Shamba lake la malisho lakini bado.
Btw walete hao wafugaji wanaohitaji elimu hawajui pa kuipata nami nitawaonesha
 
salmin siraj Idrissou02 wengine hao, hapo unapata elimu mpaka unacheua. Unapata mbegu Bora na kila kitu kinachohusu ufugaji. Elimu haikufuati, wewe ndiye unaifuata elimu.
Nothing worth comes free! Acheni kujifungia na Lawama hazikufikishi popote.
Screenshot_20220226-185902.jpg
 
Back
Top Bottom